The indigenous
JF-Expert Member
- May 14, 2018
- 312
- 143
KabisaHuyu ni Rais wa VITU na siyo WATU!
Vipaumbele vyake ni kuona barabara, flyovers, ndege(Dreamliner,Bombardier, etc) na Kujenga Ikulu za Chamwino na Chato !! Lakini mafao ya wastaafu, kuboresha mishahara na marupurupu ya Wafanyikazi Hana Fedha na wakti huohuo anasema hii nji ni Tajiri sana! Ni shidaaaa!
Mtumishi wa serikali akistaafu kuna anachopewa zaidi ya michango yake toka mifuko ya hifadhi ya jamii? Afadhali baadhi ya mashirika ya umma yana mafao yaliyoorodheshwa kwenye mkataba wa hiarikwakweli wastaafu hawa wamelitumikia taifa hili kwa uaminifu na uzalendo mkubwa katika hali ngumu za kimaisha wengi wao wakitokea vijijini hebu wapewe stahiki hizo ambazo ni jasho lao
Sikio la kufa
Nimenunua dream liner kwa cash wakati hata makampuni makubwa ya ndege ya nchi tajiri yanakopa, kumbe kachota mafao ya wastaafu! Kilangila.
Hii mifuko ya hifadhi ya jamii siyo Benji,kwa nini inakopesha fedha?Hiyo siyo aina nyingine ya utakatishaji fedha?Kulingana na report ya Ukaguzi ya CAG 2019/20 Serikali inadaiwa na Mifuko ya Jamii PSSSF kiasi cha zaidi ya Tshs. 700 Bilioni ambazo Serikali imekopa toka PSSSF na haijarudisha/kulipa fedha hizo.
Kuna Habari za kuaminika kwamba fedha hiyo imekopwa kwenda kujengea miradi mikubwa ya Serikali kama SGR na Stieglers Gorge(Bwawa la Nyerere).
Tunajua Bunge linamaliza muda wake na kuvunjwa June hii,2020. Kwa uhakika Wabunge na Mawaziri wote watalipwa mamia ya mamilioni ya Shilingi baada ya kulitumikia Bunge kwa miaka 5 tu!
Kinachosikitisha kuna wazee Wastaafu wamelitumikia Taifa hili kwa uaminifu na kwa miaka mingi kati ya 25~40 lakini mpaka sasa wengi wao hawajalipwa mafao yao tangu Wastaafu.
Wengine wana miaka 3,2,1 na wengine wana miezi kadhaa. Wazee hawa wanapofika PSSSF hupewa Majibu yaliyojaa visingizio vya uchelewesho wa malipo ya michango toka kwa Waajiriwa au makosa ya ujazaji wa fomu, majina au tarehe za kuzaliwa ilhali Ukweli ni kwamba Mifuko haina Fedha ya kuwalipa wazee hao.
Kama Hali itaendelea kuwa hivo Rais Magufuli ajue kuwa hatopata kura hata moja toka kwa hao wazee Wastaafu pamoja na familia zinazowategemea.
Wazee hao wamepigika sana hasa kipindi hiki cha Covic-19 maana hawana kipato chochote, hawana mishahara, hawana malipo ya pensheni na hawawezi kukopesheka popote.
Chondechonde Rais Magufuli toa maelekezo kwa Hazina ilipe Deni Hilo la PSSSF ili mfuko uwalipe Wastaafu hao wanyonge.
Kulingana na report ya Ukaguzi ya CAG 2019/20 Serikali inadaiwa na Mifuko ya Jamii PSSSF kiasi cha zaidi ya Tshs. 700 Bilioni ambazo Serikali imekopa toka PSSSF na haijarudisha/kulipa fedha hizo.
Kuna Habari za kuaminika kwamba fedha hiyo imekopwa kwenda kujengea miradi mikubwa ya Serikali kama SGR na Stieglers Gorge(Bwawa la Nyerere).
