Rais Magufuli: Huduma za NIDA ziwe kila Wilaya au NIDA watoe hela ya 'guest' kwa Wananchi. Ukiona bei ya mahindi iko juu, kalime yako

Rais Magufuli: Huduma za NIDA ziwe kila Wilaya au NIDA watoe hela ya 'guest' kwa Wananchi. Ukiona bei ya mahindi iko juu, kalime yako

Rais Magufuli amesema serikali haiwezi kuwapangia wakulima wa mahindi bei ya kuuza mazao yao kwa sababu haikuwasaidia wakati wanalima.

Rais Magufuli amesisitiza kuwa wakati wa serikali kuwapangia wakulima bei za mazao yao umepita na hizi ni zama za soko kuamua.

Source Eatv habari!
Hii ni sera ya CCM ama ni yake!!
 

Rais Magufuli amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dkt. Arnold M. Kihaule kufika Mkoani Morogoro leo na ikiwezekana akae Mkoani humo hata siku tatu ili kushughulikia tatizo la Watu wengi kukosa Vitambulisho vya Taifa huku Mkoa mzima ukiwa na ofisi moja pekee ya NIDA.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo pamoja na kuzungumzia masuala mengine mbalimbali wakati akiongea na wananchi wa Msamvu, Morogoro akiwa njiani akielekea mkoani Dodoma.

Kuhusu usajili wa NIDA, Rais amesema:

"Mkurugenzi ondoka sasa hivi Dar es Salaam uje hapa Morogoro kushughulikia hili tatizo la NIDA, Nimemtaka Mkurugenzi Mkuu NIDA aje ashughulikie changamoto ya vitambulisho na nataka huduma hii iende kila Wilaya, haiwezekani watu wasafiri kutoka Wilayani kuja Mjini au muwape nauli na hela ya ‘Guest’,na hili litazamwe nchi nzima watu wapewe vitambulisho”

''Leo uje hapa ukae na mkuu wa mkoa na wilaya muangalie namna ya kuseti namna ya kutoa huduma hizi kwa wananchi hawa. Na hili liwe pia kwa Tanzania nzima. Inawezekana matatizo haya hayapo hapa Morogoro tu''

''Hatuwezi kucheleweshwa na watu fulani fulani kwa kushindwa kufanya majukumu yao na kuharibu majukumu ya wananchi kushindwa kufanya kazi zao huko''

“Watu wanataka kusajili laini zao za simu na mambo mengine lakini zoezi la vitambulisho linacheleweshwa na watu wachache; suala la NIDA linaenda polepole sana. Mkurugenzi Mkuu wa NIDA nitahitaji unipe na tathmini ya zoezi lote Nchi nzima"

Kuhusu wakulima na wafanyabiashara, Rais amesema:

“Wanaofanya biashara ndogondogo nilishasema wasionewe ndiyo maana nilitoa vitambulisho. Nilisema mfanye biashara mahali popote lakini sikusema wapiga debe na wazuluraji waendelee kuzulura tu, kuna sheria na mimi nimeapa kulinda sheria"

“Nataka wakulima washangilie kama bei ya mahindi imepanda, biashara hii lazima iwe huru, bei ya mahindi itajipanga yenyewe, wakati wa kuwapangia bei wakulima kwenye mazao yao umekwisha”

‘’Morogoro Ilikuwa ni mmoja kati ya mikoa muhumu sana katika uzalishaji. Viongozi wa Morogoro mukawahamasishe watu kufanya kazi ili mkoa uendelee na sifa yake ya siku zote’’

"Ukiona wengine wachache wanalalamika bei ya mahindi iko juu, najua wakulima wanashangilia, na nataka wakulima washangilie zaidi,tulizungumze hili wazi kwa watanzania wote,ukiona mahindi yako juu nenda kalime yako ya bei ya chini biashara hii lazima iwe huru"

“Wana Morogoro JPMMorogoro “Wana Morogoro nataka mtunze amani, navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kulinda amani yetu, kila mtu atimize wajibu wake katika eneo lake la kazi”

Kuhusu kamatakamata ya wazururaji, Rais amesema:

''Wapo wanaokamatwa kwa kosa la uzururaji na wanapopelekwa mahakamani wanashindwa. Kwanini wasishinde kule mahakamani kwamba siyo wazururaji? Wapo waliojitetea mahakamani wakashinda, sasa hao waliofungwa kwa uzururaji munataka niwarudishe?''

''Wale wanaofanya biashara ndogondogo wala wasionewe ndiyo maana nikatoa vitambulisho. Sikusema wapiga debe, wazururaji waendelee kuzurura tu – kuna sheria na mimi nimeapa kulinda sheria.''

