digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,926
- 17,880
Kwa hili la kuzuia watu kusafiri ni muhimu zaidi,ila na mikusanyiko ya watu isiyo na tija ipigwe marufuku
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mpingaji sio mpinzani!Yeye kama raisi wa nchi amechukua hatua gani? Magufuli is a country bumpkin!(in Kiranga voice)
Maana halisi ya kuanza safari kuelekea Mwanza lakini unajikuta gari limefunga breki mko Malawi!🤯Hatua nyingine tuliochukua kama Taifa hii hapa![emoji16][emoji16][emoji16] View attachment 1386843
Karibu.
Unaweza pia kuona kupitia Channel ten tv na ITV.
Up dates;
Rais Magufuli ameishukuru serikali ya Germany kwa msaada walioutoa kujenga karakana hiyo ya kisasa.
Pia Rais Magufuli amempa balozi barua maalumu ya shukrani kwa counvillor Mikael wa Germany.
Kadhalika Rais Magufuli ametumia fursa hiyo kuwataka watanzania wajihadhari na ugonjwa huo hatari.
Rais Magufuli amevitaka vyombo vyote vya habari kutoa elimu kuhusu corona.
Kadhalika amewataka wananchi kutosafiri hovyo na amemuagiza CS kutotoa vibali vya kusafiri kwa safari zisizo muhimu.
Rais Magufuli amesisitiza hata ndege ya ATCL inayofanya safari za India ikirejea kesho haitasafiri tena kwenda huko.
Maendeleo hayana vyama!
----------
Kupitia hii hotuba yangu ya leo naomba tu watanzania wote mkachukue tahadhari kila mmoja kujikinga na ugonjwa wa Corona, upo na ni hatari unaua kwa haraka. Tanzania bara na Visiwani hakuna mgonjwa ila haina maana kwamba tusichukue tahadhari.
Niwaombe ndugu zangu tusipuuze ugonjwa huu. Kwa wale wanaopenda kusafiri safiri sana, kama safari sio ya lazima sana usisafiri. Nimeshatoa taarifa kwa Katibu Mkuu Kiongozi kwamba vibali vya kusafiri viwe kwa safari maalum
Tusishikane mikono, tusibusuane, sasa sifahamu usiku watafanyaje, lakini napo unaweza tu usibusu mambo yakawezekana na ni raha tu.
Na hii tahadhari msiwaachie viongozi tu ndio wazungumze,kila mmoja kwenye familia yetu tutoe elimu ya tahadhari. mashuleni walimu watoe tahadhari kwa watoto wetu, kwenye makambi etc ili tuweze kudhibiti hili gonjwa lisiweze kuingia nchini mwetu, gonjwa hili linaharibu uchumi wetu.
Niwaombe wahariri wa magazeti ikiwezekana kila siku kwenye gazeti watoe tahadhari ya ugonjwa wa Corona. Kwenye Tv na redio zetu hata kabla ya kutangaza taarifa ya habari basi wapitishe mistari ya tahadhari ya ugonjwa huu. Tukidharau ndugu zangu tutakwisha, mpaka sasa wanatibu tu symptoms lakini dawa ya kuponesha Corona haipo. Kupitia meseji hii ambayo naitolea hapa jeshini Lugalo ikawaguse watanzania.
Vyombo vya habari mkilisimamia hili tutashinda hii vita, unapopiga Muziki weka na tangazo la corona ili anaecheza na kubinuka amevaa kichupi anaweza akavaa hata gauni kwa kusikia tu neno corona, wekeni Dakika hata moja ya kuelimisha, Wanahabari hili ni jukumu lenu kubwa
Niwaombe viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali kila mmoja katika imani yake tuendelee kumuomba Mungu aweze kutusaidia, Mungu anaweza kila kitu.Hata wakati wa Sodoma na Gomora tahadhari zilitolewa Watu walidharau wakaangamia, tahadhari tuzizingatie,Nchi zimepunguza safari hata sisi Ndege yetu inayoenda India ilienda jana ikirudi leo haitoenda tena. Nchi yetu inaenda vizuri kiuchumi, janga hili litaturudisha nyuma.
[/QUO
Yesu Kristo atuepushie mbali na hili balaa.
Tusibusiane, sasa sifahamu usiku watafanyaje; lakini napo unaweza tu usibusu mambo yakawezekana, na ni raha tu.
