Tetesi: Rais Magufuli kupangua wakuu wa wilaya na wakurugenzi muda wowote

Tetesi: Rais Magufuli kupangua wakuu wa wilaya na wakurugenzi muda wowote

Baba Yetu uliye mbinguni,ufalme wako uje,utakalolifanyike huku Duniani kama huko mbinguni,Utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyowasamahe waliotukosea, utupatie riziki yetu,usitutie majaribuni bali utuepushe na yule mwovu shetani,

Umkumbuke na Tumbili Kafullila,Machali,Patrobas,Mwigamba,J Murro, Msando, Lemtusi, Afande Sele, Masha,Musiba, nami wa Mzalendo baba.
Kwa kuwa inawezekana kwa kila aaminiye
amen
Afanye huu uteuzi wa mamburura kama musiba atuongezee sababu za tarehe 260418
 
Rais wetu Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli alishamema hapangiwi na ukimpangia ndiyo hafanyi kabisa ulichopanga. Sasa wewe hizi porojo za mabadiliko umezitoa wapi?
 
Tatizo la hizi teuzi kujuana kwingi ni heri wakanipa hiyo nafasi mm hapa nina utaalamu nilioupata darasani ila napotezewa tu daah
 
Kama katika uteuzi huu Mtangazaji ' kimbelembele ' na bingwa wa ' kujipendekeza ' Bwana Hassan Ngoma akikosekana basi akaoge maji ya kutoa ' nuksi ' Kwao Makanya Upareni Mkoani Kilimanjaro.
Bila kumsahau Sam Mapene wa ITV
 
Wewe utakuwa unaogopa kuondolewa unakuja kuandika humu..
Naskia ndo mbinu zao cku hiz mtu akilikoroga anakimbilia kweny mitandao na kutoa taarifa kua safu flan ya viongoz itapanguliwa na wanajua Raisi hapendi kuvuja kwa taarifa ivyo anagairi..
 
Mi mwenyewe nautamani sana U-Dc, sema sijui anayeratibu upatikanaji wa majina,one day yes
Yaan mm mwenywe natamani ka ww alafu nipelekwe kule kweny madin ya tanzanite au pale kahama kweny madin niwe navaa mizahabu tupuuu
 
Muda wowote kuanzia sasa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania anatarajia kupangua wakuu wa wilaya na wakurugenzi nchini ikiwa ni pamoja na kujaza nafasi za wazi katika wilaya husika na halmashauri husika. Katika mabadiliko hayo vijana wengi na sura mpra zinatarajiwa kuingia.

Stay tuned....
Vijana wengi wametuangusha sana.Katika uteuzi wao uangalifu mkubwa unahitajika.Ingekuwa vema,hekima na busara kama wangewekwa kwenye lower positions kwanza halafu wakapandishwa pole pole ili wapate uzoefu kwanza na umri uongezeke mihemko ipungue.Wana pupa mno.
 
Back
Top Bottom