Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Atakuwa ameudhi watu wengi wa CCM kwa hii kauli. Wakome! Hili Bunge la sasa wabunge wote wameupata ubunge kwa ridhaa yake. CCM wakachekelea wakasema Lissu na Chadema wamekomolewa! Ona sasa.. wamemlea wee mpaka sasa hivi amefikia hatua ya kuamua ni nani awe rais na nani asiwe! Na bado. Na hatanii kweli. Atakachofanya ni atam-point mtu anayemtaka kwa kidole na kwenye kura atapenyeza tena kura kama alivyofanya huu uchaguzi. Walifikiri upinzani ndiyo unakomolewa kumbe dawa yao iko jikoni!
Unachopaswa kufanya ni kumnyima kura
 
Magufuli yuko sahihi kabisa, najua behaviour ya wasaka urais, awamu ya pili huwa wanakosa focus ya kuwatumikia wananchi badala yake wanaanza kampeni za urais.Safari hii kibano hadi mwisho,akiwalegezea hawatamsaidia watabaki kujipalilia njia.SAFI SANA JPM, BANA MPAKA 2025 TUMEZOEA KUPATA SURPRISE YA MGOMBEA URAIS SIYO HAWA WASAKA TONGE
 
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi.

Hakuna sehemu katika katiba ya Nchi yetu inayomkataza mtu yeyote kugombea nafasi ya Urais kwa kigezo cha umri mkubwa.

Washauri wa Rais jaribuni kumshauri Bwana Mkubwa kuna kauli akizisema ninaleta mtafaruku mkubwa sana katika jamii.
Joe Biden Ana 77, Sasa kwanini jakaya kikwete asigombee Tena kisa anamzidi Magufuli?
 
Hii nchi ina watu wengi sana wanaofaa kuwa viongozi.
Yeye ni nani aanze kuzuia watu kugombea?
Huyu mzee namkubali sana ila anaboa sometimes
kama angekuwa hazuii watu kugombea, basi kusingekuwa na watu kupitishwa pasipo kupingwa, wapinzani kutiwa vilema, kuuwawa na kutekwa..bora mkoloni mzungu kuliko mkoloni mweusi.
 
Mara hii wameanza kuongelea urais 2025! CCM kweli wameamua kuitafuna nchi milele liwe jua iwe mvua; hii nchi hawaiachii kwa "vikaratasi". Badala ya kuongelea vitu vya muhimu hususan tume huru ya uchaguzi, Katiba Mpya, etc. wanaanza kutajataja nani anafaa na nani hafai mapema hivi? Kwa mtindo huu, tundelee kuzoea "bao la mkono" miaka mingi ijayo!
Afu chandimu wapo bize ICC, ccm ishaanza kujiandaa, unafikiri chandimu watashinda kweli?
 
Wewe wasema
[emoji6][emoji6][emoji6]Jamaa anatoa kipondo heavy halafu hapo pembeni kuna kipeperushi kimeandikwa hapa kazi tu![emoji1787]
Emn32CaW4AEEAJg.jpg
 
kama angekuwa hazuii watu kugombea, basi kusingekuwa na watu kupitishwa pasipo kupingwa, wapinzani kutiwa vilema, kuuwawa na kutekwa..bora mkoloni mzungu kuliko mkoloni mweusi.
Mzee amezingua kwenye hili
 
Jamaa ni wa hovyo sn anafikiria madaraka tu.. 🤔🤔
 
Sina hakika kama katiba ya nchi hii ina ukomo wa umri kwenye sifa za kuwa rais wa JMT.

Chochote kinawezekana ikiwemo na Lukuvi kuwa Rais wa JMT.(Ndani au nje ya CCM)😁

What if Magu asiwepo hiyo 2025 yenyewe na "king makers" waliobaki wakawa hawana maoni kama yake?

Michael Chilufya Sata (King Cobra) mwenyewe aliukwaa akiwa 74.
Jamaa ni mbabe na kwa maneno yake inamaanisha kuwa hao Marais hawachaguliwi na wananchi bali na system. Hivyo kwa wale wanaojiandaa kugombea, hakuna cha bahati bali kuna mpango tayari ......!!
 
Leo umeeongea point mzee point tupu

Sio kwamba tunakupinga pinga tu

Ila pia Kuna wakati unaongea vinavyoleta mantiki

Kwa Leo Nimekukubali sio kesho utakujaje[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Yeye alivyooendekezwa na Mzee Mkapa alikuwa kijana??
 
Katika Hilo kundi la vijana mtu Ninaye muona afadhali humo ndani ya CCM labda januari makamba na ana nguvu kubwa Sana

Na ana presidential charisma kuliko hawo wengine vichwa maji .

Japo nayeye Ni mchimbachumvi fulani hivi Ila katika CCM yeye ndio ana afadhali

Na naona atakuwa back up kubwa Sana labda wampishe mwinyi

Otherwise January atawafaaa

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom