Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Ameyasema hayo leo wakati wa kumuapisha Waziri wa Sheria na katiba kuwa vyombo vya usalama vilipenyeza sampuli kutoka kwenye mananasi, mafenesi, mbuzi, kondoo, nk kwa siri na kuzifanya ni za binadamu. Jambo la kushangaza matokeo ya baadhi ya sampuli hizo au yalionyesha yana maambukizi ya corona.
"...tunawasiliana na Madagascar na wamehaidi kututumia dawa inayotibu covid 19...." JPM
Mambo ni mengi ngoja niweke clip ya video!
Chanzo ITV....
assuming hajatulisha matango pori....yeye ni mkemia ina maana hajui kitu inaitwa "cross contamination" kwenye sample handling??
 
AISEE HADI PAPAI LINAPIMWA???BADALA WABORESHE VIPIMO VYA RAIA WAO WANAPIMA KONDOO
Kikanuni, lab tests zinapofanyika, sampuli husika huwa zinafanyika against quality control (QC) samples ili kuwa na uhakika na majibu unayotafuta. QC samples huwa majibu yake yanajulikana, kwa hiyo majibu ya QC yakiwa mabaya lazima majibu yote yatiliwe shaka. QC husaidia kujua aidha maabara nzima ni tatizo, au kifaa kinachotumika kufanya analysis ni mbovu, au wataalam ni mbumbumbu. Kwa maelezo hayo ya Rais, manake ni kwamba kama nchi hatuna maabara kwa ajili ya kupima COVID-19 na majibu yote yaliyotoka awali ni serious cheatings. Kwa nchi zenye uelewa Waziri wa afya na wataalam wake walitakiwa nyuma ya nondo siku nyingi sana.
Kwenye hili nimemwelewa vizuri Magufuli. Hata hivyo unapimaje kitu sensitive kama hii katika maabara ambayo hana ithibati kimataifa (internationally accredited lab)? Yaani unafanyaje vipimo katika maabara ambayo competency yake haijulikani kitaifa na kimataifa?! Kweli? Kila siku utamsikia Ummy Mwalimu akijinasibu ati ''tumepeleka sampuli kwenye maabara yetu ya Taifa kwa ajili ya uchunguzi zaidi''! Shit!
 
Yana corona
IMG_20200503_111648.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe akiongea maneno kumi unakuta moja tu ndio la kweli, angekuwa kama anavyosema corona ni ugonjwa mdogo angekuja zake dodoma aendelee kuchapa kazi.

Kwamba unapima mananasi wakati watu wanalalamika vipo havitoshi sababu maabara ni moja watu wapo Arusha wanatuma sumpuri Dar halafu wewe unaweka jam kupima mananasi!

Ni upumbavu, narudia tena ni upumbavu kuapisha waziri kwenye makazi binafsi ya Rais wakati Ikulu ipo Geita, Mwanza.

Taasisi ya urais sio mali ya mtu binafsi.

Utaongea mpaka unaingia kaburini

JPM anatenda

Utapewa likes kama zote ila kitaa hawaishi kwa maneno yako
 
Kwani hayo mafenesi na mbuzi na kondoo ukishika mwenye corona na huyo virus akatua kwenye hilo fenesi na hiyo sample ikapelekwa maabara unadhani maabara haita kwambia kuna corona. Ndio maana wataalamu wamegundua kwamba virus wa corona anaweza kukaa kwenye nguo au plastic au chuma kwa masaa kadhaa. Halafu kama maabara ya serikali inahitilafu nijambo kweli la kupepeleza na kutuambi sisi wananchi kwamba haiaminiki,yeye si ni Rais atoe hela itengenezwe au anunue nyingine. Kwa mantiki hiyo anakubaliana na wanaoponda kwamba takwimu za serikali ni za uongo!
 
Duuuh! sasa mananasi na mafenesi yana damu au hizo sampuli zake zilipenyezwa vipi ina maana hao waliokuwa wakipima walikuwa hawaoni na hawajui kuwa hizi sampuli siyo za binadamu jamani??

