Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Maneno aliyosema Rais leo kuhusu kazi ya urais na umri inatuonyesha wazi, pale ikulu kwa sasa hatuna watu wanaomsaidia Rais aione vizuri nchi yetu hasa kwa siku zijazo..muhimu si kuongelea mtu wa kujaza nafasi ya urais, nadhani muhim ni kuwa na mifumo na taasisi imara za kumsaidia anayekuwa Rais, na kwa maana hiyo UMRI si muhimu awe kijana awe mzee awe mwanamke au mwanaume kazi nzr itafanyika!! Bahati mbaya sana kwa muda mrefu tumeshindwa kugundua tatizo la nchi yetu liko wapi..wengi tunadhani ni CCM si kweli.

Hata ukisikiliza hotuba ya Rais bungeni inakosa maneno mazuri ya kujenga dira na mwelekeo imara, mfano haisemi kabisa juu ya kulileta taifa pamoja sababu hali baada ya uchaguzi upo mgawanyiko mkubwa..wengine wanakimbia nchi, wengine bado wanalalamikia uchaguzi nk, ulitarajia hotuba ya kujenga udugu na umoja zaidi baada ya uchaguzi..kumbe ni ndoto.

Ushauri:
Kama kutatokea nafasi ya kufanya marekebisho ya katiba, basi tufikirie kuwa na mabadiliko makubwa kwenye taasisi zinazomsaidia Rais, kazi hizi ziwe na kikomo, mtu atumikie hapo si zaidi ya miaka 5 kupisha wengine wenye mawazo mapya kumsaidia Rais..vinginevyo tutaendelea kuwa na hali ya uchakavu wa mawazo, kauli, tabia, mikakati nk hata kama tunapata Rais kijana wa miaka 45..Asanteni.
 
Yaani Magufuli ndo katiba. Analoliamua yeye ndo linafanyika .Kwani Katiba imeweka ukomo wa umri kwenye kugombea urais ?Ninavyojua kuna umri wa kuanzia,ila wa ukomo sijui.
 
Kabudi kashaambiwa hawezi kuwa Rais...macho yamemmchomoka yakagonga kwenye lensi...yakarudi kwenye soketi...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti soketi
 
Yaani Magufuli ndo katiba. Analoliamua yeye ndo linafanyika .Kwani Katiba imeweka ukomo wa umri kwenye kugombea urais ?Ninavyojua kuna umri wa kuanzia,ila wa ukomo sijui.
Nyie si ndio mnaomsifia humu kila kukicha?
 
Madikteta hua wanaandaa watoto wao au watoto wa dada zao.

Nafikiri Kheri James au Dotto James Ndio chaguo la Jiwe
Hivi kwanini Hawa ndugu hawatajwi n majina ya ukoo?
Kheri James..........
Dotto James...........
Kuna yule mkurugenzi. Naninani John,........
Mwenye kufahamu majina yao ya ukoo aweke hapa.
 
Magufuli hataki Yale Mambo ya Maalim Seif aliyomfanyia About Jumbe, ila Mwalimu Nyerere akamkatilia mbali akakimbilia upinzani.
Hivi maalim seif ndio alimchongea Abuu Jumbe kuhusu serikali tatu?
 
Sisi tunapendekeza Rais awe na umri mkubwa kwa yale ambayo tumeyaona kwa wengine, Rais akiwa na umri mdogo atagoma kutoka madarakani na atatawala maisha yake yote, lakini akiwa mzee hata agome madarakani haitachukua muda atakufa
 
Wacha weee, ngoja wenye 40's tuanze kupiga push up..
 
Kwanza nianze kuwasalimu Wanajamii wote wanaotumia jukwaa hili katika kutoa Elimu kwa jamii kwa masuala mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Kwanza , yapo mambo mazuri Rais ameyazungumza leo lakini katika hili la kwamba mtu aliyemzidi umri hawezi kuwa Rais wa Nchi hii , kwa kweli sikubaliani naye hata kidogo.

Hakueleza umri wake kwa sasa ni miaka mingapi ! Ili tujue , Je , aliyezidi umri huo hana sifa ya kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi?

Binafsi , mtu kama William Lukuvi , kila Mtanzania mwenye Itikadi ya Chama fulani na asiye na itikadi ya Chama chochote cha Siasa hapa nchini , wanamkubali Sana Willium Lukuvi

Kila Mtanzania naamini kwa asilimia 100% , wanampenda sana Mheshimiwa Lukuvi kwa Utendaji wake uliotukuka.

Kutuambia kwamba Lukuvi kwa sababu amemzidi umri hawezi kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi kwa nafasi ya Jamhuri ya Muungano ( Rais ), si sawa !

Naomba mawazo yenu wadau wa Siasa. Na niwaombe wala tusichangie mada hii kwa ushabiki .

Naomba kuwasilisha .
 
CCM wana wimbo wao fulani hivi una maneno haya:

"Tumeipenda wenyewe, watavimba wapasuke"

" Acha waisome namba, CCM mbele kwa mbele".

Maneno haya yalilenga kuwananga wapinzani. Lkn Mungu siyo Lukuvi wala Athuman, sasa maneno haya yameanza kula upande wao.

Acha waparurane akili iwakae sawa.
 
Hivi maalim seif ndio alimchongea Abuu Jumbe kuhusu serikali tatu?
Ndiyo, wakati huo Maalim Seif alikuwa waziri kiongozi (waziri mkuu wa smz).
Pamoja na"kazi nzuri" ya kumchongea na kupeleka ushahidi Mwalimu Nyerere alijua Nia Yake pia alijua itikadi Yake.....HIZBU.... akamkatilia mbali akakimbilia upinzani.
 
Ndiyo, wakati huo Maalim Seif alikuwa waziri kiongozi (waziri mkuu wa smz).
Pamoja na"kazi nzuri" ya kumchongea na kupeleka ushahidi Mwalimu Nyerere alijua Nia Yake pia alijua itikadi Yake.....HIZBU.... akamkatilia mbali akakimbilia upinzani.
Ama kweli wanafiki ni wabaya kuliko makafiri
Mnajipendekeza hata mkisemaje hawawezi kuwaridhia mpaka mfuate mila zao
Mnafurahia dhulma kwa waislamu eti nyerere kwani nyerere zanzibar kwao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…