Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Tukiondoa ya Asadi, Taja mengine ambayo mwishoe hapatikani kwenye city of bus polisi bila maelezo.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watekaji na Watesaji Raia ni Serikali ya CCM na vyombo vyake vya usalama, ndugu Magufuli hawezi kujitenganisha na hili. Ajikite kwenye KUSITISHA na kukomesha hivyo vitendo badala ya KUTISHA watu.
 
Mdude chadema alitekwa na nani tena mchana kweupe?? Majambazi? Wako wapi walikamatwa?? Mnataka kuwafanya watanzania wajinga? Its too late mr president.
 
Kisicho julikana ni kwamba baada ya sera zote kupokwa wenzenu wamepata pa kushika ni hatari kunyang'anya hata hii kwani wasipo tafuta huruma ya wananchi kupitia utekaji watakuwa hawana ajenda mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wa kupokonya ajenda ni yupi? Mngekuwa mmepokonya ajenda mngeshangilia kushinda kwa kunajisi uchaguzi ili mpite bila kupingwa?
 
Ukiwa jambazi, hukomi kuwa jambazi, kwa sababu kuna mtu amesema usiitwe jambazi, bali kwa kuacha ujambazi.

Siku hizi mtaani TISS wanaitwa watu wasiojulikana. Hili sasa ni jina common la TISS. Na wao wanalijua na kimazoea, ni kama wamelikubali hili jina. Siyo jina baya kwa nature ya kazi yao.

Ubaya ni Polisi wanaposema kuna mtu ametekwa au ameshambuliwa na watu wasiojulikana!
 
Well
 
Katika hili namuunga mkono Mh.Rais wa JMT Dr.John Pombe Magufuri. Binafsi nilikutana na taarifa kama hii maeneo ya Mahina jijini Mwanza ambapo bwana mmoja kwa jina kapuni aliyetoweka nyumbani kwake usiku kwa kumuaga mkewe kuwa anaenda kununua vocha usiku wa saa tano baada ya kutoka safari.

Mkewe alimsubili pasipo kuona dalili ya kurejea nyumbani,siku ya pili alianza kumtafuta kwa kuuliza ndugu,jamaa na marafiki ambao walimshauri atoe taarifa ofisi ya serikali ya mtaa kwa ushauri na maelekezo mengine. Cha kushangaza siku iliyofuata iligundulika kuwa jamaa siku aliyoondoka kutafuta vocha alikwenda kwa kimada wake na kufungiwa ndani kwa mahaba motomoto.
 
Alijuaje kama ni kikosi kazi?
Kama sio kikosi kazi alitekwa saa moja jioni watu kibao, mita 30 mbele kulikiwa na askari benk, taarifa zilitolewa polisi muda huo huo lakini mpaka leo hakuna hatua yoyote ilichukuliwa na RPC kushughulikia sakata la Mdude Nyangali.

Utaachaje kuamini kama sio vyombo vya usalama?
 
una ushahidi kuwa Usalama wa taifa ndio wanahusika na utekaji? haya ndio Mh. Rais amesisitiza watu kama ninyi mchukuliwe hatua..

Hakika mnaudhi sana..

Jitahidi kuvumilia ukweli, rais sio mkweli, anachojivunia ni madaraka yake. Hana uhalali wowote wa kuzuia watu kuongelea usalama wao, kwani huu utekaji unafanyika chini ya utawala wake, huku yeye akifumbia macho hali hiyo.
 
Return Of Undertaker,
achaneni na huyu ngosha.

alijifanya kukataza "sitaki kusikia mtu yoyote anasema vyuma vimekaza" Watu pamoja na mapolisi wake wenyewe wanaendelea kupiga kelele hadharani tena kwa nguvu kabisa "vyuma vimekaza"
 
Rai amejiabisha sana leo, amiri jeshi mkuu anataka kukamata wanaopiga kelele huku ameshindwa kuwakamata wahalifu wanaoteka na kuua, hilo jukum anamwachia nani
Naam, ndugu now i can confidently say Magufuli haelewi ukubwa na upana wa dhamana aliyo ibeba, na kwa mantiki hiyo kiti hicho kina mpwaya tena sanaaaaa!!!!!!!
 
So hata akina Azory,Ben saanane wako kwa kimada?
Zakaria asingefungulia bomba la risasi basi tungeambiwa yuko kwa kimada!
 
Naam, ndugu now i can confidently say Magufuli haelewi ukubwa na upana wa dhamana aliyo ibeba, na kwa mantiki hiyo kiti hicho kina mpwaya tena sanaaaaa!!!!!!!
Yaani utafikiri sio Rais wa nchi, anabwabwaja tu!
Hivi ni mtu gani amewahi tekwa kwenye awamu yake na watekaji wakapatikana?
 
Umemaliza mkuu!Jamaa ana roho ya ajabu sana!
 
Hivi wale waliotandikwaga risasi na yule rais wa Tarime walikuwa wanafanya kazi ofisi gani na bado bila aibu mmeendelea kumshikilia mzee wa watu kwa kesi ya siraha ambayo mmemnyanganya documents za umiliki
 
Aongee kama msomi, yeye kama rais amewahi kutoa tamko gani juu ya wanasiasa, waandishi wa habari na raia wema wanaoripotiwa kutekwa na wengine kujeruhiwa?.

Asitugeuze mapimbi, serikali inahusika na matukio tata ya utekaji, ndio maana watekaji hawajawahi kukamatwa.
 
So hata akina Azory,Ben saanane wako kwa kimada?
Zakaria asingefungulia bomba la risasi basi tungeambiwa yuko kwa kimada!
Nimewapa kisa chenye mfano,hao wengine unaowasemea hakuna ajuaye yaliyowakuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…