This dude seem to be so naive and ignorant!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwan uliambiwa corona lazima ipimwe kwa damu?
Unakimbilia kuita watu ignorant kumbe wewe ndio captain wa ma ignorant
 
Wewe nae mlugaluga embu weka ujinga wako pembeni, unataka kutufanya tuharibu swaumu zetu bure. Kuna kiwanda Cha kutengeneza vifaa Tanzania? Vifaa vyote mahospitalini tunaagiza tila nje Kama siyo vya misaada.
mzee kumbuka vipimo vyote vya korona tumeletewa toka nje, utajiridhisha vipi juu ya sensitivity na specificity ya vipimo hivyo ulivyopewa kama msaada. SIKU ZOTE USIAMINI MSAADA AMBAO HUJAUOMBA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli akimuapisha Mwigulu Nchemba alisema, kuna haja ya kuangalia Laboratory yetu inayopima Corona maana serikali ilifanya sample ya vipimo mbalimbali kutoka kwa Mbuzi, Kondop, Papai, Fenesi na Oil na majibu yakatoka tofauti tofauti.

Amesema matokeo ya vipimo vya Mbuzi ni positive - ana corona, Papai lina corona, na Fenesi pia huku kondoo na oil ikionekana 'unspecified"...

Amesema hao wataalam wa maabara ni ama wanatumika na Mabeberu, miundombinu ya maabara ni mibovu au hawana utaalam katika eneo hilo.

Amemwelekeza Mwigulu wakashirikiane kutatua jambo hilo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mtu hayuko sawa, yani hajiamini hata kidogo yani kila kitu akishindwa anasingizia mabeberu, cha ajabu akimaliza kuwasema anasema tumeongea na wenzangu ili mabeberu watusaidie grants, hata wazungu Nina amini hawana akiri yani ningekuwa ni Mimi huyu mtu hata Shilingi kumi Yangu hangekuja Kuiona hadi anaondoka madarakani yani ni mtu wa wasiwasi tuuuuu, akiona Jambo haliendi Kama anavyotaka yeye pia ni kuwatuhumu watumishi wa umma kuwa wanatumika na kuaagiza usalama kuwachunguza na kuwaathibu, huyu mzeee ataumiza watanzania Wendi Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,
Kwa mujibu wa Rais Magufuli wametuma sample kwa kuzipa majina ya binadamu baada ya kupimwa zimetest positive yaani zina corona

Hapa ndipo Magufuli ameprove uwana science wake

Magufuli ameonyesha uwezo mkubwa na kushauri nchi zingine zijaribu kupima sample zingine za mimea na wanyama kwa kutumia vipimo vya corona

Mbuzi wetu watakosaje kuwa na korona? Na tuwe makini na kauli zetu, bado tunauza nyama Dubai au ile ilikuwa trip moja tu?

3137EB04-B631-4000-92F0-7E35AE379010.jpeg
 
Spare my ribs, hahaaaa
Kweli kuangalia TBC inataka uwe na roho ngumu na nusu
Ila nyie watu wakatili wa nafsi aiseee...
Kuangalia tuu TBC inahitaji roho ngumu,
Sasa kumwangalia Huyo jamaa TBC inahitaji uwe bandidu na nusu.

Nilienda ugenini, wanaangalia TBC mda wote, Maisha yangu ile jioni yalikua magumu sanaaa, nje kuna mvua, chumbn hakwendeki maana unasubr mwongozo wa wenyeji, kuvaa earphones utaonekana wa ajabu, kuchezea simu mda wote nako hakuleti picha nzuri,
Nilitamani nianze kumchezea paka, bahat nzuri mtoto akaja akawa ananiongelesha.

Mzee mwenye nyumb anashangilia kila kitu, half anakuongelesha u comment...

Nilijitahd kuonesha unafk wa hali ya juu ile siku huku unajichekesha la sivyo naharibu hata kilichonipeleka.

Ila asikwambie mtu unafk wa nafsi yako unachoma moyoo aisee, naondoka huku najishangaa, hv kweli n mm wa kumshangilia yule jamaa...
Nilitamani nikatubu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao mabeberu wenyewe wanakufa kila siku,nasikitika sana kuwa na comforter in chief wa aina hii
 
Hakika Mkuu. Siamini kama maneno haya yametoka kinywani mwa Rais. Yaani ameamua kuidhalilisha Maabara Kuu ya Serikali a ayoiongoza kiasi kile?? Kwamba haijui watendalo hata wakiletewa papai wanasema kuna corona??

Hili siyo lakuchukulia poa kuna shida mahali kwa Kiongozi huyu. Atawafanya Watendaji wa Wizara ya Afya wanaofanya kazi ktk mazingira magumu kukata tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vipimo vya korona vimelalamikiwa sana sio na Magufuli tu wewe hauoni kama kuna shida na hivyo vipimo ? Haiwezekani uchukuliwe ute wa papai uonekane una korona
 
Back
Top Bottom