Dunia kwa sasa kuna changamoto kubwa ya kupambana na Corona Virus Disease of 19, ni kweli wengi wameambukizwa na wengi wamefariki kutokana na ugonjwa huu. Familia zimepotea wapendwa wao wengi na chumi za mataifa mbalimbali kuzorota kutokana na ugonjwa huu. Pia shughuli mbalimbali za kijamii na kitaaluma kutoendelea kama ilivyo kawaida.
Katika mapambano yoyote kuna askari walio mstari wa mbele, katika ugonjwa huu wataalamu katika sekta ya afya ndio askari wetu wakuu. Wameamua kuyaweka maisha yao rehani ili tu kutupambania.
Wataalamu wa maabara ni sekta muhimu sana katika mapambano haya ya COVID-19, nasema wao ni muhimu kwani majibu yao ndio msingi wa mapambano yenyewe. Kukiwa na tishio la ugonjwa huu kuendelea na chanjo au matibabu kutopatikana mapema, ni kweli askari wetu wa maabara wanatakiwa kuja na majibu ya kuridhisha ya namna ya kutafsiri majibu ya kiamabara.
Katika mapambano ya COVID -19, tunategemea sana kifaa kinachoitwa RT-PCR ambacho kinapima RNA au vinasaba taarifa vya kirusi chenyewe cha CORONA.
Kifaa hiki si hitimisho la kusema kuwa mtu huyu ana ugonjwa wa COVID-19 au ni mtu tu anayeishi na maambukizi ya corona.
Naomba hapa mnielewe kuwa si wote watakaokutwa ni chanya kwenye kipimo hiki cha Corona basi wanaumwa COVID -19.
Mgonjwa wa COVID-19 no yule tu mwenye dalili za ugonjwa na akiwa na hizo dalili na kipimo kuonesha kuwa yupo chanya kwa vinasaba taarifa vya COVI-19 ndio tunasema yeye ni mgonjwa wa COVID-19.
Siyo wote watakaokutwa ni chanya kwa vinasaba taarifa RNA vya COVI-19 basi ni wagonjwa, wengine ni kuwa inawezekana miili yao imeshapambana na kirusi hiko na kukififisha, hivyo kutokuwa na ugonjwa kitaalamu wanaita "active disease". Aidha kila kipimo kina sehemu yake na kuwa na majibu chanya yasiyo halisi (False postive) au majibu hasi yasiyo halisi (False negatives)
Pia siyo wote watakaokutwa ni chanya ni wagonjwa, kwani wengine miili yao inakuwa imehifadhi tu taarifa ya kuwa katika kipindi kimoja ama kingine walishwahi kuwa na virusi hivyo mwilini mwao.
Yule mwenye dalili tu ndio mwenye "active disease".
Sasa tunakuja kwenye swali la msingi, je taaluma ya maabara imeshindwa kuja na kipimo cha kuweza kutofautisha baina ya mgonjwa na wale ambao si wagonjwa?
Je dunia nayo imeshindwa kutofautisha makundi hayo hapo juu.
Ujumbe wa leo ni kuwa bado dunia haijaweza kumfahamu vizuri huyu kirusi COVI-19, bado tupo kwenye mashimo yaliyo na giza. Hakika tunahitaji sasa wana taaluma wa maabara na wanasayansi wengine duniani kuja na majibu ya hakika ya kuweza kutofautisha wagonjwa wa COVID-19 na watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Corona -19.
Hakika tumebaki kwenye mtanzuko, je ni nani wa kutohokoa?
Sent using
Jamii Forums mobile app