Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Na kitendo cha JPM kusema siyo mtazamo huu haijawa sheria. JPM ni mwenyekiti wa Sisiemu, anafahamu mwelekeo, mipango & matarajio ya Sisi-M kwa ajili ya maslahi mapana ya taifa. Ufipa mnaweza kumweka mgombea wenu yeyote hata mwenye miaka 900 ruksa.
 
Yeye amesema chama Cha mapinduzi (CCM) yeye Kama mwenyekiti hawawezi kumpitisha aliyempita umri, rejea hata mh. Mstaafu JK alisema hivyo. kwahiyo hapo Katiba haihusiki, usi-genaralize. Bali ni ndani ya chama na utaratibu wao.
Jibu makini sana. Kama ulikuwepo we jamaa!
 
Hii inaitwa tentative position. Kabla ya uchaguzi aliwahi kuwatahadharisha wateule wake (PSs, RCs, DCs, etc.) kwamba angewakata endapo wangejaribu kugombea ubunge. At the end of the day, alibadili msimamo na baadhi ya wateule wake wakagombea ubunge!
Umemnukuu kiupotoshi zaidi. Heshimu teknolojia
 
Sisi tunapendekeza Rais awe na umri mkubwa kwa yale ambayo tumeyaona kwa wengine, Rais akiwa na umri mdogo atagoma kutoka madarakani na atatawala maisha yake yote, lakini akiwa mzee hata agome madarakani haitachukua muda atakufa
Yaa napendekeza tupate raisi wa miaka 80 kuendelea mbele wanakuwaga na hekima sana
 

Strategy ya wapinzani kutumia rejects wa CCM haijawahi kuwapa nguvu ya kudumu. Wanaweza kuambulia nguvu ya soda kama kawaida!
 
Umri mkubwa ila hawakaribii Joe Biden na Donald Trump wana 74yrs na 77yrs na bado wanagombea
 
It's the total waste of time kuongelea vitu kama hivi. Na ni kwenda kinyume na katiba hata ya chama chake pia ukiacha nchi.
 
Umeeleza vizuri sana. Lakini umesema tena tatizo siyo CCM. CCM ndiyo tatizo kwa sababu ndiyo walitakiwa watengeneze hiyo mifumo na kama ni katiba waongoze kuibadilisha. Mengine umeelezea vizuri tu na hasa tatizo limeonekana kuwa kubwa kwa sababu awamu hii rais anataka kuwa ndiye kila kitu. Kwa kifupi hii mifumo awamu zilizopita japo haikuwa mizuri lakini marais waliokuwepo hawakuwa wanajilimbikizia madaraka mengi kama huyu wa sasa. Mfano mzuri wa kuwa ni mifumo mizuri ni Marekani. Unajua Marekani isingekuwa na mifumo imara Trump angeiharibu sana nchi na hata kwenye madaraka asingetoka.
 
Usitudangenye ndugu yangu. Mungu ndiye anapanga mpaka viongozi wauaji waingie kwenye madaraka?
 
Nasema tatizo si CCM sababu wapo watu nyuma yao..Mwl. Baba wa taifa aliwahi kuwaongelea hawa watu, kwamba kila alipotaka kung'atuka wao walikuwa wanamwambia ooh Mwl. watu bado wanakuhitaji na bla bla nyingi, vile Mwl. alikuwa thinker aligundua kuwa kumbe bla bla hizo za kuomba aendelee kubaki kuongoza ni kwa sababu uwepo wake hapo wala si kwa faida ya nchi ni kwa faida ya matumbo yao..hao ndio watanzania wanapaswa kudeal nao.
 
Mtu kama Lowassa umemwonea tu. Yule sidhani bado anauwaza urais na angekuwa bado anautamani huu uchaguzi bado angegombea tena kupitia Chadema. Afya yake haimruhusu kwa sasa. Ile 2015 tu ilikuwa shida.
 
Hao watu ndiyo CCM yenyewe basi ndugu yangu.
 

Wananchi wajipange kutafuta mbinu za kujikomboa kutokana na utawala haramu wa ccm!!! Ningeshauri jambo la kwanza kuwa makini na mbinu zitakazotumika kupata kwanza TUME HURU ya uchaguzi. Mimi binafsi naona ni muhimu kuwa na tume huru ya uchaguzi hata kabla ya kudai KATIBA , kwani sidhani kuwa katiba itakayoandikwa chini ya uangalizi wa JIWE na genge lake itakidhi matakwa ya wananchi!!!!
Ikipatikana TUME HURU , tutakuwa na nafasi nzuri ya kupata Bunge lenye wabunge makini wataokuwa na moyo wa kuwatumikia wananchi na hapo ndio patakuwa wakati mzuri wa kuandika KATIBA watayoitaka wananchi.

From now on strategy iwe kupata TUME HURU YA UCHAGUZI otherwise kukubali kuendelea kushiriki chaguzi zinazoendeshwa na tume hii ya JIWE ni kuonesha kuwa mapoyoyo!!
 
Jibu makini au ugoro? Mgombea anapatikana kwa kupigiwa kura na vikao mbali mbali. Hata akiwa mwenyekiti hawezi kutoa uamuzi wa aina huyo.
Really? Influnce ya Mwenyekiti wa Chama (hasa ambaye ndiye President) lazima uiweke kwenye mlinganyo wa tafakari yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…