Rais Magufuli mtumbue Bosi wa TTCL anaihujumu kampuni

Rais Magufuli mtumbue Bosi wa TTCL anaihujumu kampuni

Gawio ni jambo la kumpongeza mkuu, zaidi ya miaka 17 TTCL haikuwai kutoa gawio lakini kupitia DG Kindamba TTCL imefanikiwa kutoa gawio. kwa kweli ni jambo la kumsifia
Mkuu, wanatoaje gawio wakati wana matatizo lukuki?

Haingii akilimi kutoa gawio la billion 2 halafu kuomba trillion moja kuboresha shirika. Kuna kitu japo kidogo wangeweza kuanza kufanya na billion 2
 
Nunua kwa TPESA, yaani weka hela kwenye mpesa yako kisha itume kwenye ttcl then nunua bando juu kwa juu. Vocha ndo tatizo lao kubwa ni vyema this time wasitoe gawio kwa rais, hilo gawio watengeneze vocha wazisambaze nchi nzima.
Huu ndio Upumbavu walionishauri...... Nataka kuweka 1000... Naenda MPesa kuwaomba waniwekee Buku, buku nahamishia TTCL inakuwa tena ni Buku???

Kampuni zote wana Vocha kasoro TTCL pekee ndio hawana Vocha........

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shalom,

Niende moja kwa moja kwenye mada. Mh Rais tunaomba umtumbue boss wa TTCL haiwezekani tangu apewe uongozi mwaka 2016 mpaka leo kampuni ipo ovyo.
Kampuni haijiongezi na pia huyo boss sio mbunifu kabisa.
Yaani 52% wa watumiaji wa TTCL hawajui menyu ya kuangalia salio ipoje.
Kampuni haina ofa kwa wateja wake utadhani inauza nyanya.
Watoa huduma wa Costumer Care ndiyo ovyo baba, ukimpigia simu anakujibu oke, sawa, yes mpaka sometimea nafikiria kuwatongoz baba.

Huduma mbovu haziridhishi kabisa. Mtu yupo tu ofisini anapunga upepo hana hata hadhi ya kuongoza kampuni kama hiyo.

Tafadhali tunaomba umpe uongozi mtu mwingine mwenye huruma na Watanzania.

Mbaya zaidi mtu mwenyewe anamiliki hisa zake huko kwenye kamouni ya SMILE. TTCL ipo tangu 1993 hadi leo huduma ovyo.

Halotel wamekuja juzi tu hapa lakini wamekiwasha balaa mpaka wanyonge tunakimbilia kule.

Waziri Kindamba OUT
Unaiharibu TTCL yetu.
Yaani watoa huduma baada ya kutufuata sisi wao ndio wanataka sisi tuwafuate.

Asanteni
Hili neno OUT limenikumbusha siku mzee Mapesa alipokuwa anawafukuza wanachama waliojaribu kufanya hujuma za kutaka kumpindua uenyekiti wa chama cha UDP Mapendo. Siku hiyo mzee Mapesa alikuwa anawafukuza wanachmaa kwa staili ya kusoma jina, halafu anasema OUT, yaani kwa mfano MAKANYAGA, OUT; KIBWETERE OUT,....Yaani ilikuwa burudani siku hiyo nilicheka mpaka karibia kuzimia!
 
Shalom,

Niende moja kwa moja kwenye mada. Mh Rais tunaomba umtumbue boss wa TTCL haiwezekani tangu apewe uongozi mwaka 2016 mpaka leo kampuni ipo ovyo.
Kampuni haijiongezi na pia huyo boss sio mbunifu kabisa.
Yaani 52% wa watumiaji wa TTCL hawajui menyu ya kuangalia salio ipoje.
Kampuni haina ofa kwa wateja wake utadhani inauza nyanya.
Watoa huduma wa Costumer Care ndiyo ovyo baba, ukimpigia simu anakujibu oke, sawa, yes mpaka sometimea nafikiria kuwatongoz baba.

