Rais Magufuli: Lukuvi hawezi kuwa Mgombea urais wa CCM 2025 kwa sababu ana umri mkubwa. Ni fursa ya Vijana

Sisi tunapendekeza Rais awe na umri mkubwa kwa yale ambayo tumeyaona kwa wengine, Rais akiwa na umri mdogo atagoma kutoka madarakani na atatawala maisha yake yote, lakini akiwa mzee hata agome madarakani haitachukua muda atakufa
Atagoma jee wakati katiba inambana

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Hili si jukumu la Rais - Hili ni jukumu la kikatiba. Je katiba yetu unasemaje kuhusu Umri wa Rais wetu?

Hata hivyo hili lilikuwa dogo kwa EL na rafiki yake Mr. 0 baada ya kurudi kundini huku wakiendelea kudhani wanaweza kuukwaa Urais baada ya kuwa uhamishoni kwa muda.
 
Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli amesema uchaguzi mkuu wa 2025 utatoa fursa kwa vijana kwa sababu zaidi ya 65% ya wapiga kura ni vijana

Rais Magufuli ametoa mfano wa mh Lukuvi kwamba hawezi kuwa Rais wa JMT 2025 kwa sababu atakuwa na miaka zaidi ya 70.

Maendeleo hayana vyama!

=======

RAIS MAGUFULI: Hakuna mtu alitegemea Mwinyi atakuwa Rais wa Zanzibar lakini pia Mwinyi katika kipindi chake chote hakuutafuta Urais, vitu hivi vinapangwa. Hakuna mtu alijua profesa Ibrahim atakuwa Jaji mkuu wa Tanzania hata mimi sikujua kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa sababu katika miaka yote ishirini nikiwa waziri na nikiwa mbunge sikuwahi kuomba hata ujumbe wa NEC.

Sikuwahi, wajumbe wa NEC walikuwa wakina Lukuvi, tangu aingie mle ni mjumbe wa NEC lakini Urais hakuupata na sina uhakika kama ataupata Urais. Wewe sasa hivi ana miaka sitini na kitu, tukapendekeze kwenye central committee tukachague Rais anaenizidi umri mimi, ndio ukweli.

Maneno mengine yanaumiza lakini nataka niwaeleze muwe mnajitayarisha kisaikolojia kusudi msipoteze hata hela zenu, hata wewe profesa Kabudi huwezi ukawa Rais, najua haya mambo ni magumu lakini huo ndio ukweli.

Mzee Kikwete wakati anaondoka, alisema hataona Rais ambae anamzidi umri wake, sasa muangalie mimi nina umri gani nitakapokuwa namaliza, ujipimie kuanzia kwenye umri pale. Yaani Malecela tumpendekeze awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haiwezekani! Ameshakuwa mstaafu, tunamheshimu, tunampenda.

Najua mmenyamaza kwa hiyo inawezekana umekaa na jirani yako ambae ndie atakuwa Rais ambae labda ni kijana zaidi kwa sababu 65% ya watanzania ni vijana na hivi ndivyo vilivyomsaidia Mwinyi kushinda kule, wapiga kura ni vijana wether you like or not huo ndio ukweli, sasa huwezi ukawapelekea wapiga kura mtu ambae sio saizi yao.

Maneno yanauma lakini si mmeniomba niseme hapa, mimi nilikuwa nimekaa kimya tu leo nisiseme, nilikuwa nachomekea tu.
Ha ha ha
Naenda badilisha RITA tarehe yangu ya kuzaliwa!
 
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi.

Hakuna sehemu katika katiba ya Nchi yetu inayomkataza mtu yeyote kugombea nafasi ya Urais kwa kigezo cha umri mkubwa.

Washauri wa Rais jaribuni kumshauri Bwana Mkubwa kuna kauli akizisema ninaleta mtafaruku mkubwa sana katika jamii.
Rais ajaye ni mimi. Kwa hiyo mh. Rais amesema hivyo kwa sababu tayari anamjua Rais ajaye ambaye ni mimi
 
Hii inaitwa tentative position. Kabla ya uchaguzi aliwahi kuwatahadharisha wateule wake (PSs, RCs, DCs, etc.) kwamba angewakata endapo wangejaribu kugombea ubunge. At the end of the day, alibadili msimamo na baadhi ya wateule wake wakagombea ubunge!
 
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi.

Hakuna sehemu katika katiba ya Nchi yetu inayomkataza mtu yeyote kugombea nafasi ya Urais kwa kigezo cha umri mkubwa.

