Huku ni kutishana na labda kujaribu kunyamazishana hasa kwa kuwa tunaeleelekea kipindi kigumu cha uchaguzi ambapo wasiojulikana hao hao anaowakingia kifua wanatarajiwa kuongeza speed kwa kuwapoteza watakaoonekana kuwa mlengo tofauti sisiem.
Uwezi kuwazuia watu ku-suspect (tuhumu) unless unajua ni kweli suspects ni wahusika na wewe ni miongoni mwao hao wanaokuwa suspected hivyo unalikingia kifua genge lako.
Nadhani hili jambo ilibidi liongelewe in a opposite way! Yeye kama raia namba moja ilitakiwa ku-side upande wa wananchi na kuwa uliza hao anao watetea wajipime kama awahusiki, ni kwa nini tuhuma zinaelekezwa kwao?
Pia kwa nini baadhi ya watu kama tito, erick, nk, waliodhaniwa kuwa wametekwa mwisho baada ya shinikizo la tuhuma hizo hizo anazozikataa wanapatika huko huko anakokutetea?
Kama mtu ana makosa, ya nini kumteka kwanza na magari ya yasiyoeleweka, baadae ndiyo uje kujitokeza kusema unaye sijui ana makosa moja mbili tatu. Huu ni uhuni na ndiyo utekaji wenyewe. Kama siyo watekaji kweli, ni kwa nini utaratibu wa kawaida wa polisi wa kuwakamata watuhumiwa wa makosa usitumike? Badala yake wanateka raia wema, kisha wanawafungulia kesi kubwa za uongo ambazo hata upelelezi wake tu ni shida.