Rais Magufuli, hili la Kangi Lugola hujatenda haki. Sheria ya Uhujumu Uchumi inawahusu wananchi tu?

Rais Magufuli, hili la Kangi Lugola hujatenda haki. Sheria ya Uhujumu Uchumi inawahusu wananchi tu?

Kwa Masikitiko Makubwa Kabisa!

Japo Waziri wa Mambo ya Ndani aliamua kujitoa akili na kuonesha Immaturity mbele ya kadamnasi kwa kuongea vitu ambavyo kimsingi alikuwa akijielewa mwenyewe.

Hata hivyo, halikumzuia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Rais Magufuli kuzungumza madudu ya Wizara ya Kangi.

Sitting Allowance dola 800, plus perdiem, en plus tiketi za ndege pamoja na refreshment;

Sambamba na hilo kilichosainiwa kwenye Mkataba wa Maridhiano (MoU) ni kuwa hata mkataba ukivunjwa lakini huduma ambazo zimeshaanza kutolewa basi zitaendelea kutolewa kwa kipindi chote.

Aidha, Thamani ya Mkataba ni zaidi ya 1T.

Je huyu Waziri, Naibu Waziri, Katibu, Kamishna wa Zima Moto pamoja na Maafisa wa Mwanasheria Mkuu ambapo Mikataba yote yenye thamani kubwa inayohusu Manunuzi ya Umma lazima ipite kwa Mwanasheria Mkuu kwa ajili ya kuhakikiwa terms and conditions ndio isainiwe , je wanapaswa kweli kuendelea kuwa Uraiani?

Nilitegemea kuona Gari la Magereza likimbeba pale pale bwana Kangi pamoja na timu yake kuwapeleka mahabusu.

Ukweli , Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi Taifa hii tumbua tumbua bila ya hatma ya kisheria juu ya hawa watu kujulikana inakuwa haisaidii. Na ndio maana haya matukio hayaishi. Kwa sababu hakuna liquidated damage upon specific breach pindi wakifanya madudu.

Wizara imekiuka Public Procurement Act ya Mwaka 2011 reads together with its Regulation ya Mwaka 2013 , following its amendment ya Mwaka 2016 !

Hivyo, ana sababu zote kuwa punished kisheria yeye na timu yake wakalale mahabusu; tofauti na hapo hakuna haja ya tumbua tumbua.

Tunataka kuona hawa watu wakichukuliwa hatua za kisheria kama ifuatavyo;

1. Kwenda Mahabusu
2. Kuchukuliwa Hati ya kusafiria
3. Freeze Akaunti zao zote
4. Filisi mali zao zote
5. Wanyongwe kama wafanyavyo China.

Sitting Allowance dola 800: Halafu still tunasikia hali mtaani ni ngumu, watu hawana hela, kumbe fedha zipo kwa wachache.

Hili pia ni lako ewe Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa kujitafakari kuwa ni kweli Ufisadi kwenye Taasisi za Umma umekwisha au unafanyika lakini ni kwa kificho?

Mwisho, zifuatazo ni taasisi ambazo unatakiwa kuwaambia vijana wako wazitembelee hizi taasisi kwa uchunguzi zaidi;

1. PPP project ya Mwendokasi
2. NSSF na nyumba za Kijichi, tunajua Serikali ilikuwa na Hisa ndogo katika mradi huu, lakini cha kushangaza Serikali ndio iliyotoa Bilions of money kuliko kampuni Binafsi
3. Bohari Kuu ya Dawa chini ya Wizara ya Afya- Tulisoma Ripoti ya CAG inayoeleza upotevu mkubwa wa pesa za Dawa za wànanchi pasipokuwa na nyaraka yakinifu.Hapa rushwa ipo mno
4. NIDA ikiwa ni pamoja na Utendaji wao
5. TTCL hawa hasa kwenye huduma zao na kuna viashiria vya Rushwa vingi sana
6. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
7. Bodi ya Mikopo

Asante!
Kukosoa serikali ya mwenyekiti wako ndo uhujumu uchumi,hiyo ya lugola si pesa ya kiwi tu au umesahau kama kangi ni police mstafu
 
Mie naona General mstaafu ndio kachoma utambi, inaonekana kumetokea sintofahamu, General kampandia mkuu ofisini kamwaga kilakitu na resignation juu, labda alimtishia kuwa anarudi lugalo, akaona isiwe tabu, manake yeye kalamba ubalozi.