Washauri wa Rais jaribuni kumshauri Bwana Mkubwa kuna kauli akizisema ninaleta mtafaruku mkubwa sana katika jamii.
Wewe ni mzushi unataka katiba ieleze kila jambo
 
Kauli hiyo ya JPM inaweza kuwa ni fursa na faida kwa wapinzani kama wataweza kuwatumia wazee na wanaccm ambao wameshapigwa chini mpaka hapo!
Nina amini wapo wanaccm wa umri huo waliokipigania na kukijenga chama ambao hawatakubaliana na utaratibu huo ambao haupo hata kwenye katiba si ya ccm wala ya JMT!
Hawa wanaweza wasikubali nguvu zao kwenda bure, hivyo ni hawa ndio wanaweza kuuza ramani ya vita kwa wapinzani huku wakikipasua chama hicho vipandevipande.
Kubwa zaidi watakuwa na msaada kama watasaidia wapinzani kupenyeza mkono kwa watu wa system na vyombo vya dola!
Hivyo CCM wajuwe wameshawasha moto ambao hawawezi kuuzima!
 
Yeye amesema chama Cha mapinduzi (CCM) yeye Kama mwenyekiti hawawezi kumpitisha aliyempita umri, rejea hata mh. Mstaafu JK alisema hivyo. kwahiyo hapo Katiba haihusiki, usi-genaralize. Bali ni ndani ya chama na utaratibu wao.
Kwani mwenyekiti wa chama huwaapisha mawaziri? Pale aliongea kama Raisi wa Jamhuri ya Tanzania
 
Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli amesema uchaguzi mkuu wa 2025 utatoa fursa kwa vijana kwa sababu zaidi ya 65% ya wapiga kura ni vijana

Rais Magufuli ametoa mfano wa mh Lukuvi kwamba hawezi kuwa Rais wa JMT 2025 kwa sababu atakuwa na miaka zaidi ya 70.

Maendeleo hayana vyama!

=======

RAIS MAGUFULI: Hakuna mtu alitegemea Mwinyi atakuwa Rais wa Zanzibar lakini pia Mwinyi katika kipindi chake chote hakuutafuta Urais, vitu hivi vinapangwa. Hakuna mtu alijua profesa Ibrahim atakuwa Jaji mkuu wa Tanzania hata mimi sikujua kama nitakuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa sababu katika miaka yote ishirini nikiwa waziri na nikiwa mbunge sikuwahi kuomba hata ujumbe wa NEC.

Sikuwahi, wajumbe wa NEC walikuwa wakina Lukuvi, tangu aingie mle ni mjumbe wa NEC lakini Urais hakuupata na sina uhakika kama ataupata Urais. Wewe sasa hivi ana miaka sitini na kitu, tukapendekeze kwenye central committee tukachague Rais anaenizidi umri mimi, ndio ukweli.

Maneno mengine yanaumiza lakini nataka niwaeleze muwe mnajitayarisha kisaikolojia kusudi msipoteze hata hela zenu, hata wewe profesa Kabudi huwezi ukawa Rais, najua haya mambo ni magumu lakini huo ndio ukweli.

Mzee Kikwete wakati anaondoka, alisema hataona Rais ambae anamzidi umri wake, sasa muangalie mimi nina umri gani nitakapokuwa namaliza, ujipimie kuanzia kwenye umri pale. Yaani Malecela tumpendekeze awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haiwezekani! Ameshakuwa mstaafu, tunamheshimu, tunampenda.

Najua mmenyamaza kwa hiyo inawezekana umekaa na jirani yako ambae ndie atakuwa Rais ambae labda ni kijana zaidi kwa sababu 65% ya watanzania ni vijana na hivi ndivyo vilivyomsaidia Mwinyi kushinda kule, wapiga kura ni vijana wether you like or not huo ndio ukweli, sasa huwezi ukawapelekea wapiga kura mtu ambae sio saizi yao.

Maneno yanauma lakini si mmeniomba niseme hapa, mimi nilikuwa nimekaa kimya tu leo nisiseme, nilikuwa nachomekea tu.
Dongo kwa kina membe
 
Kitendo cha Mh Rais kutamka hadharani kuwa mtu yeyote aliyemzidi umri asijidanganye kuomba nafasi hiyo ni kwenda kinyume kabisa na katiba ya Nchi.

Hakuna sehemu katika katiba ya Nchi yetu inayomkataza mtu yeyote kugombea nafasi ya Urais kwa kigezo cha umri mkubwa.

Washauri wa Rais jaribuni kumshauri Bwana Mkubwa kuna kauli akizisema ninaleta mtafaruku mkubwa sana katika jamii.
Anaongelea CCM wewe katika yako utakutana na NEC na chama chako
 
Back
Top Bottom