Rais Magufuli: Makongoro na Madaraka Nyerere mnaishi Butiama lakini wajumbe wamewapa kura 5 na 2, Tungewasaidiaje?

Rais Magufuli: Makongoro na Madaraka Nyerere mnaishi Butiama lakini wajumbe wamewapa kura 5 na 2, Tungewasaidiaje?

Rais Magufuli amewapongeza watoto wa baba wa taifa Makongoro na Madaraka kwa kuelewa demokrasia na kutolalamika baada ya uteuzi wa wagombea ubunge kufanywa.

Dkt. Magufuli amesema Makongoro na Madaraka hawaishi Mtwara wala Dsm bali wapo hapo hapo Butiama lakini wajumbe waliwapa kura 5 na 2, sasa Kamati Kuu ingewasaidiaje?

Pamoja na kuwa ni watoto wa baba wa taifa hawajalalamika, nawapongeza sana amesema Dkt. Magufuli.

Maendeleo hayana vyama!
Alimusaidiaje katambi shinyanga?

Pumbavu kabisa.
 
Hii kauli ya kuwalaumu wajumbe wakati yeye na Kamati kuu waliwatoa wale waliopendekezwa na wajumbe...

Huku Ni kutafuta huruma kwa wale walioenguliwa ktk Kamati kuu... Ukweli ndani ya CCM upo msuguano mkali Sana.
Bahati mbaya wanaogopa kufungua midomo, yule Masele wa Shinyanga Mjini yupo kimya tu lakini ana lake moyoni.
 
'Kilichonisikitisha' zaidi ni kwamba inakuwaje hata 'Wasaidizi' wake tu 'Taarifa' kama hii wanashindwa kuwa nayo hadi Mheshimiwa 'anakosea' hivi?
Issue si wasaidizi kuwa na taarifa sahihi.
Issue ni uwezo wa kutunza kichwani taarifa sahihi na kuzitoa tena kwa usahihi.
Huwezi kuwa sahihi wakati wote.
 
Gwajima anaishi kawe ila alifeli ukambeba
Akaja Katambi ukambeba

Mama maria "nimelazimishwa kuja kwenye mkutano kwa sababu sikuwa na cha kuongea(kusifia)"
Duuuh!
 
Attachments

  • 2508834_IMG_9895.mp4
    400.7 KB
These days Meko anafuka sana majukwaani. Kuna mambo mengine bora kukaa kimya tu kuliko kuonyesha unafiki na ujuha mchana kweupe
 
Rais Magufuli amewapongeza watoto wa baba wa taifa Makongoro na Madaraka kwa kuelewa demokrasia na kutolalamika baada ya uteuzi wa wagombea ubunge kufanywa.

Dkt. Magufuli amesema Makongoro na Madaraka hawaishi Mtwara wala Dsm bali wapo hapo hapo Butiama lakini wajumbe waliwapa kura 5 na 2, sasa Kamati Kuu ingewasaidiaje?

Pamoja na kuwa ni watoto wa baba wa taifa hawajalalamika, nawapongeza sana amesema Dkt. Magufuli.

Maendeleo hayana vyama!
Kila kitu "maendeleo hayana chama" sasa hapo waliowakata hao watoto wa Nyerere ni CHADEMA?
angesema uongozi hauna kujuana, yaani jamaa hajui kukonekti maneno kabisa.
anaami yeye mwenyewe ndio anajua nondo za madaraja zinapouzwa!

Kikweye
 
Katambi

Gwajima

Silinde

Kimei

Pauline Gekul

Na wengineo

....mbona walibebwa? Au mbeleko zao ziliwatosha wakati kwa wengine zilipwaya?
Mbeleko zilipwaya watoto wa Nyerere, kura 5 , Na 2
 
magufuli ni mnafiki,KATAMBI kapata kura 7 lakini kambeba,alishindwa mini kwa madaraka na makongoro?
 
Rais Magufuli amewapongeza watoto wa baba wa taifa Makongoro na Madaraka kwa kuelewa demokrasia na kutolalamika baada ya uteuzi wa wagombea ubunge kufanywa.

Dkt. Magufuli amesema Makongoro na Madaraka hawaishi Mtwara wala Dsm bali wapo hapo hapo Butiama lakini wajumbe waliwapa kura 5 na 2, sasa Kamati Kuu ingewasaidiaje?

Pamoja na kuwa ni watoto wa baba wa taifa hawajalalamika, nawapongeza sana amesema Dkt. Magufuli.

Maendeleo hayana vyama!
Alimsaidiaje Katambi. Anhetumia mbinu hiyo hiyo kumsaidia na Madaraka au Makongoro
 
Makongoro ni kama Le Mutuz watoto wa wakubwa ambao hawakutumia fursa vizuri.Utawabebaje sasa!

Sasa hawa watoto wa Mwalimu watabebwa mpaka lini? Hivi sasa tu bado wanakaa nyumbani na watu wana wajukuu. tunawalisha kupitia pension anayopata mama yao!!! Makongolo alishabebwa sana kwani alikuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki na sasa nadhani jumbe wa NEC ya ccm!! Mama yao ana viwanja kwenye prime areas kule Mbezi Beach[ alikuwa anafuga kuku huko enzi hizo] ambazo wangeziendeleza wangeweza kujikimu lakini kwavile wanalishwa na state hawajishuhulishi!! Ni watu wazima waache wajitegemee kama wenzao wanavyojitegemea.
 
'Kilichonisikitisha' zaidi ni kwamba inakuwaje hata 'Wasaidizi' wake tu 'Taarifa' kama hii wanashindwa kuwa nayo hadi Mheshimiwa 'anakosea' hivi?
Jamaa hashauriki wasaidizi wake waliojaribu kumrekebisha anawatumbua
Mtu kama huyu dawa ni kumuacha aaibike kwa umma
 
Madaraka anaishi Canada na,

Makongoro anaishi Arusha.
Acha uongo, mm si timu JPM lakini Madaraka yupo Butiama siku zote ama nyingi. Ndiye msimamizi wa mji pale.

Makongoro ndie anatembea tembea..
 
Back
Top Bottom