Uchaguzi 2020 Rais Magufuli jipime umwachie Membe, Lissu atakuangusha mapema sana

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli jipime umwachie Membe, Lissu atakuangusha mapema sana

Lissu huyu wa "MIGA"
Hivi yale makontena ya mchanga bado yapo pale bandarini? au tulinyoosha mikono baada ya kulipwa tr 400 tunapewa bil 600 tena kwa mkataba wa miaka 5 kama mazuzu mnashangilia!
 
NAUSAPOTI UPINZANI KWA SANA ILA SIJAONA KAMA WAKO TAYARI KUSHIKA NCHI
Hakika, na ndio wanasababisha ccm watawale kwa muda mrefu.
Hakuna mpinzani au upinzani thabiti TZ, huyu anayepigwa kila siku na akiamka anaomba maridhiano, kwenye sherehe za ccm yuko kiti cha mbele kujichekeshachekesha hawezi kuaminika kama ana nia thabiti.
Ni afadhari ACT Wazalendo wako siriaz kidogo sana. Tatizo wako upande mmoja wa tz na wenye raia wachache.
Huyu akiamka tu hospitari anaanza kuishukuru ccm na fikra za mwenyekiti hamna kitu kabisa.
 
Mkuu mwanzoni mwa Mada nawaona mataga wametiririka kwa kasi sana.
 
mali zipi zingine zaidi ya gesi kikwete aliyompa mchina?
IMG_20200610_123732_867.jpg
 
Ukweli mchungua Lissu ni maaarufu sana kuliko Magufuli, Lissu amesoma na kuelimika kuliko Magufuli, Lissu anaijua Tanzania na tatizo la nchi hii kuliko Magufuli, Lissu anaijuwa siasa ya ndani ya Tanzania na nje kuliko Magufuli, Lissu hana hata tuhuma moja ya ufisadi kama Magufuli.

Lissu anaelewa mizizi ya ufisadi wa taifa ili kuliko Magufuli, Lissu amekuwa akiwatetea watanzania hata kabla ya Magufuli kuanzia miaka ya 2000 uko.

Muda bado upo angalau ungemuachia Membe au Makamba angalau wangejenga hoja, Ila ukiendelea kutumia nguvu kupambana na Lissu utaenda Chato na mwenzio ataenda Ikulu.

Ukitaka kushinda jenga hoja ila kwa kutumia nguvu utaanguka na wapambe watakukimbia hakuna watu wanafiki kama watanzania hasa wapambe wa rais.

Mkuu Kwanini unapenda ku promote your stupidity. Kama wanastahili usingekuwa na haja ya kuandika.
 
Mapema asubuhi Membe anachukua nchi akishindanishwa na jiwe.
 
Mmeamua kumchafua tu, lakini Lissu ni Messiah hata Herrord afanye nini maandiko yatatimia.
Kwa suala la haki za binadamu atatusaidia, hasa kupigania haki za wanawake kama kina Bulaya, Halima, watoto sio Riziki lakini kwa Urais bado sana.
 
Rais magufuli anavyochukua form ni kwamba ameona jeraha alilotupa miaka5 halitoshi au?mpaka anaamua kulitia chumvi.
 
Chadema huwa wanapenda kutishia nyau
Afadhali hata ya lema anaweza kupata kura
Huyo lissu huo urais ataupataje wakati ameamua kujilipua?
Mlimpiga marisasi Mungu Baba akamponya, sasa tulia kampeini ianze uone mziki wa TLissu!!
 
Rais magufuli anavyochukua form ni kwamba ameona jeraha alilotupa miaka5 halitoshi au?mpaka anaamua kulitia chumvi.
Amejuruhiwa nini? Kuendesha siasa bila ustaarabu? au Ulitaka awe kama Kikwete? kila aingiae madarakani ana utaratibu wake wa kiutawala.
 
