Jamani hili sio suala la kufanyiwa siasa wala mzaha huu ugonjwa ni wa hatari hata serikali yetu inatambua kuwa upo. Hivyo usitumike kama njia ya kujinufaisha kisiasa.
Rais Mgufuli alipoviagiza vyombo vya ulinzi na usalama ili kuchunguza utendaji kazi wa na vifaa vya maabara vinavyotumika alikuwa na nia njema. Kujua ubora wa vifaa na pili kujua kama kuna njama zilikuwa zinafanyika ili kutoa takwimu za uongo ili kuwapa watanzania hofu.
Sasa nashangaa sana wafuasi na wanachama wa upinzani wanawapotosha wananchi kuwa, mbuzi,kondoo ,mapapai na mafenesi yana corona virus.Jambo ambalo sio kweli.
Sampuli hizi zilichukuliwa kama mtego ili kubaini kama kuna njama na ubora wa vifaa vinavyotumika. Lakini hakuna mbuzi,papai,fenesi,wala kondoo mwenye Coronavirus maana hata hayo matunda tuliambiwa hayajanyauka.
Hivyo wapinzani kama mmekosa hoja za kupambana na Ccm bora mkae kimya maana mnawachanganya wananchi mpaka wanagopa kula nyama ya mbuzi na mapapai.