Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Kuna mtu mmoja wa idara nyeti aliniambia kuwa ipo siku nchi hii itakita sehemu mbaya na kuitoa hapo haitakuwa kazi rahisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado tuna safari ndefu sana kuelewa mambo!
Alichokiongelea Rais ni tofauti sana na kilivyopokelewa na kueleweka kwa walio wengi... tusijitoe ufahamu, ni bora tukatafakari alilolisema kiongozi mkuu wa nchi linawezekanaje na kwanini?
Mkuu kiongozi wa nchi ambayo literacy level ya watu wake iko chini hawezi akatumia fasihi au nahau kuongea na taifa.Please usitake kuleta tafasri zako uchwara
 
Kuna baadhi ya watu mnapenda kusikia habari mbaya tu kuhusu corona.

Mkisikia corona imeua watu sabini kwa mpigo basi roho zenu kwatu!

Hakuna cha corona. Watu wafanye kazi na maisha yaendelee.

Ujuaji tu!



Sent using Jamii Forums mobile app
Isije ukawa na wewe janjajanja unawaambia wenzio wakati uko kwenye handaki! Au ndio mambo ya TEAM ROHO MBAYA? Wenzio wafe baadae uanze kuwakashufu
 
kosa kubwa la nchi hii ni kutoa elimu ya kula na kulala! wananchi hawazijui haki zao. yaan wangezijua japo hata nusu!!! mpaka dak hii ingekua stori yuko chato analima na sio kuapisha watu
 
Hivi vifaa vimetengenezwa hapa hapa Tanzania? Au tumenunua? Kama tumenunua tunatest ubora wake tukiwa tumeshalipa pesa na vifaa vipo nchini? Je aliyependekeza vinunuliwe bado yupo kazi? Je hao wafanyakazi aka akina Kilango Malecela wanaomdanganya rais bado wapo kazini?
 
Hizo ni siasa. Na kulidhihirisha hilo, Ndio maana waziri wa katiba na sheria ameambiwa akafanye uchunguzi...


Bado tuna safari ndefu sana kuelewa mambo!
Alichokiongelea Rais ni tofauti sana na kilivyopokelewa na kueleweka kwa walio wengi... tusijitoe ufahamu, ni bora tukatafakari alilolisema kiongozi mkuu wa nchi linawezekanaje na kwanini?
 
Okay tumekuelewa kaka mtaalamu,kwa hiyo tusiogope Corona maana ni ugonjwa wa kawaida tu hata Mbuzi na Papai wanao..

Au tuamini kwamba wataalamu wa Maabara ya Taifa wanatumiwa na mabeberu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiuhalisia ugonjwa wa COVID-19 upo na kuchukua tahadhari ni muhimu. Ila kitu kinachoshangaza ni kwamba hili tatizo linakuzwa zaidi kuliko uhalasia ambacho si kitu kizuri...

Na lengo la Mh. Rais halikuwa kubeza juhudi za wataalamu wetu kama baadhi ya watu wanavyosema huko mitandaoni, lengo lilikuwa kuangalia je? wataalamu wetu wako makini na kile wanachokifanya? Na niende mbali zaidi huwenda matokeo yale yametokana na uzembe wa wataalamu wetu ambapo wameishia ku contaminate sampuli hizo walizoletewa hivyo kupata matokeo matokeo hayo...

Tukumbuke pia wale ni binadamu na kwa shughuli za maabara usipokuwa makini basi utaishia kupata majibu ambayo siyo, na pia kama wataalamu wetu wa maabara walikuwa wanatumia vile vipimo vya kichina mfano rapid test huwenda pia wakapata hayo majibu maana vipimo hivyohivyo vilionekana na shida ndio maana mataifa mengine kama wingereza, India na baadhi ya mataifa kutoka barani ulaya wamevikataa ama pengine kuvirudisha china maana specifity na sensitivity iko chini kwa vifaa hivyo ndio maana imesoma false positive..

Na kama wametumia PCR test kwa upande wa sample za wanyama na ikasoma positive ni sawa maana hii corona zipo serotypes mbalimbali ambazo huathiri wanyama wafugwao ndio maana hata kwa mbwa kuna vaccine inaitwa "Nobivac canine 1-CV" hii ni chanjo maalamu kwa ajiri ya mbwa kuwakinga na virusi hao, ila tukija kwa matunda nahisi uchovu ama uzembe wa wataalamu wa maabara imepelekea sampuli kuwa contaminated ndio maana imesoma positive...
 
Hiyo namba mbili na namba tatu kama kweli corona ipo basi tutashuhudia watu wakifa live bila chenga. Hapo ndio tutajua kama maabara zilidanganya au lah?
 
Kama kweli maambukizi yamepatikana katika sample ya vitu hivi..please kaa mbali na vitu vifuatavyo:

MBUZI!

PAPAI!

FENESI!

Popote vilipo keep your distance..........
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ loh!
 
Mkuu unadhani watu waliozoea kusiliza nyimbo za mipasho na magazeti ya udaku kila saa wana uwezo wa kufuatilia mambo na kuanalyze? UMEBEA NA USHABIKI WA KISIASA NDIYO USIO NA TIJA NDIYO UMETAMALAKI HAPA TZ!
Inasikitisha sana kwa nguvu kazi kushinda mitandaoni kushabikia mambo ya ajabu, nawaona hata kule twitter yaani wanajadili upuuzi tupu. Sisi kama taifa ni vyema tukajitathimini kwa kweli..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…