Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Rais Magufuli: Mtu akipotea, marufuku kuhusisha vyombo vya Dola, utakamatwa na utoe ushahidi

Kama wanajiteka wenyewe na kujirudisha sasa yeye atajuaje? Na hao waliotekwa kwa nni wasifungue kesi kuhusu hao watekaji na kuwasema hadhalani ili wakate mzizi wa fitina? Maana wakitajwa mara mbili wataacha, hii mi naona ni mipango ya wao wenyewe kujiteka kisha wanarudi na hawasemi walipokuwa ili wasingizie serikari.

..Mwanaharakati Mdude Nyagali amefungua kesi dhidi ya maofisa wa polisi waliomteka na kumtesa.

..Mdude ameweza kuwatambua maofisa hao kwa majina na force number zao.

..Pia alipeleka malalamiko yake Tume ya haki za binaadamu, lakini tume hiyo imekuwa ikikwepa kufanyia kazi malalamiko ya Mdude.
 
Sahihi kwenye lipi, hivi kama hao aliwasema hawahusiki kwa nini hawakanushi,na pia wananchi wamempa nchi ili awahahakikushie ulinzi na usalama wao badala awahakikishie ulinzi anaongea vitu vya ajabu,yaani Africa ni shida Rais badala awadhibitishie usalama kwa waliompa cheo anawatisha sasa.
Mheshimiwa Rais yupo sahihi naunga mkono

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aseme alipo Ben Saanane
Then kwa kuwa watanzania siyo wajinga,anatakiwa pia atuambie kama Mo alitekwa au alikuwa kwa mchepuko wake?na kama alitekwa hao wengine hao wengine inashindikana nini kutekwa?
 
Mh Rais anahitaji semina ya kujua URAIS wa katiba yetu sio UFALME na HAVIKARIBIANI,Anapiga marufuku yeye kama nani? Jeshi halihitaji kushauriwa lifanyaje kazi ,na mtu kushhikiliwa sio kwa maagizo ya rais bali taratibu ambazo zipo toka 1977 za namna ya kushuhurikia uhalifu
 
Return Of Undertaker,

Mheshimiwa kuwatishia watu sio uongozi baba! Unatakiwa ujiulize ni kwa nini vyombo vya usalama vinahusishwa na sio majambazi?! We ni mtu mzima una akili ila unajisahau kuwa umebeba dhamana ya watanzania!! Mbona unaonekana kama unakereka sana pale watu wanapopatikana baada ya kutekwa?! Umedhamiria kuuwa watu au kuwaongoza?!
 
Nina wasi wasi na dhamira ya Rais Magufuli kwa raia wa Tanzania. Kuna watu wengi wametekwa katika utawala wake lakini ni nani aliyewahi kubainika alikuwa kwa hawara yake? Au anataka kusema hakuna utekaji ya kweli bali watu wanazua hofu na kuvichafua "vyombo"? Kama vyombo vya dola havihusiki ni nani anahusika? Na kwa nini hakuna aliyehi kubainika kuwa ndiye mtekani?

Hi kuna sheria yoyote inakataza kutuhumu bila kuwa na ushahidi? Au ni yeye tu na vyombo vyake havipaswi kutuhumiwa bali wao ndo watuhumu? Kama ni hivyo ile dhana ya sheria ni msumeno inazingatiwa? Lakini kwanini "akamatwe" kwa ajili ya kutoa ushahidi/uthibitisho wa tuhuma?
 
Huyu anajihami tu baada ya yule mangi kule himo kuwachezesha polisi waliomteka na kudai rushwa ya milioni 30! Nakuuliza, hao polisi si ndio walinzi wa Mali na watu?

Haoni Kama vyombo vya dola vimeacha kutimiza majukumu yao ya kisheria na kugeuka magenge ya utekaji? Alitakiwa avikemee kwanza na kwa nguvu badala ya kuwatosha raia! Kwa maana hiyo yeye kavihalalisha vyombo vya dola kuendekeza kuteka.

Apekeke mswada bungeni ili kipengele Cha utekaji kihalalishwe kiwe Sheria na moja ya majukumu ya vyombo vya dola! Uchaguzi ujao unamnyima usingizi hivyo raia wajiandae kutekwa!
 
Vip kuhusu eric kabendera mwanzo alipopotea tuliambiwa ni watu wasiojulikana in few days tukaambiwa ni yupo mikonon mwa polisi then ndo kusomewa kesi kibao sijui ni za kweli au kubambikiwa mpka saiv anasota, hivyo hivyo Tito amepotea na wasiojulikana badae inaonekan kumbe ni serikali.

Wananchi lazima wahusishe vyombo vya usalama kwa sabab kuu zifuatazo
1. Baadhi ya waliopotea wakajulikana walipo ilionekan ni vyombo vya usalama km polisi ndo wanawashikilia

2. Baadhi ya waliopotea wakapatikan km roma walishindwa kusema nan amewafanyia hivyo. Na polisi hawakujishugulisha kumsaidia kumpata alie fanya hivyo. Mmoja alisema roma atapatikana kbla ya j2 na ikawa hivyo.

3. Baadhi ya waliopotea moja kwa moja km ben saanane na azory. Hakuna jitihada za uchunguz zinafnywa na juu ya matukio hayo na viongozi wenyew wanatoa majib yenye utata.

4. Asili ya watu wanaopotea ni wale wenye mlengo wa kushoto ie. Wenye mawazo mbadala/tofauti na mtazamo waserikali

5. Matukio km la kupgwa mtu risasi hadharani mchana ni matukio makubwa na hatar sana ndan ya nchi lakin vyombo vya usalama vimekua vinatoa majib mepesi juu ya uchunguz wake zaid sana serikal imeonyesha chuki za wazi juu ya muhanga wa tukio hilo. Kuanzia kwenye kumnyima matibab kwa visingizio vya kitoto mpka kumnyanganya nafasi yake aliyopewa na wananchi kish kupewa nafasi hyo mtu wanaemtaka wao.

Hii imejengea jamii dhana ya kua mtu yeyote asipoonekana katka mazingira km hayo mwenye mtazamo uliojionesha kua upotofaut na watawala mfano CAG, bas vyombo vya ulinz na usalama km TISS vinahusika moja kwa moja.

Lakin pia tunajiuliza kwa nin haya matukio yameshamili sasa hivi!?? kwa nin yasikike zaid awamu hii na sio zilizopita!??? Rais asiilaum jamii kwa makosa yake yeye mwenyew.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh ajiulize kwanini mtu akipotea mazingira ya kutatanisha wa kwanza kuhisiwa ni vyombo vya usalama? kwnn raia wasi suspect watu wengine? haoni kma kuna kitu hapo? Mfano mtaani ukitokea wizi hua raia hua wanajua wapi pa kuanzia sababu tuna fahamiana tabia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Digba Sowey usiwe mbulula wa Lumumba, Azory haonekani, Ben Saanane Haonekani, Lissu kamwagiwa risasi watu wasiulize??
Unaishi Congo au mwezini??
Ni wajibu wa vyombo vya ulinzi na usalama kutoa majibu!!
Wanalipwakodi zetu na sisi sio watumwa tunahitaji haki sio vitisho.
Huu sio ufalme ni serikali iyochaguliwa na watu waheshimiwe maana sio manamba!!
Akipotea mjomba wako utasemaje??
 
Back
Top Bottom