Duh!Unapopiga muziki, weka na tangazo la corona ili anaecheza na kubinuka amevaa kichupi anaweza akavaa hata gauni
Bashiru ameonewa sana kupewa jukumu asilolimudu.Kwakweli atafute washauri wazuri wa masuala ya siasa...bashiru Na PhD yake ni hopeless kabisa...yani movies wanazocheza za kitoto sana.
Kwani alikuahidi kuwa atakuondolea Corona?Habari yenu wakristo kwa waislamu!
Huu ndio wakati muafaka sana wa nyie (wakristo na waislam) kumuomba Mungu awapambanie dhidi ya ugonjwa wa Corona, au mnataka kuendelea kufa? Yule Mungu wenu anayeitwa Yahweh (in Hebrew) na Allah (in Arabic), yule Mungu ambaye alijithibitisha kwa Abraham... ndiye Mungu mnaetakiwa kumlilia sasa awaweke mbali na hili janga la huu ugonjwa.
Kwa maana huyu Mungu ni Mungu aliyekuwepo tangu milele yote na ataendelea kuwepo, ni Mungu anayeweza yote, anayejua yote na ndiye aliyeumba huu ulimwengu wote. Mbali na hizo sifa, hamuishii hapo, ndiye Mungu mtakatifu, mwenye haki, mkamilifu na yupo kila mahali. Lakini sifa ya muhimu sana kwa wakati huu juu yenu, ni Mungu anayesikiliza maombi na anajibu pia.
In reality, huyo Mungu mwenye hizo sifa zote hapo juu, ni Mungu mzuri sana, na hawezi kuacha mteseke.. ni lazima atasikia maombi yenu na kwa kuwa ni Mungu wa haki, mkamilifu na mwenye huruma, hawezi kuwaacha viumbe wake msio na hatia juu ya janga la Corona mteketee.
Hebu muombeni basi ainusuru dunia, yeye ni muweza yote, sio?
Hapana mkuu! Aliahidi kuniletea Corona 😀
Ninachojua kuna nguvu iliyo juu sana ya nguvu zote hiyo nguvu ndiyo inao uwezo wa kuruhusu na kutoruhusu na kila maamuzi yanayo sababu ila binadamu wameitafsiri nguvu hiyo ni mungu lakini wanapishana katika kuheshimu nguvu hiyo ndipo ikazaliwa dini viongozi wa hizo dini ndiyo wakaleta hizo falisafa/teolojia hapo kwenye teolojia kuna Dini nyingi zilizaliwa na zitendelea kuzaliwa. Ila wewe na mimi tujiulize Shwali rahisi tu kwanini tupo duniani? Ni nani nani aliyemwambia mwanamke kwanza utakapomzaa mtoto umnyonyeshe, Ni nani hasa aliyetengeneza Mtu mweusi aishi kwenye jua Kali na misitu minene hivi na magonjwa makubwa na bado akahimili hapohapo akatengeneza mtu mweupe kwenye baridi Kali na wanashindwa kumudu kuishi vizuri kwenye ardhi ya mtu mweusi.Habari yenu wakristo kwa waislamu!
Huu ndio wakati muafaka sana wa nyie (wakristo na waislam) kumuomba Mungu awapambanie dhidi ya ugonjwa wa Corona, au mnataka kuendelea kufa? Yule Mungu wenu anayeitwa Yahweh (in Hebrew) na Allah (in Arabic), yule Mungu ambaye alijithibitisha kwa Abraham... ndiye Mungu mnaetakiwa kumlilia sasa awaweke mbali na hili janga la huu ugonjwa.
Kwa maana huyu Mungu ni Mungu aliyekuwepo tangu milele yote na ataendelea kuwepo, ni Mungu anayeweza yote, anayejua yote na ndiye aliyeumba huu ulimwengu wote. Mbali na hizo sifa, hamuishii hapo, ndiye Mungu mtakatifu, mwenye haki, mkamilifu na yupo kila mahali. Lakini sifa ya muhimu sana kwa wakati huu juu yenu, ni Mungu anayesikiliza maombi na anajibu pia.
In reality, huyo Mungu mwenye hizo sifa zote hapo juu, ni Mungu mzuri sana, na hawezi kuacha mteseke.. ni lazima atasikia maombi yenu na kwa kuwa ni Mungu wa haki, mkamilifu na mwenye huruma, hawezi kuwaacha viumbe wake msio na hatia juu ya janga la Corona mteketee.