Mzee leo amekumbushwa kwamba alikula kiapo. Naona anasahau. Maandiko yanasema usiape kwa kitu chochote. Ukishafanya hivyo, kiapo kile kitasimama mbele yako daima. Na kila kiapo kina madhara yake ukienda kinyume
 
hapa alipita tu kukagaua ujenzi wa fly over wamejaa ivi, akianza kampeni itakuaje
1593202735774.png
 
Katika kusoma Biblia Takatifu, agano jipya bila kunukuu injili husika na aya zake, Wakati ule Yesu Kristo ameshitakiwa na Mayahudi kwa Herodi na Herodi kumwona hana hatia, lakini Mayahudi walilazimisha asulibiwe.
Herode, kulingana na mila na Desturi za Kiyahudi, siku ya Pasaka alikuwa anaruhisiwa kumsamehe mfungwa au mtuhumiwa moja. Herodi aliwaambia Mayahudi kuwa amemsamehe Yesu kulingana na madaraka aliyopewa. Mayahudi yalipiga kelele na kusema Mtoe Baraba ambaye alikuwa jambazi sugu na Yesu asulubiwe.
Yesu pamoja na kutokuwa na hatia lakini alisulubiwa na Baraba aliachiwa huru.
Mh. Dr, Rais Makufuli hana hatia na ameifanyia Inchi mambo ambayo ni nadra kwa kiongozi wa Inchi
kuyafanya lakini kwa hulka ya Binadamu atasema asulubiwe.
Tutafakari falsafa za Kitaaluma.
Rais wetu ni Mwanasayansi.
Hulka ya mwanasayansi yeyote Duniani ni Kujenga, kuunda na kukabati/kukavati.
Mchumi na Mwanasiasa hulka yake ni kutafuta kuwafurahisha watu na kupigiwa makofi.
Mwanataaluma ya fedha ni kuweka akiba na mwoga kuingiza pesa kwenye ujenzi au mali za kudumu.
Tulipofika Watanzania, ulikuwa wakati mwafaka kumpata Rais Mwanasayansi ili aijenge Inchi yetu kwa
sababu ilifika mahali kama tungeendelea na uongozi tofauti na huu Inchi hii isingefaa kuishi hasa sehemu kama Dar.
Dar imebadilika kwa kujenga fly overs na kupunguza msongamano
Makao makuu yamehamishiwa Dodoma na kupunguza msongamano huko Dar.
Railway ianaimarishiwa.
Nishati ya umeme inaimarishwa.
Bara bara za lami zinaongezeka
Bandari inaimarishwa.
Makusanyo ya kodi yameongezeka kwa kiasi kikubwa na pesa inatumika vizuri
Ufisadi umekomeshwa.
Nk.
Tumuunge mkono Rais huyu wa kipekee ili atimize ndoto zake kwa manufaa ya Watanzania.
Wale wanaomsuta sasa wakumbuke kuwa siku za usoni jina lake litakuwa LULU kama la Mwalimu Nyerere.

unapoteza mda kuwaandikia hawa majamaa, ukweli unajulikana na upo wazi: yaani ukitaka kujionea kituko subiria mda wa kampeni utaona uzito wa mgombea, hapa wanakasirisha watu tu yaani wanachama wao wenyewe hawaikubali cdm wanahamia ccm , sasa iweje ambao tupo ccm tuwakubali.
 
Taifa pamoja na mengine linahitaji prestigious katika mambo yake. Rais ndio icon ya nchi ndio maana kauli na matendo yake yanalindwa kwa gharama kubwa sana. Sasa aibu kama hizi huko nje ya nchi mpaka lini? Hatutaki tena, kushindwa kuelewa swali na kujibu swali hizo ni level za katibu kata sio Rais.
Tunataka atakaye simama kusema jambo au kujibu iwe Tanzania imejibu. Jee hapa kuna mtu anaweza kusema Tanzania imejibu zaidi ya kusema atajijua?



sasa aibu gan? ENGLISH isnt our language, mbna china hawatumii english??? what are you talking about
 
Back
Top Bottom