fundimchundo
JF-Expert Member
- Jul 23, 2010
- 739
- 1,032
Wanasheria watusaidie hapa.Rais Magufuli leo amewashukuru wananchi wa Kibamba kwa kumpa kura nyingi wakati wa uchaguzi mkuu na pia kuchagua mbunge na madiwani wote wa CCM.
Rais Magufuli amesema Kibamba wamejicheweshea wenyewe maendeleo kwa kushindwa kuchagua mbunge sahihi huko nyuma ambaye kwa muda wote amefanikisha kujenga km 5 tu za barabara ya lami.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa kufanya kosa siyo kosa ila kurudia kosa ndio tatizo hivyo amewapongeza wananchi hao kwa kumchagua Mtemvu wa CCM na amewaahidi ujenzi wa barabara zote jimboni humo.
Rais Magufuli amesema Mtemvu ni mnyenyekevu na kwa kuanzia amempa heka 52 za ardhi ili zitumiwe na wananchi wa kibamba kwa ujasiriamali na miradi yao mbalimbali.
J J Mnyika wa Chadema ndio mbunge mstaafu wa Kibamba
Source: TBC
Maendeleo hayana vyama!
Magufuli kukusanya kodi Kibamba kisha akawanyima maendeleo, kwa sababu ya kuwa na Mbunge wa Upinzani, Katiba yetu na Sheria za Kimataifa zinasemaje?
Kwa kuwa Magufuli hawezi kushitawa hapa Tanzania kutokana na kukosekana Katiba ya Wananchi, Wananchi wa Kibamba watapaje fidia ya kutozwa kodi kisha wakanyimwa huduma kama alivyosema mwenyewe Magufuli kuwa wamejichelewesha?