''Niviombe vyombo vya usalama vinavyo-deal na wazururaji, wasiwaonee watu kwa kuwashitaki kama wazururaji wakati wana kazi zao. Haya ya uonevu yasiwepo.''

‘’Wale ambao siyo wazururaji musiwaonee, muwaache wafanye kazi zao.''

AKIWA WILAYANI GAIRO


Akiwa Gairo, Rais Magufuli amechangia shilingi milioni 5 kwa ajili ya kujenga maabara ya Shlue ya Sekondari Sekwawa baada ya kaka Mkuu wa shule hiyo Athumani Saidi Omari kufikisha ombi la kuongeza ukubwa wa maabara hiyo ambayo amesema haitoshi.

‘’Changamoto kubwa inayaotu-cost wanafunzi wako ni maabara haitoshi’’, alisema Kaka Mkuu huyo

Rais Magufuli: ‘’Nitachangia milioni tano kama mchango wa kujenga maabara; nakabidhi milioni tano kwa ajili ya ujenzi, ikiliwa na nyie mujiandae kuliwa’’

Mkuu wa Wilaya Gairo: ‘’Hakuna mahakama ya wilaya, wanaenda Kilosa, zaidi ya kilomita 100. Hakuna ofisi ya Mkuu wa Wilaya, nimejishikiza katika ofisi za Mji Mdogo. DAS ana-share ofisi na Afisa Tarafa.''

Rais Magufuli, Tembea, ongeza gas, kasi, bila wasiwasi.

Muhimu sana kutowaonea wanyonge, maskini, mtu yoyote.

Pia kuwasaidia vijana kupata kazi. Tusiwaweke jela. It doesn't make sense, tujaribu kuwasaidia kupata kazi.

Elimu yetu tuiiangalie. Iko sawa kwa karne hii, mahitaji, kuwatayarisha vijana kujiari, kupata kazi?
 
Unaonekana ww ni wale wasomi uchwara mnaokaa mjini, mkulima wa kawaida analima zao analolimudu kulingana na mazingira yake. Matarajio yake ni kuuza ziada ya mazao yake. Huo muda wa kutsget soko gani ni kwa mtaji gani alio nao?
Asante
 
Hhahaah baada ya kuharibu soko la korosho, Bangi sorry tumbaku, Mahindi etc ndio anakuja na huu msemo saa hizi?? Hongera sana san aserikali ya awamu ya Tano
Haitoshi, vijana wamezagaa mjini wanauza soksi. umetoka job unataka kupumzika sehemu unaona kundi la vijana aged 15- 30 wanakuja kundi as if wanakuvamia alaa kumbe wachuuzi...kila mtu na kiroba chake...

Hawa wanatakiwa wawe mashambani wakizalisha....hawa wanatakiwa kuingia ubia na Serikali...Serikali inatoa resources wao ni NGUVU KAZI...umri wao unarihusu...

Hii kauli haitoshi...ondoa hawa vijana mjini wakafanye kazi huko mashambani watajirike...weka utaratibu mzuri wa uzalishaji na masoko... hela ya Dreamliner moja tu unawabadilisha hawa vijana kabisa kabisa..!!
 
Nawaangalia
Halafu Nasema Hii Bhaghoshaa 😁😀😂🤣😃😄
 
Wanaopiga kelele ni CHADEMA kwani hawataki kulima kabisa Wanataka kushinda humu wanatukana kalimeni mahindi hayashuki bei mpaka mkalime na nyinyi.
 
korosho alitetea wakulima kuwa underpaid.
Mazao mengine anaopinga wakulima kupangiwa low prices na system.
Kwa wenye akili timamu tunajua anazidi kumtetea mkulima wa korosho na wa mazao mengine.
Hivi kwa wanaoijua korosho vizuri mtujuze hili zao LA shamba au kiwandani.Mi nilidhani ni zao LA shambani nikataka kujiuliza Inamaana anajipinga operation yake ya korosho?
 
Na kahawa ya Kagera kuuzwa kwa Waganda kwa Bei nzuri kuliko ya vyama vya ushirika ameruhu au tusubiri mwongozo kipindi Cha kampeni 2020.
 
Mkuu tumshauri aongeze nguvu kazi
Maana ofisi za nida kila wilaya zinaupungufu wa rasilimali watu
Ni siasa tu. Tatizo analijua sana. Alianza kumkosoa Jakaya kuhusu Vitambulisho lakini hakuna kubwa alilofanya kuendeleza.
Hawapi hela. Kila kitu ni madege na upuuzi mwingine.
 
Back
Top Bottom