Huduma mbovu haziridhishi kabisa. Mtu yupo tu ofisini anapunga upepo hana hata hadhi ya kuongoza kampuni kama hiyo.

Tafadhali tunaomba umpe uongozi mtu mwingine mwenye huruma na Watanzania.

Mbaya zaidi mtu mwenyewe anamiliki hisa zake huko kwenye kamouni ya SMILE. TTCL ipo tangu 1993 hadi leo huduma ovyo.

Halotel wamekuja juzi tu hapa lakini wamekiwasha balaa mpaka wanyonge tunakimbilia kule.

Waziri Kindamba OUT
Unaiharibu TTCL yetu.
Yaani watoa huduma baada ya kutufuata sisi wao ndio wanataka sisi tuwafuate.

Asanteni
Anaondolewa ukakae wewe
 
Yaani 52% wa watumiaji wa TTCL hawajui menyu ya kuangalia salio ipoje.

Hii wangefanya iwe standard kwa makampuni yote kama ilivyokuweka salio *104*...

Kuangalia salio TTCL ni mlolongo mrefu sana unachosha maswali kibao!!
 
Ainisha ubovu wa huduma za TTCL.Tuanzia hapo kamanda!

Mojawapo ni ugumu katika upatikanaji wa huduma za vocha, vifurushi na mabando kwa mawakala mahali popote.

Havipatikani .

Yani eti inabidi ununue huduma ya M- pesa , au Tigo pesa au airtel kisha ndiyo ubadilishe kwenye T-Pesa ndiyo upate huduma ya TTCL.

Sasa kwa kufanya hivyo kunaongeza gharama za manunuzi na za kutokea.

Hapo ipo tatizo kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ndio Upumbavu walionishauri...... Nataka kuweka 1000... Naenda MPesa kuwaomba waniwekee Buku, buku nahamishia TTCL inakuwa tena ni Buku???

Kampuni zote wana Vocha kasoro TTCL pekee ndio hawana Vocha........

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu next time weka hela kwenye T.PESA kisha nunua muda wa maongezi. Njia rahisi sana au
kama una account number NMB or CRDB unaweza nunua.
 
Yani hawajaweza kuwa na mkakati wa market penetration hata kidogo.

Huduma zao hazipatikani kwa wepesi Yani conveniently.

Kila kwa wakala unaeenda ukimwambia nataka huduma ya T-pesa , au vocha za TTCL anakwambia sina.

Sasa mteja hapo utahisikiaje kwa mfano?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi sina nia ya kumshambulia mtu, ila kuna siku nilikuwa na mtumishi mmoja wa TTCL ambaye awali alikuwa sekta binafsi, baadae akaamua kuja mashirika ya serikalini, alilalamika sana kwamba yaani huku mtu unaweza ukakaa siku 3 hakuna ulichofanya na wala mtu hajisikii vibaya (alitumia neno '' watu sio aggressive kabisa kibiashara). lakini mimi mwenyewe naweza kuawa uliza watumishi wa TTCL ,swali dogo, mteja akipiga simu ya kuhitaji msaada mnchukua muda gani kumjibu/ kupokea simu, utafiti wangu umeonyesha ni kuanzia dakika 8, ximu inaita tu !

suala la pili mnajua vocha zenu hazipatikani kirahisi , kwanini hamuweki matangazo kwenye TV kuonyesha kwamba mtu anaweza kununua kwa salio lililomo kwenye simu yake au akahamisha fedha toka laini nyingine kisha akabadilil kuwa muda wa maongezi ?

vifurushi vyenu ni vya bei rahisi sana lakini watu hawajui , jitangzeni

mwisho , mimi nawapongeza hata hapo mlipofika ila muwe AGGRESSIVE, pia mnapokwama iambieni serikali kwamba pengine speed ya data zetu iko chini, tunatakiwa tununue mtambbo fulani unauzwa shililingi bilioni 1.5, mkitununulia huo, aah, yaani tutakuwa vizuri , vitu kama hivyo !
 
Mkuu, wanatoaje gawio wakati wana matatizo lukuki?

