Uchaguzi 2020 Rais Magufuli, kama kweli ni mcha Mungu basi muombe radhi Halima Mdee na watu wa Kawe kwa uliyosema hadharani maana uligusa maisha ya watu

...yani hii clip inatakiwa itumike kwenye mikutano yote iliyobaki ya Lissu na Mdee ...watumie njia anyotumia Lema ya kuweka clip yote kwenye maspika makubwa wakati wa mikutano...na kuijadili kwa kina huku wananchi wakisikiliza kwenye maspika makubwa.....

Hili jambo linatakiwa likemewe kwa nguvu zote na lisipite hivi hivi...maana Halima na Lissu wote wameadhibiwa kwa tuhuma tu za kutokuwa wakweli kwenye matamshi yao...Sasa nao watume ujumbe kwa nchi kwa kuijadili hii clip kwa upana wake na nchi ijue.....
 
Umenikumbusha chuoni, hii ni course kabisa inaitwa adivocacy and lobbying, hata upige kelele kiasi gani wananchi wanachotaka kuona ni impact yq hizo kelelem
 
Lissu kamchanganya.
 
Lobbying sio mwenendo wa uadilifu. Ndio maana watu wa upamde huo kila baya kwenu ni halali. Maendeleo hayapelekwi kwa wananchi mpaka kufanyike lobbying? Ovyo kabisa.......!!!!
 
Waache tu mama hao walishaziba masikio kwa wapinzani, hizo barabara mbovu tutapita tu maana tumezoea.
 

 
Ulishaenda Ilala ukaangalia jinsi kulivyo? Kwahiyo Zungu naye alikuwa mahabusu? Rais Magufuli anatumia jukwaa kudanganya waziwazi kwenye maeneo ambayo yalikuwa yamekaliwa na upinzani. Mbaya zaidi uongo wake ni mbaya sana!
Nenda Mbgala na Temeke ndo utaelewa.
Mchukue n Halima ajionee.
 
Mdee miaka 10 haijakutosha tuuu.....nadhani imetoshaaa sasa hebu waachie wengine nao walete maendeleo ya vitu kwa watu wa kawe.
usilazimishe sana kimsingi mdee alipaswa kustaaafu kabisa ubunge ila wanasiasa tabu yao wanataka hadi akataliwe ndio aache.....miaka 10 utadhani hakuna watu wengine duh! halafu maendeleo yenyewe kiduchu! hayalingani hata na miaka 10!!
naona nyota sasa ni ya Gwajimaa, tuache naye apimwe na wananchi kwa miaka mitano tuone nini atafanya
 
Kwa hapo Rais, waziri husika, mkurungezi wa halmashauri husika na wenyeviti wa serikali za mtaaa ndo wakulaumiwa hakika mbunge amewakilisha matatizo ya wananchi wake bungeni.

HALIMA APEWE TENA MIAKA MITANO
 
Mkuu usiwe mshamba.
Wengine tumefika hadi Capitol Hill na kuonana na wajasiriamali na wabunge jinsi wanavyo canvass na kulobby kwa ajili ya issue za spheres zao.
Acheni usomi wa vitabuni, kama Halima, muwe practical.

Katika siasa kuna kitu inaitwa realpolitik, kutambua mpini uko wapi unaoweza kukusaidia.
Piga mayowe kama Halima, hilo linakuwa ushahidi tu kwa kuonyesha waliomchagua, kumbe hajafanya lolote na chochote cha follow up.
 
We baki huko makongorosi kawe haikuhusu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…