Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Huku ni kutishana na labda kujaribu kunyamazishana hasa kwa kuwa tunaeleelekea kipindi kigumu cha uchaguzi ambapo wasiojulikana hao hao anaowakingia kifua wanatarajiwa kuongeza speed kwa kuwapoteza watakaoonekana kuwa mlengo tofauti sisiem.

Uwezi kuwazuia watu ku-suspect (tuhumu) unless unajua ni kweli suspects ni wahusika na wewe ni miongoni mwao hao wanaokuwa suspected hivyo unalikingia kifua genge lako.

Nadhani hili jambo ilibidi liongelewe in a opposite way! Yeye kama raia namba moja ilitakiwa ku-side upande wa wananchi na kuwa uliza hao anao watetea wajipime kama awahusiki, ni kwa nini tuhuma zinaelekezwa kwao?

Pia kwa nini baadhi ya watu kama tito, erick, nk, waliodhaniwa kuwa wametekwa mwisho baada ya shinikizo la tuhuma hizo hizo anazozikataa wanapatika huko huko anakokutetea?

Kama mtu ana makosa, ya nini kumteka kwanza na magari ya yasiyoeleweka, baadae ndiyo uje kujitokeza kusema unaye sijui ana makosa moja mbili tatu. Huu ni uhuni na ndiyo utekaji wenyewe. Kama siyo watekaji kweli, ni kwa nini utaratibu wa kawaida wa polisi wa kuwakamata watuhumiwa wa makosa usitumike? Badala yake wanateka raia wema, kisha wanawafungulia kesi kubwa za uongo ambazo hata upelelezi wake tu ni shida.
 
Ni sawa kabisa,tena itungwe sheria Kali dhidi ya vyombo vya habari vinavyohusika kutoa taarifa za uzushi kama hizi ili Iwe mwisho wa upuuzi huu,mtu amekamatwa let's say na polisi mijitu inasema ametekwa,mtu yuko offline kwa matatizo ya mtandao wanadai ametekwa,hatuwezi kufika kwa kuendekeza upuuzi kama huu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hofu ya kutekwa imeletwa na matukio halisi ya watu kutekwa na wahusika wa utekaji bado hawajakamatwa. Hivyo basi ni jukumu la Serikali kuwaondolea watu hofu ya ketekana tekekana kwa kuwabaini watekaji. Badala ya kuwanyamazisha wenye hofu kwa mkono wa chuma.​
 
Huyu mpuuzi ameshalewa madaraka, sasa anatuona Watanzania wote kama watoto wake tu. Hii ni kawaida kwa Watawala wote wanaotumia MKONO WA CHUMA kuongoza Serikali zao.
 
Baada ya kuona misaada hailetwi tena na uchumi ķuyumba.
Na uchaguzi unakaribia lazma ajisafishe
Not every lost is kidnapped by national security, some have gone to their lovers ( 640 X 640 ).jpg
 
Lakini Rais ajue watanzania si wajinga! Kuna siku nayeye atatoa ushahidi!
 
Kwa Nini matukio ya utekaji yameshamiri awamu hii ambayo anaiongoza?
 
Pengine tungejiuliza kwa nini watu aina fulani wanatekwa, nani anawateka, na tutazuiaje utekaji na ni nani hasa mwenye jukumu hilo?

Kwa nini wawe ni wale waopinga jambo ndani ya utawala au wale walioandika jambo linaloudhi au wana msmamo unaoeleweka dhidi ya kiongozi fulani.

Kwa nn wengi wana characteristics zinazofanana?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Washangilie na kusifia kila kitu hata kutekwa kwao wenyewe.
Hofu ya kutekwa imeletwa na matukio halisi ya watu kutekwa na wahusika wa utekaji bado hawajakamatwa. Hivyo basi ni jukumu la Serikali kuwaondolea watu hofu ya ketekana tekekana kwa kuwabaini watekaji. Badala ya kuwanyamazisha wenye hofu kwa mkono wa chuma.​

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Rais hafikirii sawa sawa kwakweli. Kwa hiyo kwa akili yake ni kuwa Azory na Ben wako kwa wapenzi wao?
 
Kwa Nini matukio ya utekaji yameshamiri awamu hii ambayo anaiongoza?
Ndo maana katuchimba Mikwara tusitangaziane kutekwa ili matukio ya utekaji yapungue kwenye Media, ili utekaji na watekaji wasijulikane.
 
Return Of Undertaker,
Vyombo vya usalama basi viseme ni nani ambaye anateka watu na silaha. Na ni kwanini hawa watekaji wameanza muhula huu wa uongozi? Na nia yao hasa ni nini ya kuteka?
 
Kupitia onyo hilo watu wanaandaliwa kisaikolojia tuelekeapo uchaguzi wa mwaka huu. Inaonyesha kuna maandalizi makubwa na ya kutosha kuhusu watu kutekwa, kuteswa na kupotezwa, hasa upande wa Zanzibar na hii ni jitihada ya wazi kabisa ya kufanya "preemption" ili watu waogope kuhoji. Katika masuala ya uchaguzi, CCM ya awamu hii wapo tayari kufanya upuuzi wowote ule, pasipo kujali madhara yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatukana ukiwa umejificha nyuma ya keyboard! Angalie usije ukapotea halafu uanze kusingizia kuwa ni TISS kumbe ni sisi wanaume wa shoka tulioapa kumlinda Rais wetu kipenzi
Acha ukweli usemwe. Ujinga uitwe ujinga bila kujali nani katenda ujinga huo. Kama umeapa kulinda ujinga wa mtu basi wewe ndiyo mjinga uliyepitiliza.
 
Back
Top Bottom