Kangi inaonekana kapigwa katafunua, yaani nyani usimwangalie usoni, hakutegemea ataenda kukumbana na kadhia ile asingeenda mkutanoni.

Romania niwatengenezaji wa magari mazuri ya zimamoto aina ya Magnus pia ndio watengenezaji wa bidhaa Bora za kuzimia Moto. Chamsingi mkataba upitiwe upya nakuweka mambo sawa.

Nashauri hapo mambo ya ndani atafute jembe jingine kutoka jeshini, mie napendekeza major general Makakala balozi wetu Zimbabwe.
Usonji unamsumbua, angalau angetumia akili kumlinda informer wake huyo mwanajesshi, lakini akili hiyo hana anam-expose
 
Mwite P,labda anaweza kuondoa huu ukakasi
Tumemsikia wenyewe Rais wetu, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, alipokuwa akitengua uteuzi wa waziri wa mambo ya ndani, Kangi Lugola, akitoa sababu kuwa ni kutokana na waziri huyo kusaini mkataba nje ya nchi, wa kuingiza vifaa vya zimamoto, vyenye thamani ya zaidi ya shilingi trillion moja

Kama madai ya Rais Magufuli ni ya kweli, ni kwanini Jeshi la Polisi nchini halijamkamata Mheshimiwa Lugola na kumfungulia mashitaka ya utakatishaji wa pesa nyingi kiasi hicho?

Tunajua kuwa yupo mwandishi wa habari, Eric Kabendera, anayeendelea kusota rumande, kwa zaidi ya miezi 6 sasa, kwa tuhuma za utakatishaji pesa wa shilingi milioni 170

Tunajua pia yule mfanyakazi wa kituo cha haki za binadamu, Tito Magoti, naye amefunguliwa mashitaka ya utakatishaji pesa wa shilingi milioni 17 pekee!

Inakuwaje kwa hawa akina Lugola, ambapo kwa Maelezo ya Rais wetu Magufuli, amewatuhumu kushiriki kusaini mkataba wa kununua vifaa vya thamani ya zaidi ya shilingi trillion moja, waeendelee kukaa uraiani, ambapo Rais mwenyewe ametuhakikishia kuwa wanahusika na utakatishaji pesa wa zaidi ya shilingi trillion moja?

Hivi ni kipi kikubwa ni trillion moja ya Kangi Lugola au shilingi milioni 17 za Tito Magoti?

Kama Kangi Lugola hajafunguliwa kesi ya utakatishaji pesa basi tutajua kuwa hili suala ni la kisiasa

Tusaidiane katika kulidadavua suala hili kwa maslahi mapana ya Taifa letu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu haya ni wachache tu wanaelewa hakuna nchi rahisi kuongoza kama Tz

Sent using Jamii Forums mobile app

IMG_1264.JPG


Tuone mwisho wa hili suala ; je wataenda Rumande
 
Usanii mtupu. Ila muda ndiyo utakaosema ukweli. Mnamhoji aliyekuwa Katibu Mkuu wakati Mkuu wa nchi alishamsafisha? Je ni nani atakaekwenda kinyume na maamuzi yake? Ndio maana nasema huu ni usanii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usanii mtupu. Ila muda ndiyo utakaosema ukweli. Mnamhoji aliyekuwa Katibu Mkuu wakati Mkuu wa nchi alishamsafisha? Je ni nani atakaekwenda kinyume na maamuzi yake? Ndio maana nasema huu ni usanii.

Sent using Jamii Forums mobile app

Cha Ajabu Kangi kaenda Takukuru akiwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi! Je ni nini tafsiri ya hii kitu?

Je anamaanisha alichokifanya ni moja ya sehemu ya Ilani ya CCM?

Inawezekana kapelekwa huko baada ya wananchi kupiga kelele; All in all let’s see the culminating result of this marathon.
 
Back
Top Bottom