Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Mzee kuna marupurupu yakutosha, yy ndo kila kitu akiamua kuchota anachota tu
 
Marehemu Mkapa alipokuwa Mr Clean alipoapishwa alitutangazia mali zake ikiwemo nyumba,magari na mashamba lakini alipotoka hakututajia tena.
Kuna namna ambayo watu wakipata madaraka wanawaona wengine kama hawajui kitu.
 
Mimi simpendi wala simchukii,nipo huru napoona kafanya zuri kwa mtazamo wangu naeleza hilo jambo kuwa ni zuri na pia napoona upungufu pia nasema na ndio maana utaona hata humu nimeeleza mapungufu yake.

Binafsi sina chuki nae wala mapenzi nae,hivyo sina upande kwamba nijilazimishe kumzungumzia mazuri tu au mabaya tu,nipo huru kutoa maoni yaliyo huru pasina upande.
 
Daah ngoja ntajibu baadae, na ntajibu hapahapa public[emoji1787][emoji1787]
Sidhani kama utaweza, ngoja tuone! Ila nimehisi tu una kauzoefu humu. Haya tuendelee kujadili marupurupu ya mkulu[emoji39][emoji39]
 
Sidhani kama utaweza, ngoja tuone! Ila nimehisi tu una kauzoefu humu. Haya tuendelee kujadili marupurupu ya mkulu[emoji39][emoji39]
Haya marupurupu hayakusaidii kitu mkuu, yatakupa stress tu, tafuta hela
 
Hata nikitafuta vipi, 9m kwa mwezi sitafika. Naomba niwe mpole katika hili, niendelee kujadili nisiyoyaweza.. hahaha!
Kwa kweli, maana wanatuhadaa kwa.kutaja mishahara yao pasipo kuwela wazi other benefits ili tupime
 
Naweza kusema huyu Anko ni mzalendo sana, sijui kama kuna Rais mwingine Afrika anayelipwa hela kama hii.

Anko Magu analipwa mil. 9 tuu. Kiasi ambacho ni kidogo kuliko hata mshahara wa wabunge ambao wao hulipwa mil 12....
Haya na Yule 'Mbelgiji Mweusi' nae atuambie au atuweke wazi hao 'Mabeberu' wake wa Kijerumani, Kimarekani na Kibeleshi wanamlipa Kiasi gani?
 
Haya na Yule 'Mbelgiji Mweusi' nae atuambie au atuweke wazi hao 'Mabeberu' wake wa Kijerumani, Kimarekani na Kibeleshi wanamlipa Kiasi gani?
Bila wewe kwenda Dodoma na Bashite kumpiga risasi angefikaje Belgium? CCM wakienda ulaya kuomba omba misaada huwaita wazungu ni wafadhili wahisani lakini hao hao wazungu wakikataa ujinga upumbavu uonevu unyanyasaji wa CCM kwa wapinzani ndipo hugeuka na kuwaita wanaume wenzenu mabeberu utazani nyinyi CCM ni mbuzi jike
 
Mimi simpendi wala simchukii,nipo huru napoona kafanya zuri kwa mtazamo wangu naeleza hilo jambo kuwa ni zuri na pia napoona upungufu pia nasema na ndio maana utaona hata humu nimeeleza mapungufu yake...
Mabaya ni mengi kuliko mazuri ingawa mabaya mengi huwanufaisha wale waotumwa kuyatekeleza na hao ndiyo hupiga kelele kwani uwepo wa mabaya ni manufaa kwao, Mfano kuwabambikia kesi wapinzani au ununuzi wa covid 19 kwenye kesi kuna Rushwa na kwenye ununuzi kuna 10% wanufaika wa mabaya huwa hawataki mtukufu akosolewe kwani akiacha mabaya watakosa pa kupiga pesa.
 
Bado tu unatamani Mimi niwe 'Mume' wako kama ambavyo umekuwa ukitaka hivyo na 'Kunisumbua' mara kwa mara Maji Mafupi kule nje ya hapa?
 
Wajinga ndio waliwao...endelea kuaminu hivyo hivyo ! Je ametaja posho achilia mbali why alipwe 9 M ilhali kila kitu anapitiwa kwa kodi za wananchi na anapokea kiasi hicho pia bila makato! Think Twice
 
Sikulazimishi kunielewa,muhimu umekubali tu kuwa kweli una chuki na umeshindwa kutenganisha kati ya chuki na kukosoa sasa kwa hali hiyo lazima ushindwe kunielewa navyosema simchukii wala simpendi. Wewe haupo huru unachoeleza humu si kukosoa bali ni chuki na mwenye umekubali. Sasa tofauti mimi sina chuki nae hivyo nikikosoa nakosoa kwa sababu naona hilo jambo halipo sawa na nikipongeza napongeza kwa sababu naona ni jambo zuri haina maana nampenda. Sasa wewe unataka kusema et haiwezekani mtu kupongeza na kukosoa kwamba lazima mtu awe na chuki au mapenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…