Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Duuuh! sasa mananasi na mafenesi yana damu au hizo sampuli zake zilipenyezwa vipi ina maana hao waliokuwa wakipima walikuwa hawaoni kuwa hizi sampuli siyo za binadamu jamani??

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliekwambia corona inapimwa kwa damu ni nani aisee, umekariri mno maisha.
Corona inapimwa kwa kuingizwa kifaa mfano wa kijiti kirefu kwa njia ya puani...kinaingizwa mpaka kinagusa kuta na kwenye koo ndani kabisa...alafu kinazungushwa zungushwa kukusanya ule tuseme ute kwa lugha nyepes alafu ndio hiyo sample inakwenda kupimwa maabara....hakuna cha damu wala nini...ndio maana imewezekana kuchukua fenesi,papai,mbuzi nk na ikaweza kufanana na sample ya binadamu.
 
2015 lilifanyika kosa kubwa sana

jk nafsi inakusuta sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakika Mkuu. Siamini kama maneno haya yametoka kinywani mwa Rais. Yaani ameamua kuidhalilisha Maabara Kuu ya Serikali anayoiongoza kiasi kile?? Kwamba haijui watendalo hata wakiletewa papai wanasema kuna corona??

Hili siyo lakuchukulia poa kuna shida mahali kwa Kiongozi huyu. Atawafanya Watendaji wa Wizara ya Afya wanaofanya kazi ktk mazingira magumu kukata tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mikakati iliwekwa baada ya kile kikao cha awali na wakuu vyombo. Walitaka kujua how effective hifaa na vipimo tunavyotumia ktk maabara ndio maana wakachukua sampuli za vitu mbalimbali na kuichanganya na sampuli za wa binadamu na kutuma maabara kuu.

Matokeo ndio hayo, vifaa vimeshindwa kutambua tofauti ya hizo sampuli na kutoa matokeo yasio halisia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nani ni mmiliki wa hivyo vifaa hapo maabara..??
 
Huku kijijini wazee huwa wana tabia ya kuchukua chai ya rangi na kuchanganya na kuchanganya na maji ili kupata rangi kama ya mkojo na kupeleka zahanati ya kijiji "kumpima" mtaalamu wa maabara waliyeletewa kama anajua kazi! Ole wako uwaambie kuna UTI utasikia wanasema "yule daktari hakuna kitu kabisa' kwahiyo walichofanya watu wa "usalama" hata kuku kijijini nilipo huwa wanafanya sana tu mkuu!
Hicho kijiji kiko nchi gani? Swala la kupeleka boga ukaambiwa unasafura ni kitu cha kawaida hapa kwetu. Mimi nimeuliza nchi nyingine, wewe unasema udhaifu wa vipimo.
 
AISEE HADI PAPAI LINAPIMWA???BADALA WABORESHE VIPIMO VYA RAIA WAO WANAPIMA KONDOO
mzee kumbuka vipimo vyote vya korona tumeletewa toka nje, utajiridhisha vipi juu ya sensitivity na specificity ya vipimo hivyo ulivyopewa kama msaada. SIKU ZOTE USIAMINI MSAADA AMBAO HUJAUOMBA
 
Ahahhahahahahaa leo ndio kanichekesha ni kama ze comedy show huyu mzee anaongea huku haamini alichotamka yani ili mradi tu upoyoyo huu jamani hahahhaha.Cha msingi watu washampuuza saiz
Bado muda wa kuhama nchi mnao.
 
COVID-19 ni really.. Watu wanaambukizwa kila uchwao, watu wanakufa kila uchwao.


Anajaribu kuwambia nn wananchi kwa kauli zake kama hizi??


Haya makauli ndio yamefanya Watu waache kwenda Hosp, wengine kutoroka, sababu ya maujinga kama haya.


Ni kama vile, Corona ni mradi nakwamba haipo ???.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unandugu yako au jiran yako kafa kwa corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Kinjekitile alipowaambia watu kuwa risasi ikipigwa sema maji na yenyewe itageuka kuwa maji watu walimuamini. Yani siku hizi kila mtu atumie akili zake. Kutegemea za mwenzako utakufa badala yake ooohooo.
 
mzee kumbuka vipimo vyote vya korona tumeletewa toka nje, utajiridhisha vipi juu ya sensitivity na specificity ya vipimo hivyo ulivyopewa kama msaada. SIKU ZOTE USIAMINI MSAADA AMBAO HUJAUOMBA

Na hapohapo kumbuka muamba ngozi huvutia kwake. Wanasiasa sio wakuwaamini

Mara zote hututoa kwenye mstari kwa malengo yao
 
Huoni kwamba kile kitu wanasema Kuingilia muhimili wa Bunge?
Mimi sina maneno kuhusu ruhusa ya speka au laaa,ninacho shangaa nikwamba Rais wako anaonyesha wazi kwamba yeye ndiye analiamrisha Bunge nini chakufanya,umeelewa?
Yupo sahihi,kwani wana ruhusa ya Spika? Atawalipa Mwenyekiti wao,kila kitu/sehemu kuna utaratibu na ni lazima ufuatwe.

macson

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upuuzi
Rais Magufuli akimuapisha Mwigulu Nchemba alisema, kuna haja ya kuangalia Laboratory yetu inayopima Corona maana serikali ilifanya sample ya vipimo mbalimbali kutoka kwa Mbuzi, Kondop, Papai, Fenesi na Oil na majibu yakatoka tofauti tofauti.

Amesema matokeo ya vipimo vya Mbuzi ni positive - ana corona, Papai lina corona, na Fenesi pia huku kondoo na oil ikionekana 'unspecified"...

Amesema hao wataalam wa maabara ni ama wanatumika na Mabeberu, miundombinu ya maabara ni mibovu au hawana utaalam katika eneo hilo.

Amemwelekeza Mwigulu wakashirikiane kutatua jambo hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom