Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

Rais Magufuli: Maabara Kuu ya kupima sampuli za COVID-19 yaonyesha mafenesi, mapapai na mbuzi yana uambukizi

misasa mkuu una maoni gani juu ya hili hahahahaha..ila huyu rais katufanya sisi watoto aisee! Ama kweli huyu mzee kwa uongo tu ni professional. Anaonekana hata kwenye maisha yake ni mtu flani muongo muongo(mzee wa kamba)

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu asante sana kwa kuni mention kutaka kusikia maoni yangu, binafsi naunga mkono kwa context ya tafiti upingwa kwa tafiti.

Kingine mheshimiwa rais ni smart sana maana aliamua ku challenge technology(vifaa vya maabara), hii inamaanisha sio kinatengenezwa na MZUNGU kipo sahihi kabisa, kutokana na maelezo yake amechukua sampling kwenye mapapai, mafenesi,mananasi, mbuzi etc.

Mheshimiwa kafanya tafiti akukurupuka na kaamini juu ya tafiti yake na ana vifaa vya kutosha hadi rasilimali watu anao juu ya tafiti yake, mimi nani hadi nimpinge? Wakati hata bensen burner sina mkuu?

Je,kama muongo,wewe ulishafanya tafiti kwa kuchukua sampling ya mapapai, mafenesi,mbuzi juu ya COVID-19 hadi upinge?

Kumbuka no research no right to speak.
 
Nchi iliyojijengea heshima miaka mingi leo inakuja na ulozi Eti Mizizi ya mpapai ni dawa ya korona ila tunda lake (papai ) ukilipeleka maabara ni +ve Korona.
 
Jiwe is a scientist who is very unscientific. Anataka kuleta vurugu na taharuki tu. Hakuna vipimo ambavyo viko sahihi 100%. Viwe vya malaria, TB, nk. huwa vina "false positives" na "false negatives". Isitoshe vipimo hivi vilijaribiwa katika binadamu kwanza. Yeye ndiye wa kwanza kuvijaribu katika mapapai na kwale. Kama ilitokea vikawa positive kwa kwale ama mapapai haina maana kuwa positive zilizotokea kwa binadamu lazima ziwe za uongo. Na isitishe huko Marekani, corona virus walipatikana kwa mnyama anaitwa tiger. Wataalam wake wanajua sana ila ndio hivyo hasikilizi mtu. Huyu mkuu anachemsha sana. This is health science and not chemistry.

Wanabodi,

Kwa mujibu wa Rais Magufuli wametuma sample kwa kuzipa majina ya binadamu baada ya kupimwa zimetest positive yaani zina corona

Hapa ndipo Magufuli ameprove uwana-science wake.

Magufuli ameonyesha uwezo mkubwa na kushauri nchi zingine zijaribu kupima sample zingine za mimea na wanyama kwa kutumia vipimo vya corona.
 
Nashangaa anawalaumu waliokuwa wanapima kule maabara ya kitaifa kuwa wanamhujumu, kwa kutoa matokeo positive Ya corona, anadai kuwa walionekana ni positive ni uongo, eti alipeleka sample Ya Mbuzi, papai, na vitunguu eti wale watu Wa maaabara ya taifa walimuhujumu, eti na hizo sample hao wa maaabara Walisema ni positive aiseee anaone kuwa hakuna corona anasema hata ligi ya mpira atairuhusu iendelee aisee huyu mzeee akishindwa Jambo anasingizia mabeberu na kuwa anazungukwa, yani hahahahaha, Halafu nashangaaa anaenda anasema corona kweli ipo halafu anasema vipimo ni vya uongo watu waliokuwa wanapima wachunguzwe yani mmmmh simwelewi

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamani. Tusubiri. Time will tell. Kila mmoja ajilinde mahala alipo. Tusifanye mzaha. Tutakwisha.
 
Swaga za kijifukiza Leo sijasikia .... nimesikia eti ndafu ina Corona .... wajinga ndiyo waliwao ... puke
 
