Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Nashangaa anawalaumu waliokuwa wanapima kule maabara ya kitaifa kuwa wanamhujumu, kwa kutoa matokeo positive Ya corona, anadai kuwa walionekana ni positive ni uongo, eti alipeleka sample Ya Mbuzi, papai, na vitunguu eti wale watu Wa maaabara ya taifa walimuhujumu, eti na hizo sample hao wa maaabara Walisema ni positive aiseee anaone kuwa hakuna corona anasema hata ligi ya mpira atairuhusu iendelee aisee huyu mzeee akishindwa Jambo anasingizia mabeberu na kuwa anazungukwa, yani hahahahaha, Halafu nashangaaa anaenda anasema corona kweli ipo halafu anasema vipimo ni vya uongo watu waliokuwa wanapima wachunguzwe yani mmmmh simwelewi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mtu mmoja wa idara nyeti aliniambia kuwa ipo siku nchi hii itakita sehemu mbaya na kuitoa hapo haitakuwa kazi rahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado tuna safari ndefu sana kuelewa mambo!
Alichokiongelea Rais ni tofauti sana na kilivyopokelewa na kueleweka kwa walio wengi... tusijitoe ufahamu, ni bora tukatafakari alilolisema kiongozi mkuu wa nchi linawezekanaje na kwanini?
Mkuu kiongozi wa nchi ambayo literacy level ya watu wake iko chini hawezi akatumia fasihi au nahau kuongea na taifa.Please usitake kuleta tafasri zako uchwara
 
Kuna baadhi ya watu mnapenda kusikia habari mbaya tu kuhusu corona.

Mkisikia corona imeua watu sabini kwa mpigo basi roho zenu kwatu!

Hakuna cha corona. Watu wafanye kazi na maisha yaendelee.

Ujuaji tu!



Sent using Jamii Forums mobile app
Isije ukawa na wewe janjajanja unawaambia wenzio wakati uko kwenye handaki! Au ndio mambo ya TEAM ROHO MBAYA? Wenzio wafe baadae uanze kuwakashufu
 
kosa kubwa la nchi hii ni kutoa elimu ya kula na kulala! wananchi hawazijui haki zao. yaan wangezijua japo hata nusu!!! mpaka dak hii ingekua stori yuko chato analima na sio kuapisha watu
 
Sijui watu wanapata faida gani juu ya huu upotoshaji,nyie watu bwana!

Alichokimaanisha rais ni kutaka kuonesha madhaifu ya hivi vipimo au wapimaji ,yaani haiwekani papai .mbuzi au kuku kuwa na corona

Na rais alifanya hivi ili kutaka kubaini ubora wa hivi vipimo vya korona ikiwezekana pia wapimaji


Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi vifaa vimetengenezwa hapa hapa Tanzania? Au tumenunua? Kama tumenunua tunatest ubora wake tukiwa tumeshalipa pesa na vifaa vipo nchini? Je aliyependekeza vinunuliwe bado yupo kazi? Je hao wafanyakazi aka akina Kilango Malecela wanaomdanganya rais bado wapo kazini?
 
Hizo ni siasa. Na kulidhihirisha hilo, Ndio maana waziri wa katiba na sheria ameambiwa akafanye uchunguzi...


Bado tuna safari ndefu sana kuelewa mambo!
Alichokiongelea Rais ni tofauti sana na kilivyopokelewa na kueleweka kwa walio wengi... tusijitoe ufahamu, ni bora tukatafakari alilolisema kiongozi mkuu wa nchi linawezekanaje na kwanini?
 
Okay tumekuelewa kaka mtaalamu,kwa hiyo tusiogope Corona maana ni ugonjwa wa kawaida tu hata Mbuzi na Papai wanao..

Au tuamini kwamba wataalamu wa Maabara ya Taifa wanatumiwa na mabeberu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiuhalisia ugonjwa wa COVID-19 upo na kuchukua tahadhari ni muhimu. Ila kitu kinachoshangaza ni kwamba hili tatizo linakuzwa zaidi kuliko uhalasia ambacho si kitu kizuri...

Na lengo la Mh. Rais halikuwa kubeza juhudi za wataalamu wetu kama baadhi ya watu wanavyosema huko mitandaoni, lengo lilikuwa kuangalia je? wataalamu wetu wako makini na kile wanachokifanya? Na niende mbali zaidi huwenda matokeo yale yametokana na uzembe wa wataalamu wetu ambapo wameishia ku contaminate sampuli hizo walizoletewa hivyo kupata matokeo matokeo hayo...

Tukumbuke pia wale ni binadamu na kwa shughuli za maabara usipokuwa makini basi utaishia kupata majibu ambayo siyo, na pia kama wataalamu wetu wa maabara walikuwa wanatumia vile vipimo vya kichina mfano rapid test huwenda pia wakapata hayo majibu maana vipimo hivyohivyo vilionekana na shida ndio maana mataifa mengine kama wingereza, India na baadhi ya mataifa kutoka barani ulaya wamevikataa ama pengine kuvirudisha china maana specifity na sensitivity iko chini kwa vifaa hivyo ndio maana imesoma false positive..

Na kama wametumia PCR test kwa upande wa sample za wanyama na ikasoma positive ni sawa maana hii corona zipo serotypes mbalimbali ambazo huathiri wanyama wafugwao ndio maana hata kwa mbwa kuna vaccine inaitwa "Nobivac canine 1-CV" hii ni chanjo maalamu kwa ajiri ya mbwa kuwakinga na virusi hao, ila tukija kwa matunda nahisi uchovu ama uzembe wa wataalamu wa maabara imepelekea sampuli kuwa contaminated ndio maana imesoma positive...
 
Hiyo namba mbili na namba tatu kama kweli corona ipo basi tutashuhudia watu wakifa live bila chenga. Hapo ndio tutajua kama maabara zilidanganya au lah?
Watu wamaabara zetu wamenunuliwa na mabeberu ili wapotoshe Taifa sisi hatuna Covid19
Nawaza sana juu yakauli za baba saaingine nabaki tu sina majibu
1.Tengua uteuzi wa Waziri na Naibu wake
2.Tengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Maabara
3.Nunua Mashine mpya yakupimia japo hata ukinunua utanunua kwa mabeberu haohao
Kabla ya kuongea hebu tufikirie juu ya haya

4 Mm nashukuru kwa mambo matatu hivi ameongea Leo
1.Kusema Ligi anafikiria ianze
2.Marufuku kuzika usiku
3.Watu kuruhusiwa kusafirisha misiba yao
Haya na pongeza sana ila yale juu pale tujadili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unadhani watu waliozoea kusiliza nyimbo za mipasho na magazeti ya udaku kila saa wana uwezo wa kufuatilia mambo na kuanalyze? UMEBEA NA USHABIKI WA KISIASA NDIYO USIO NA TIJA NDIYO UMETAMALAKI HAPA TZ!
Inasikitisha sana kwa nguvu kazi kushinda mitandaoni kushabikia mambo ya ajabu, nawaona hata kule twitter yaani wanajadili upuuzi tupu. Sisi kama taifa ni vyema tukajitathimini kwa kweli..
 
Back
Top Bottom