Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Tatizo anajiona yeye ndio Mungu wa Tanzania chochote anachosema ni sahihi walishindwa kina Nyerere kuwrka mtu aliyemtaka sembuse yeye
 
Mtu akila nyama ya mtu haachi-mwl.Nyerere
Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli amesema uchaguzi mkuu wa 2025 utatoa fursa kwa vijana kwa sababu zaidi ya 65% ya wapiga kura ni vijana

Rais Magufuli ametoa mfano wa mh Lukuvi kwamba hawezi kuwa Rais wa JMT 2025 kwa sababu atakuwa na miaka zaidi ya 70.

Maendeleo hayana vyama!

=======

RAIS MAGUFULI: Hakuna mtu alitegemea Mwinyi atakuwa Rais wa Zanzibar lakini pia Mwinyi katika kipindi chake chote hakuutafuta Urais, vitu hivi vinapangwa. Hakuna mtu alijua profesa Ibrahim atakuwa Jaji mkuu wa Tanzania hata mimi sikujua kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa sababu katika miaka yote ishirini nikiwa waziri na nikiwa mbunge sikuwahi kuomba hata ujumbe wa NEC.

Sikuwahi, wajumbe wa NEC walikuwa wakina Lukuvi, tangu aingie mle ni mjumbe wa NEC lakini Urais hakuupata na sina uhakika kama ataupata Urais. Wewe sasa hivi ana miaka sitini na kitu, tukapendekeze kwenye central committee tukachague Rais anaenizidi umri mimi, ndio ukweli.

Maneno mengine yanaumiza lakini nataka niwaeleze muwe mnajitayarisha kisaikolojia kusudi msipoteze hata hela zenu, hata wewe profesa Kabudi huwezi ukawa Rais, najua haya mambo ni magumu lakini huo ndio ukweli.

Mzee Kikwete wakati anaondoka, alisema hataona Rais ambae anamzidi umri wake, sasa muangalie mimi nina umri gani nitakapokuwa namaliza, ujipimie kuanzia kwenye umri pale. Yaani Malecela tumpendekeze awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haiwezekani! Ameshakuwa mstaafu, tunamheshimu, tunampenda.

Najua mmenyamaza kwa hiyo inawezekana umekaa na jirani yako ambae ndie atakuwa Rais ambae labda ni kijana zaidi kwa sababu 65% ya watanzania ni vijana na hivi ndivyo vilivyomsaidia Mwinyi kushinda kule, wapiga kura ni vijana wether you like or not huo ndio ukweli, sasa huwezi ukawapelekea wapiga kura mtu ambae sio saizi yao.

Maneno yanauma lakini si mmeniomba niseme hapa, mimi nilikuwa nimekaa kimya tu leo nisiseme, nilikuwa nachomekea tu.
 
Kabudi kashaambiwa hawezi kuwa Rais...macho yamemmchomoka yakagonga kwenye lensi...yakarudi kwenye soketi

Kama sio miwani kuzuia saa hii tungeshasema mengine

Ila JPM sio poa kuwananga wanaomzidi umri, mbona Joe Biden kawa Rais na miaka 78.!

Au dhambi ya ubaguzi inaendelea.?
😀😀😀jamaa anawakatisha tamaa
 
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi.

Hakuna sehemu katika katiba ya Nchi yetu inayomkataza mtu yeyote kugombea nafasi ya Urais kwa kigezo cha umri mkubwa.

Washauri wa Rais jaribuni kumshauri Bwana Mkubwa kuna kauli akizisema ninaleta mtafaruku mkubwa sana katika jamii.
Mbona unaonekana uelewa wako ni mdogo sana? Hajakataza mtu kugombea yeye amesema kwenye chama chake itakuwa vigumu kupita kama wewe una umri mkubwa. By the way kwani chama hakina vijana wanaoweza kugombea mpaka mzee wa miaka 70 agombee? Mshauri mgombea wako akagombee upinzani CCM hataweza kupita kuna vijana wa kutosha kugombea Urais.
 
Huyo anaandaa mbeleko ya kubebea mtu wake kuwa Rais ajaye kama yeye alivyobebwa ili muda ukifika atuletee tumchague kuendeleza utamaduni wa CCM wa kupata viongozi. Ingawa yeye alibeba mtu wake akatuletea, ni JK pekee ndo hakubebwa na kiongozi yeyote. Nyerere alimbeba Mwinyi kwa maneno mawili tu: "Mwinyi je?" na Mkapa kwa maneno: "Huyu ndio Rais wenu" akawa. Lukuvi ni wa Nyanda za Juu hata angekuwa kijana hatabebeka!
 
kwanza kabisa mkwe wake si mwafrika mtu huyo hafai kabisa kupewa mafasi
 
Kumbe mgombea urais wa ccm huteuliwa na Rais?

Kama ndivyo,huwa kuna sababu gani ya kukusanya wajumbe kupiga kura?Au wanapigia kura machaguo ya rais?
 
Alipoomba urais kundi kubwa la vijana lilikuwa asilimia ngapi? Tunapata rais wa nchi kwa legal processes na uwezo wa mtu kiutawala

Ujana tu hauwezi kuwa qualifications - anyway remain silent huenda nikawa mimi
ukawa wewe kabende msakila et
😂
 
Naona CCM mnazungumza Jambo na mungu wenu.

Hakuna ajuae kesho yake, na Wala usiseme ww hauwezi kuwa rais au Nani.

Who are you?
 
Mbona unaonekana uelewa wako ni mdogo sana? Hajakataza mtu kugombea yeye amesema kwenye chama chake itakuwa vigumu kupita kama wewe una umri mkubwa. By the way kwani chama hakina vijana wanaoweza kugombea mpaka mzee wa miaka 70 agombee? Mshauri mgombea wako akagombee upinzani CCM hataweza kupita kuna vijana wa kutosha kugombea Urais.
🙄🙄🙄 Mjomba mbona hueleweki
 
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi.

Hakuna sehemu katika katiba ya Nchi yetu inayomkataza mtu yeyote kugombea nafasi ya Urais kwa kigezo cha umri mkubwa.

Washauri wa Rais jaribuni kumshauri Bwana Mkubwa kuna kauli akizisema ninaleta mtafaruku mkubwa sana katika jamii.
Kwa bahati Mbaya wengi wa wanaomzunguka ni waoga na wanafki kama akina Mwingulu. Hawana uwezo wa kumwambia ukweli pale Mhe. anapotoka nje ya Mstari.

So, usitegemee kama kuna atakaye weza kumshauri vinginevyo. Mana washauri wake wanaoshia kichekacheka hovyo na kumwambia you are the best ever.
 
Hii nchi ina watu wengi sana wanaofaa kuwa viongozi.
Yeye ni nani aanze kuzuia watu kugombea?
Huyu mzee namkubali sana ila anaboa sometimes
Haya maneno hata Jakaya aliyaongea na ikawa alikataa kumuachia mtu wa umri zaidi yake.Unachosahau ni kwamba ccm ndiyo chama kinachotoa rais wengine wasindikizaji.Rejea chaguzi za 1995 2000,2005,2010 na 2015
Leo alikuwa anaongea kama mwenyekiti wa ccm.Nani anaweza kubishana na mwenyekiti?????????? Hiyo ndiyo ccm chama chenye mifumo thabiti
 
Kwel ccm wanawaza mbali ,yaan shv wanaoanga ya 2025 wakati vijana ajira hawana ,mishahara midogo,katiba mpya haisemwi .wao wanawaza nan atakuwa rais .mtakuja kuroganaa muuwaneee kisa uraisi
 
Kwanza anaongea tu hapo. Hachomoki huyo kwenye hicho kiti.
 
Back
Top Bottom