Kikanuni, lab tests zinapofanyika, sampuli husika huwa zinafanyika against quality control (QC) samples ili kuwa na uhakika na majibu unayotafuta. QC samples huwa majibu yake yanajulikana, kwa hiyo majibu ya QC yakiwa mabaya lazima majibu yote yatiliwe shaka. QC husaidia kujua aidha maabara nzima ni tatizo, au kifaa kinachotumika kufanya analysis ni mbovu, au wataalam ni mbumbumbu. Kwa maelezo hayo ya Rais, manake ni kwamba kama nchi hatuna maabara kwa ajili ya kupima COVID-19 na majibu yote yaliyotoka awali ni serious cheatings. Kwa nchi zenye uelewa Waziri wa afya na wataalam wake walitakiwa nyuma ya nondo siku nyingi sana.
Kwenye hili nimemwelewa vizuri Magufuli. Hata hivyo unapimaje kitu sensitive kama hii katika maabara ambayo hana ithibati kimataifa (internationally accredited lab)? Yaani unafanyaje vipimo katika maabara ambayo competency yake haijulikani kitaifa na kimataifa?! Kweli? Kila siku utamsikia Ummy Mwalimu akijinasibu ati ''tumepeleka sampuli kwenye maabara yetu ya Taifa kwa ajili ya uchunguzi zaidi''! Shit!
...na watu wanakufa kama nzige.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I wish angeileta hii habari angeileta hivi
Katika kuchunguza vifaa vya upimaji tumejiridhisha pasipo Shaka kwamba vifaa vinavyotumiwa vinaleta majibu yenye sintofahamu kwamba tumepima sample za mbuzi mananas etc zimetest positive
Hivyo Kama serikali tumejipanga kutafuta test kits zenye ubora wa Hali juu ili kupambana na maambukizi haya.

Sasa sijui anafeli wapi jamani 🤦 yanii Ana act Kama vile yeye sio mkuu wa nchi hausiki kabisa na hayamuhusu afu mwisho ndo anajitokeza kuonekana Hero with no solution or implementing something
Alishindwa Nini kuchukua hatua stahiki?? Kwanini vifaa visipimwe kwanza before kutumiwa?? Kwanini Basi Kama amehisi Kuna cheating asiwaadhibu hao wanahisiwa wanatumiwa na mabeberu??
Ananichosha anvyoact Kama housegirl Wakati ye ndo baba mwenye nyumba.
 
Mkuu asante sana kwa kuni mention kutaka kusikia maoni yangu, binafsi naunga mkono kwa context ya tafiti upingwa kwa tafiti.

Mheshimiwa kafanya tafiti na kaamini juu ya tafiti yake na ana vifaa vya kutosha hadi rasilimali watu anao juu ya tafiti yake, mimi nina hadi nimpinge? Wakati hata bensen burner sina mkuu?

Je,kama muongo ulishafanya tafiti na wewe hadi upinge?

Kumbuka no research no right to speak.
Mkuu acha uwongo!! Kafanyia wapi huo utafikiti? Hivi kwenda kupima fenesi kwa siri ndiyo utafikiti? Kama ni kweli kwanini asipublisize huo utafiti ili kuwaumbua mabeberu?
Taarifa ya kitafiti hutolewa kitaalam sio, kutaka cheap popularity kwa they know not.
 
Acha kukariri nani kakuambia sampuli ya kupima covid 19 ni damu?

Sampuli inayotumika ni nasal swabs na si damu, ambapo majimaji huchukuliwa katika pua za mnyama kwa kutumia kitu kama pamba na kisha hupelekwa maabara kuchunguzwa kwa kutumia PCR...

Watanzania embu tujifunze ku reason kabla ya kuchangia mada, pia niwaase vijana tumieni muda wetu wa akiba kujifunza vitu vipya ambavyo vitawaongezea kitu katika bongo zenu...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye oil au papai walichukua sampuli gani?
 
Nashangaa anawalaumu waliokuwa wanapima kule maabara ya kitaifa kuwa wanamhujumu, kwa kutoa matokeo positive Ya corona, anadai kuwa walionekana ni positive ni uongo, eti alipeleka sample Ya Mbuzi, papai, na vitunguu eti wale watu Wa maaabara ya taifa walimuhujumu, eti na hizo sample hao wa maaabara Walisema ni positive aiseee anaone kuwa hakuna corona anasema hata ligi ya mpira atairuhusu iendelee aisee huyu mzeee akishindwa Jambo anasingizia mabeberu na kuwa anazungukwa, yani hahahahaha, Halafu nashangaaa anaenda anasema corona kweli ipo halafu anasema vipimo ni vya uongo watu waliokuwa wanapima wachunguzwe yani mmmmh simwelewi

Sent using Jamii Forums mobile app
"Eti"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hayo mafenesi na mbuzi na kondoo ukishika mwenye corona na huyo virus akatua kwenye hilo fenesi na hiyo sample ikapelekwa maabara unadhani maabara haita kwambia kuna corona. Ndio maana wataalamu wamegundua kwamba virus wa corona anaweza kukaa kwenye nguo au plastic au chuma kwa masaa kadhaa. Halafu kama maabara ya serikali inahitilafu nijambo kweli la kupepeleza na kutuambi sisi wananchi kwamba haiaminiki,yeye si ni Rais atoe hela itengenezwe au anunue nyingine. Kwa mantiki hiyo anakubaliana na wanaoponda kwamba takwimu za serikali ni za uongo!
Ina maana hata wale 100 anaosema wamepona inaweza kuwa sio kweli, ni matango mwitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu acha uwongo!! Kafanyia wapi huo utafikiti? Hivi kwenda kupima fenesi kwa siri ndiyo utafikiti? Kama ni kweli kwanini asipublisize huo utafiti ili kuwaumbua mabeberu?
Taarifa ya kitafiti hutolewa kitaalam sio, kutaka cheap popularity kwa they know not.
Wewe na rais nani mwenye access ya resources(technology na vifaa vya maabara) na rasilimali za watu wakutosha?

