Suala la Corona virus Sasa hivi Ni mlipuko wa dunia nzima. Ni kweli media imechangia Sana watu kupanick, lakini hapa kwetu Tanzania tunasubiri Nini kuchukua hatua stahiki. Maana so far naona vikauli kauli na visalamu vya utani utani tu lakini juhudi za ukweli na serious hakionekani Kama kwingine. Au ndio mpaka ije?
Kenya na Rwanda wao wameshaconfirm na wanachukua hatua kali za tahadhari Kama kuzuia watu safari zisizo za lazima nk. Nchi zilizoendelea ndio usiseme wamefunga mashule, na kusimamisha shughuli zote za mikusanyiko, huku Jana tu Jmamosi harusi kama kawa.
Leo mwendo kasi kama zote, mipira inaendelea. Je, hii ni sawa? Corona itakapofika nani tumpake damu za Watanzania watakaokufa? Maana Wachina wanakuja, watalii Arusha kama wote, na mipaka ipo free to as if sisi tuna mkataba na Mungu kuwa haitofika kwetu.
Hivi ni pesa tu inatufanya tunajisahau namna hii?
Disappointed.