Maneno aliyosema Rais leo kuhusu kazi ya urais na umri inatuonyesha wazi, pale ikulu kwa sasa hatuna watu wanaomsaidia Rais aione vizuri nchi yetu hasa kwa siku zijazo..muhimu si kuongelea mtu wa kujaza nafasi ya urais, nadhani muhim ni kuwa na mifumo na taasisi imara za kumsaidia anayekuwa Rais, na kwa maana hiyo UMRI si muhimu awe kijana awe mzee awe mwanamke au mwanaume kazi nzr itafanyika!! Bahati mbaya sana kwa muda mrefu tumeshindwa kugundua tatizo la nchi yetu liko wapi..wengi tunadhani ni CCM si kweli.
Hata ukisikiliza hotuba ya Rais bungeni inakosa maneno mazuri ya kujenga dira na mwelekeo imara, mfano haisemi kabisa juu ya kulileta taifa pamoja sababu hali baada ya uchaguzi upo mgawanyiko mkubwa..wengine wanakimbia nchi, wengine bado wanalalamikia uchaguzi nk, ulitarajia hotuba ya kujenga udugu na umoja zaidi baada ya uchaguzi..kumbe ni ndoto.
Ushauri:
Kama kutatokea nafasi ya kufanya marekebisho ya katiba, basi tufikirie kuwa na mabadiliko makubwa kwenye taasisi zinazomsaidia Rais, kazi hizi ziwe na kikomo, mtu atumikie hapo si zaidi ya miaka 5 kupisha wengine wenye mawazo mapya kumsaidia Rais..vinginevyo tutaendelea kuwa na hali ya uchakavu wa mawazo, kauli, tabia, mikakati nk hata kama tunapata Rais kijana wa miaka 45..Asanteni.