Tafiti upingwa kwa tafiti mkuu.
 
Dunia kwa sasa kuna changamoto kubwa ya kupambana na Corona Virus Disease of 19, ni kweli wengi wameambukizwa na wengi wamefariki kutokana na ugonjwa huu. Familia zimepotea wapendwa wao wengi na chumi za mataifa mbalimbali kuzorota kutokana na ugonjwa huu. Pia shughuli mbalimbali za kijamii na kitaaluma kutoendelea kama ilivyo kawaida.
Katika mapambano yoyote kuna askari walio mstari wa mbele, katika ugonjwa huu wataalamu katika sekta ya afya ndio askari wetu wakuu. Wameamua kuyaweka maisha yao rehani ili tu kutupambania.
Wataalamu wa maabara ni sekta muhimu sana katika mapambano haya ya COVID-19, nasema wao ni muhimu kwani majibu yao ndio msingi wa mapambano yenyewe. Kukiwa na tishio la ugonjwa huu kuendelea na chanjo au matibabu kutopatikana mapema, ni kweli askari wetu wa maabara wanatakiwa kuja na majibu ya kuridhisha ya namna ya kutafsiri majibu ya kiamabara.
Katika mapambano ya COVID -19, tunategemea sana kifaa kinachoitwa RT-PCR ambacho kinapima RNA au vinasaba taarifa vya kirusi chenyewe cha CORONA.
Kifaa hiki si hitimisho la kusema kuwa mtu huyu ana ugonjwa wa COVID-19 au ni mtu tu anayeishi na maambukizi ya corona.
Naomba hapa mnielewe kuwa si wote watakaokutwa ni chanya kwenye kipimo hiki cha Corona basi wanaumwa COVID -19.
Mgonjwa wa COVID-19 no yule tu mwenye dalili za ugonjwa na akiwa na hizo dalili na kipimo kuonesha kuwa yupo chanya kwa vinasaba taarifa vya COVI-19 ndio tunasema yeye ni mgonjwa wa COVID-19.
Siyo wote watakaokutwa ni chanya kwa vinasaba taarifa RNA vya COVI-19 basi ni wagonjwa, wengine ni kuwa inawezekana miili yao imeshapambana na kirusi hiko na kukififisha, hivyo kutokuwa na ugonjwa kitaalamu wanaita "active disease". Aidha kila kipimo kina sehemu yake na kuwa na majibu chanya yasiyo halisi (False postive) au majibu hasi yasiyo halisi (False negatives)
Pia siyo wote watakaokutwa ni chanya ni wagonjwa, kwani wengine miili yao inakuwa imehifadhi tu taarifa ya kuwa katika kipindi kimoja ama kingine walishwahi kuwa na virusi hivyo mwilini mwao.
Yule mwenye dalili tu ndio mwenye "active disease".
Sasa tunakuja kwenye swali la msingi, je taaluma ya maabara imeshindwa kuja na kipimo cha kuweza kutofautisha baina ya mgonjwa na wale ambao si wagonjwa?
Je dunia nayo imeshindwa kutofautisha makundi hayo hapo juu.
Ujumbe wa leo ni kuwa bado dunia haijaweza kumfahamu vizuri huyu kirusi COVI-19, bado tupo kwenye mashimo yaliyo na giza. Hakika tunahitaji sasa wana taaluma wa maabara na wanasayansi wengine duniani kuja na majibu ya hakika ya kuweza kutofautisha wagonjwa wa COVID-19 na watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Corona -19.
Hakika tumebaki kwenye mtanzuko, je ni nani wa kutohokoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari, na jaribu kuwaza na kupembua mawazo ya walio wengi na yale ya kiongoz wetu wa nchi, kwa kweli nakosa jibu ni nan mkwel kat ya hiz pande mbili maana mtukufu amekil ugonjwa upo ila x ule wanao sema upande wa pili.

Pia, anasema kipimo cha maabara ya taifa hakifanya kazi vizuri au wale watu wa maabara wanakuja n majibu yao kutoka mfukon. Sasa hivi wale waliopimwa ni kukutwa n Corona inakuwaje sa maana wamezurumiwa maisha yao, mtu hana ila amewekwa na aliye kuwa nao na kama kweli hao watu wa maabara wamefanya hila watakuwa ni wahujumu uchumi na wanahitajiki kupewa adhabu kali kabisa.

Uchunguzi ufanyike kwao na wanahitajika kusimamishwa mara moj kuanzia PM, UMMY, MGANG MKUU NA HAO MAABARA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom