Uchaguzi 2020 Rais Magufuli jipime umwachie Membe, Lissu atakuangusha mapema sana

Nilichogundua wapiga kura wanaomtaka Lissu hawataki Lissu ashindane na Magu ila wanatamani Lissu ashindane na Membe!
 
Lissu amekuwa akiwatetea watanzania hata kabla ya Magufuli kuanzia miaka ya 2000 uko.
Hahahhaa miaka ile ya Nyamongo na Bulyanhulu, aliwatetea kwa pesa zake na kwa muda wake bure!! wakati huo Mwenyekeiti akiwa Bungeni akipiga makofi tu. Nanio mwenye ile speech ya Lissu?
 
Siku zimeendelea sana na mambo yanabadilika kwa kasi ya ajabu. Zamani watu walikuwa wanaota ndoto usiku wakati wamesinzia, siku hizi mtu anaota ndoto mchana kweupe, mbuzi wanakula majani! Eti TL anamzidi JPM?
 
Ulicho andika hapa ni dhihaka au ndio akili yako ionavyo ? Mbona kinyume kabisa na ground? Magufuli kwa sasa ni mtu maarufu sana yawezekana mbali ya ndani ya nchi hata njee ya nchi kwa Afrika. Mjitahidi sana japo kuweka ka ukweli kidogo ili mtengeneze heshima. Sisi wengine tumekuwa Chadema kwa miaka 18 kwa hiyo mapungufu yetu sasa hivi nayaona kwa uwazi sana.
 
Wewe mtafuta ubunge njoo nakusubiri huku Mwanga na naweza kukupa msaada sana kuanzia tarafa ya Kilomeni, Usangi, Kirongwe, Shinghatini, Kikweni na eneo la Kirya.

Maeneo yaliyo baki ni ya mjini matapeli wa kisiasa wengi sana. Yaani watadai hela na suala la kupigiwa kura sahau.
 
Nilichogundua wapiga kura wanaomtaka Lissu hawataki Lissu ashindane na Magu ila wanatamani Lissu ashindane na Membe!
Sio Lissu tuu, yaani kwa ujumla Chadomo wanamogofya Mkulu, hawataki kabisa awepo kwenye wagombea Urais wa CCM. Japo wengine wanaweka wazi.
 
Kamanda hapa umetuvua nguo sisi makanda wenzako, hizo ngonjera zako siyo msimamo wetu, tafadhali.
 
Nakuja aiseee, week ya kwanza ya July 2020 nitakua Usangi, nakuja Mpwa, Shukrani sana
 
Dalili ya uoga hii
Si umuache lissu aingie mchezoni?
Pia mshauri Membe achukue fomu kupitia CHAUSTA nae agombee kama kweli anao ubavu
Atagombeaje CHAUSTA wakati chama chake ni CCM?
Uliwahi ona Shehe anagombea uongozi CCT?
 
Ni vyema tukabadilika na kutambua kuwa Demokrasia halisi hailetwi kwa kumtegemea mtu moja kuwa ni hodari na anamaamuzi ya mwisho katika taasisi.
Chama cha Siasa ndiyo chenye mamlaka ya kuchagua mtu wa kugombea U rais na akishinda bado atatakaiwa keteleleza sera za chama chake na wale si sera zake.
Mgombea ambaye hatokani na mfumo imara uliomchagua na ambaye anatawala huo mfumo wa kuchagua mgombea wa U rais, hafai kuongoza Inchi.
Vyama vyetu vya Upinzani bado ni mali ya Waanzilishi na wameingia gharama kuvianzisha kwa hiyo mwisho wa siku wakichukua madaraka watataka kurudisha gharama zao na faida juu.
Inchi itauzwa.
Kwa mfano, Lowasa alipochaguliwa na CHADEMA kugombea Urais, haikuwa bure, aliingia gharama kubwa katika kupata ile nafasi na katika kampeini.
Je kama angeshinda urais nini kingetokea katika swala Zima la pesa alizotumia.
Tundu Lissu na wengine wanaweza kuwa wazuri sana lakini wakawa wako kwenye taasisi au vyama vibovu sana na kwa hiyo na wao wakawa hawafai kuongoza Inchi.
 
Mbatia namwelewa zaidi kuliko chadema siasa zake za kistaarabu
 
Mpaka sasa hakuna wa kushindana na JPM. Akitokea tutamuona kama taahira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…