Rais Magufuli: Mpaka sasa Tanzania (Bara&Visiwani) hatuna mgonjwa wa Corona. Nawasihi watanzania kuchukua hadhari

Kasisitiza sana kuhusu tahadhari za gonjwa KORONA wakati akiwa anafungua KARAKANA.
Tuchukue hatua, gonjwa baya hili
 
Akitoka anaenda Kimara kwa ndugu wa Msigwa Peter

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
Jamani tuhamasishe maeneo ya kunawa mikono na sabuni kwenye sehemu zote za mikusanyiko, hata makanisani, misikitini, sokoni, mashuleni, hospitalini, vituo vyote vya usafiri, nk.

Kunawa kwa maji safi na sabuni angalao kwa sekunde 20-30 iwe desturi mpya.
 
Amekosa kazi mzee kinganganizi hataki hata mawaziri wake waonekane wakizindua miradi, karakana izinduliwe na waziri wa ulinzi. Bado Mbowe michango inaendelea.
 
Wale aliowaita marafiki zetu China si wanaendelea kuingia nchini wkt nchi zingine zimepiga ban?
 
“Tanzania hatujapata corona ila hatuwezi kujiweka pembeni lazima tuchukue tahadhari, Corona inaua kwa haraka sana, Watanzania tusipuuze, tuchukue hatua za kujikinga, wanaopenda kusafirisafiri kama safari sio ya lazima usisaifiri na hatutotoa vibali vya Watu kusafiri hovyo” - JPM

“Narudia Watanzania tuchukue tahadhari, Waziri amesema tusishikane mikono, tusibusiane sasa sifahamu usiku watafanyaje ila napo unaweza kukwepa usibusu na mambo yakawezekana tu na ni raha tu, ila kiukweli corona ni hatari, haijafika Tanzania ila tujikinge”-JPM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti mnaweza msibusiane mambo yakawezekana na ikawa raha tuu. Interesting

Ndo akili zake huyo, yaani hotuba yake siku zote usikae karibu na watoto wala unaowaheshimu.
Ni kama mondi, hachelewi kumwaga mitusi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…