Tunajua Bunge linamaliza muda wake na kuvunjwa June hii,2020. Kwa uhakika Wabunge na Mawaziri wote watalipwa mamia ya mamilioni ya Shilingi baada ya kulitumikia Bunge kwa miaka 5 tu!
Kinachosikitisha kuna wazee Wastaafu wamelitumikia Taifa hili kwa uaminifu na kwa miaka mingi kati ya 25~40 lakini mpaka sasa wengi wao hawajalipwa mafao yao tangu Wastaafu.
Wengine wana miaka 3,2,1 na wengine wana miezi kadhaa. Wazee hawa wanapofika PSSSF hupewa Majibu yaliyojaa visingizio vya uchelewesho wa malipo ya michango toka kwa Waajiriwa au makosa ya ujazaji wa fomu, majina au tarehe za kuzaliwa ilhali Ukweli ni kwamba Mifuko haina Fedha ya kuwalipa wazee hao.
Kama Hali itaendelea kuwa hivo Rais Magufuli ajue kuwa hatopata kura hata moja toka kwa hao wazee Wastaafu pamoja na familia zinazowategemea.
Wazee hao wamepigika sana hasa kipindi hiki cha Covic-19 maana hawana kipato chochote, hawana mishahara, hawana malipo ya pensheni na hawawezi kukopesheka popote.
Chondechonde Rais Magufuli toa maelekezo kwa Hazina ilipe Deni Hilo la PSSSF ili mfuko uwalipe Wastaafu hao wanyonge.
Unaota ww mliimba haya kipindi cha lowasa na mrema iko wapi
Asante na Mungu akubariki sana, huyu Rais kuna baadhi ya Mambo anaudhi sana na anatengeneza chuki za bure asisahau vyeti veki, darasa la saba, dhuluma kwa wazabuni, hasara ya mahindi mwaka jana, nyongeza za mshahara, nyongeza ya mwaka, kutopanda vyeo na kutolipwa mishahara mipya kwa waliopanda vyeo, malimbikizo, na hawa wastaafu wengi kiafya hawakosi changamoto, kura yangu simpi na nitawapa sababu huwezi kunadi maendeleo wakati unawaongezea watu wako huzuni kila siku. Anajijengea maadui wengi acha jeshi,usalama na polisi wamrudishe madarakani, Nimekuwa mfuasi wake miaka yote sasa basi.
Kama weweni mtumishi wa umma na bado upo katika ajira kwa nafasi yoyote nakushauri wekeza katika eneo la uchumi kwani katika maisha nyakati hubadilika na nguvu hupungua. uwekezaji wa muda mrefu na mfupi ni muhimu sana, kuwa na mahusiano ya kibiashara na watu nje ya kazini kwako. Punguza idadi ya wategemezi wasio na tija katika familia yako mapema.
Haya ni machache yatakayowasaidia waajiriwa au waliostaafu kupunguza kuhangaika na wanasiasa ambao historia yao tangu enzi inajulikana na hata yeyote atakayeingia ni lazima atabadilika kuwa kama waliopita.

Amekuwa ni Rais mwenye kauli Tata siku zote. Nakumbuka aliwahi kutamka kwenye Mei mosi ya 2017 akadai WAFANYAKAZI WAMWACHE KWANZA AMALIZE KUJENGA SGR, STIEGLERS GORGE, FLYOVERS na KUNUNUA MIDEGE NDIPO ATAFIKIRIA KUONGEZA MISHAHARA!
Mpaka Sasa hakuna mradi wowote uliokamilika kati ya hiyo aliyoitaja. Maanake ni kiwa Wavuja jasho wa Tanzania waendelee kusota tu na hakutakuwa na nyongeza yoyote!!!.
Kiukweli ni kwamba huyu atakuwa ni Rais aliyetawala kwa miaka yote 10 bila kuboresha maslahi ya WAFANYAKAZI!