Haingii akilimi kutoa gawio la billion 2 halafu kuomba trillion moja kuboresha shirika. Kuna kitu japo kidogo wangeweza kuanza kufanya na billion 2

Kumpa shareholder gawio lake at the same time unamuomba awekeze ni vibaya???
 
Mojawapo ni ugumu katika upatikanaji wa huduma za vocha, vifurushi na mabando kwa mawakala mahali popote.

Havipatikani .

Yani eti inabidi ununue huduma ya M- pesa , au Tigo pesa au airtel kisha ndiyo ubadilishe kwenye T-Pesa ndiyo upate huduma ya TTCL.

Sasa kwa kufanya hivyo kunaongeza gharama za manunuzi na za kutokea.

Hapo ipo tatizo kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye soko la telecom ni muhimu kuwa na njia mbalimbali za kusambaza muda vocha sokoni, hiyo inampa mteja mutple selection. Hakikikosa vocha ya kukwangua, anaweza nunua kupitia T,PESA au Banks au Selcom etc. Kwa ushindani uliopo sokoni huwezi ku-rely njia moja tu
 
Mbona TTCL iko poa zaidi ya makampuni mengi tu.. watu muache chuki binafsi.. watu tunakuka bando za maana , hawatafuni MB kwa kasi kama voda wanatoa dk za kutosha... speed inaridhisha.. mambo ya gawio na faida mimi hayanihusu as long as nakula bando kubwa na speed ya uhakika
 
Kumpa shareholder gawio lake at the same time unamuomba awekeze ni vibaya???
Shareholder anapewa gawio kama kuna faida.
Tatizo gawio la Bongo ni lakisiasa si kibiashara. Ndiyo ya Chuo Kikuu cha umma kutoa gawio. Kwa biashara ipi ya faida?
 
Mojawapo ni ugumu katika upatikanaji wa huduma za vocha, vifurushi na mabando kwa mawakala mahali popote.

Havipatikani .

Yani eti inabidi ununue huduma ya M- pesa , au Tigo pesa au airtel kisha ndiyo ubadilishe kwenye T-Pesa ndiyo upate huduma ya TTCL.

Sasa kwa kufanya hivyo kunaongeza gharama za manunuzi na za kutokea.

Hapo ipo tatizo kubwa sana

Sent using Jamii Forums mobile app
TTCL wana huduma nafuu ya internet hususani kwa laini ya chuo.Hakuna gharama ya kununua vifurushi vya TTCL kwa kupitia Tigo pesa
 
Hii wangefanya iwe standard kwa makampuni yote kama ilivyokuweka salio *104*...

Kuangalia salio TTCL ni mlolongo mrefu sana unachosha maswali kibao!!
Mimi ni mteja wa TTCL kwa miaka mingi, ninatumia simu ya mezani, natumia MI-FI na mobile
kuangalia salio kwa mobile iko standard kwa wote piga *102# kuona salio lako au kwa upande wa vifurushi piga *148*30# select number 9
 
Shareholder anapewa gawio kama kuna faida.
Tatizo gawio la Bongo ni lakisiasa si kibiashara. Ndiyo ya Chuo Kikuu cha umma kutoa gawio. Kwa biashara ipi ya faida?

Mkuu naona umenisoma vizuri, shareholder kupewa gawio lake ni kitu muhimu sana kibiashara na kujenga mahusiano mazuri na shareholders . mm naona mpaka TTCL wanatoa gawio ina maana walipata faida. let's support TTCL hii ni yetu
 
Namba hazidanganyi,

Kindamba kaikuta TTCL mahututi mbapaka sasa inatoa gawio serikalini. Tatizo kuu lilikua ni mtaji na hakupewa,anafanya maboresho kutokana na mtaji mdogo uliopo,hata awekwe mwingine hataweza kufanya zaidi ya huyu Kindamba.

Mungu Jehovah akusaidie kama kweli unaamini TTCL walitoa gawio.
 
Back
Top Bottom