Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Rais Magufuli: Mshahara wangu kwa Mwezi ni Sh. Milioni 9.5. Nitatoa salary slip...

Njaa zinawasumbua sasa sijui tusifie ama tujadili? Tutajuaje kama kweli anakula mil 9
Hakuna mwenye uhakika wa hiyo milion 9 kwani hakuna mwenye uthubutu wa kuidhibitisha popote, pesa inayotumika kwa mambo ya hovyo kama mfano kuwabambikia kesi wapinzani nk ni bora ingekuwa inatumika kuboresha mishahara ya watumishi wa umma kuliko kukaa kututengenezea sinema za kuwahadaa watanzania kila kukicha
 
Si ajabu anapokea milioni zaidi ya arobaini kwa mwezi.

Bado hajapiga mapesa ya wizi wa hapa na pale.

Posho na mapochopocho!

Wakati kuna mwalimu analipwa laki mbili kwa mwezi na anatakiwa kulipa kodi za kila aina!

Aiseee....
Pesa inayotumika kudidimiza demokrasia ingetosha kupelekea mwalimu kulipwa milion 2 kima cha chini, lakini wapo radhi kuwanunua wapinzani kufanya mambo yasiyo na tija kwa Taifa badala ya kuboresha mishahara ya watumishi wa umma
 
Kusema yeye ni sawa....how can we verify kwamba anasema ukweli?

Kuchukulia anasema ukweli on anything ni one of the stupidiest naive decision you have ever made...

Everybody knows how unreliable this guy is!
Hujawahi kumzungumzia vizuri huu jamaa yani kila anapomzungumzia huu jamaa basi ni mabaya ya huyu jamaa,hii inaonesha unamchukia.
 

Aweke salary slip yake hadharani huyo ni muongo wa hali ya juu.
Naweza kusema huyu Anko ni mzalendo sana, sijui kama kuna Rais mwingine Afrika anayelipwa hela kama hii.


Anko Magu analipwa mil. 9 tuu. Kiasi ambacho ni kidogo kuliko hata mshahara wa wabunge ambao wao hulipwa mil 12.

Leo kwenye hafla ya kumwapisha Naibu waziri wa Madini, Mheshimiwa Rais alijikuta akitaja kiasi anacholipwa wakati akiongelea suala la mishahara ya watumishi waliokuwa TMA baadae kubadilishiwa sekta, watumishi hao ambao Rais alidai waliboronga huko TMA wanapaswa wasilipwe mil 10 tena mishahara yao ipunguzwe na kuongeza kuwa asiyetaka aache kazi. Maana kuna wengine wanalipwa mishahara ya ajabu sana.

Kwa mshahara huo wa Magu watumishi wengi mno wenye mshahara kumzidi, nashawishika kusema kuwa Rais Magufuli ana mabaya yake lakini ni Rais bora sana kwenye mambo mengi.
 
Rais kama huyu hutokea mara moja ndani ya miaka 1000, tumebahatika kumpata 2015, angalia miradi mikubwa anavyopambana kuisimamia na kuhakikisha hakuna pesa inayoibwa, tena akilipwa mshahara mdogo kuliko hata wakurugenzi wengi wa taasisi mbali mbali waliopo serikalini. Sio binadamu wa kawaida anayeweza kuweka pembeni tamaa ya pesa na kupambania maendeleo ya nchi yake.
Kamtumbua naibu et hajui kusoma atashindwa kusoma mikataba ya madini na anaona sifa kufanya hivyo wakati huo huo kasahau kuwa anajisifu kuwa wale anaowateuwa wote amepitia mafile yao anawajua vizuri.

Ni kweli marais wa aina hiyo hutokea mara moja ndani ya miaka buku.
 
Hujawahi kumzungumzia vizuri huu jamaa yani kila anapomzungumzia huu jamaa basi ni mabaya ya huyu jamaa,hii inaonesha unamchukia.
Kusema mabaya au mapungufu ya mtu siyo kumchukia bali ni kumsahihisha ajirekebishe
 
Kamtumbua naibu et hajui kusoma atashindwa kusoma mikataba ya madini na anaona sifa kufanya hivyo wakati huo huo kasahau kuwa anajisifu kuwa wale anaowateuwa wote amepitia mafile yao anawajua vizuri.
Tanzania kuna vioja na hicho ni mojawapo ya kioja na pia ni Aibu kwa kile kikundi cha kuwachuja wateule kabla ya uteuzi kamili, kwa Lugha ingine kamati za uteuzi zina mapungufu? Nani wa kuwajibika kwa hilo kosa?
 
CCM hawana huruma na wananchi wapiga kura wameunajisi kuubaka kuulawiti uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani na bado wanaendelea na sinema za kuwahadaa wananchi, CCM ebu waacheni wananchi wapumzike kidogo
Mafisi hayo
 
Mimi nipo tayari niwe rais kwa mshahara walaki 5 tuuuu!!!
 
Kusema mabaya au mapungufu ya mtu siyo kumchukia bali ni kumsahihisha ajirekebishe
Kuna kueleza mabaya ya mtu kwa msukumo wa kukosoa tu, lakini pia kuna msukumo wa chuki pia hufanya kumuelezea mtu kwa mabaya na dalili yake ni pale unajikuta unamzunguzia huyo mtu kwa yale mabaya tu yani huwezi kumuelezea huyo mtu kivyengine tofauti na mabaya yake.
 
*Anakula bure.
*Analala bure.
*Anaenda popote bure.
*Kila akitoka anapewa posho nono.
*Hadi bajeti ya suti zake analipiwa na serikali.
*Hata yeye anapiga madili yake, huenda ikafika 1.5tr.

Endelea kujilinganisha na raisi wa nchi.
 
*Anakula bure.
*Analala bure.
*Anaenda popote bure.
*Kila akitoka anapewa posho nono.
*Hadi bajeti ya suti zake analipiwa na serikali.
*Hata yeye anapiga madili yake, huenda ikafika 1.5tr.

Endelea kujilinganisha na raisi wa nchi.
Hahaha wewe unataka kukumbusha 1.5 tr za Mussa Assad
 
Back
Top Bottom