Uchaguzi 2020 Rais Magufuli lipa Mafao ya Wastaafu kabla ya Uchaguzi Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli lipa Mafao ya Wastaafu kabla ya Uchaguzi Oktoba 2020

Kulingana na report ya Ukaguzi ya CAG 2019/20 Serikali inadaiwa na Mifuko ya Jamii PSSSF kiasi cha zaidi ya Tshs. 700 Bilioni ambazo Serikali imekopa toka PSSSF na haijarudisha/kulipa fedha hizo.

Kuna Habari za kuaminika kwamba fedha hiyo imekopwa kwenda kujengea miradi mikubwa ya Serikali kama SGR na Stieglers Gorge(Bwawa la Nyerere).

Tunajua Bunge linamaliza muda wake na kuvunjwa June hii,2020. Kwa uhakika Wabunge na Mawaziri wote watalipwa mamia ya mamilioni ya Shilingi baada ya kulitumikia Bunge kwa miaka 5 tu!

Kinachosikitisha kuna wazee Wastaafu wamelitumikia Taifa hili kwa uaminifu na kwa miaka mingi kati ya 25~40 lakini mpaka sasa wengi wao hawajalipwa mafao yao tangu Wastaafu.

Wengine wana miaka 3,2,1 na wengine wana miezi kadhaa. Wazee hawa wanapofika PSSSF hupewa Majibu yaliyojaa visingizio vya uchelewesho wa malipo ya michango toka kwa Waajiriwa au makosa ya ujazaji wa fomu, majina au tarehe za kuzaliwa ilhali Ukweli ni kwamba Mifuko haina Fedha ya kuwalipa wazee hao.

Kama Hali itaendelea kuwa hivo Rais Magufuli ajue kuwa hatopata kura hata moja toka kwa hao wazee Wastaafu pamoja na familia zinazowategemea.

Wazee hao wamepigika sana hasa kipindi hiki cha Covic-19 maana hawana kipato chochote, hawana mishahara, hawana malipo ya pensheni na hawawezi kukopesheka popote.

Chondechonde Rais Magufuli toa maelekezo kwa Hazina ilipe Deni Hilo la PSSSF ili mfuko uwalipe Wastaafu hao wanyonge.
Hata asipowalipa hawana watalofanya
 
Hawa hata wasipopewa kabisa siwezi umia kabisa,

You're correct! You know what?
Mapoliccm wana maroho yaleyale yaliyoko Marekani yaliyo mwua George Floyd kwasababu za ubaguzi wa rangi tu!
Policcm Tanzania wanawaua Watanzania wasio na hatia kwa vile tu WAKO UPINZANI. Huu Ni ubaguzi Kama ubaguzi mwingine wowote...To hell with Tanzania Police Force under IGP Simon Zero brain!
 
Fedheha Ni pale mifuko inapokataa kumlipa mafao mstaafu sababu tu mwajiri (serikali) alikuwa hapeleki michango ya mstaafu huyo au pale ambapo mwajiri alimbadilishia mstaafu daraja na hivyo kutokumrekebishia mshahara.
Adha Ni nyingi na kibaya watumishi wengi wanaishi mbali na ziliko ofisi za Psssf. Kila Mara unspofanya ufuatiliaji hupati jibu la uhakika mbali ya kuambiwa, inashughulikiwa, network hakuna, file limesajiliwa, subiri mwezi ujao na majibu mengine mengi tu.
Kweli inaboa na Cha kushangaza wabunge wetu wako kimya Sana kuhusu Hili. Hakuna kiongozi mkuu wa kitaifa anayeguswa na mateso ya wastaafu. Hakuna bodi inayomwakilisha mstaafu. Maisha Ni magumu huku jamani
 
Onjwayo,
I can feel your expressions. Pole sana Mzee. Umeongea hoja mtambuka kweli hapa! Ni kweli kabisa Wastaafu hawana chombo cha kuwasemea na hao Wabunge wao wako Kimya Bungeni wakisubiri mafao yao tarehe 19/6/2020 Bunge litakapovunjwa na Jiwe!!
Ushauri kwa Wastaafu wajikusanye wakae na waweke mkakati wa kwenda kum-face Rais Magufuli Dodoma kujua hatima ya Mafao yao!
Pengine inaweza kusaidia ingawa huyu jamaa hatabiriki!
 
Kulingana na report ya Ukaguzi ya CAG 2019/20 Serikali inadaiwa na Mifuko ya Jamii PSSSF kiasi cha zaidi ya Tshs. 700 Bilioni ambazo Serikali imekopa toka PSSSF na haijarudisha/kulipa fedha hizo.

Kuna Habari za kuaminika kwamba fedha hiyo imekopwa kwenda kujengea miradi mikubwa ya Serikali kama SGR na Stieglers Gorge(Bwawa la Nyerere).
Duuh . . .hii mbona ni hatari ? kuna ukweli hapa? Na kama ni kweli basi mzigo wa Pension katika madeni ya serikali unazidi kutuelemea
 
Halafu Rais Magufuli huyu huyu anajiita RAIS WA WANYONGE!

Fedha za kujenga SGR, FLY OVERS na GORGE zipo lakini za kuwalipa wazee hazipo...huyu Rais ni tatizo!
Raisi anapenda maendeleo ya kuruka,lakini hizo megaproject anazotamani zianze mara mmoja kwa pammoja zinahitaji pesa nyingi na sidhani kama ana hata robo yake.
 
Magufuli nitamtumbuwa mwaka huu bila huruma. Naomba nieleweke hivyo.
 
kwakweli wastaafu hawa wamelitumikia taifa hili kwa uaminifu na uzalendo mkubwa katika hali ngumu za kimaisha wengi wao wakitokea vijijini hebu wapewe stahiki hizo ambazo ni jasho lao
 
Back
Top Bottom