Uchaguzi 2020 Rais Magufuli muombe Rais Mstaafu Kikwete akusaidie kupiga kampeni

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli muombe Rais Mstaafu Kikwete akusaidie kupiga kampeni

Mikakati ya ccm ipo kwenye nguvu ya rais ambaye anaweza kuagiza tume ya uchaguzi imtangaze mgombea yoyote wa ccm. Toka lini mbeleko ikawa mikakati?
Hii ni dalili ya kushindwa. Yaani ni sawa na mpira haujaanza uwanjani, mnaanza kumlalamikia refa atapendelea. Sasa kama mnaona refa atapendelea wekeni mpira kwapani tuokoe kodi za watanzania.
 
Magufuri hata asipopiga kampeni atashinda tu... Hamna mtu anayeweza kuwapa chadema nchi. Mbona haitaji hata elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo. Watu wengine vichwa vyenu vina nini? Mbona hamuelewi?
Acha zako wewe. Jiwe kapiga campain kwa miaka mitano peke yake baada ya kuwafungia wengine na bado leo hii anahaha! Hakutegemea haya yanayoendelea hivi sasa. Na anaweza kudondoka jukwaani wakati wowote kwa hofu.
 
Hata ukipewa wewe ukampigie Kampeni Magufuli na Yeye apumzike, bado atashinda tu!!
Kwamba anapendwa Sana au ana lipi jipya zaidi ya maneno ya shobo? Walinena zamani kuwa aliyesimama aangalie asije anguka! Hilo una habari nalo?
 
Hii ni dalili ya kushindwa. Yaani ni sawa na mpira haujaanza uwanjani, mnaanza kumlalamikia refa atapendelea. Sasa kama mnaona refa atapendelea wekeni mpira kwapani tuokoe kodi za watanzania.

Tofautisha kulalamika na kuongea ukweli
 
CCM ni chama cha mikakati. Hawa wastaafu inajua itawatumia wapi na wakati gani? Subiri kampeni bado hazijaisha ndo kwanza kumekucha asubuhi. Wapinzani wao haijulikani kama hata kampeni zao watazimaliza kabla pumzi haijakata.
Wananchi wapo kwenye mikutano ya kampeni za ccm mifukoni hawana hata Senti tano. Mnasema JK aende akawaambie nini watanzania? Hali ya kimaisha kuwa watanzania ni mbaya Sana Sana. Maendeleo anayoongelea hakuna anaye tapinga tatizo ni maisha yamekuwa magumu kuliko serikali zote zilizowahi kupita.
 
Magufuri hata asipopiga kampeni atashinda tu... Hamna mtu anayeweza kuwapa chadema nchi. Mbona haitaji hata elimu ya chuo kikuu kuelewa hilo. Watu wengine vichwa vyenu vina nini? Mbona hamuelewi?
Toa sababu zenye ushawishi wa kwanini CHADEMA isipewe nchi! Jambo gani linainyima CHADEMA sifa za kuongoza nchi? Au nawe no Kati ya wale wanaoamini kuwa CCM Ina hati miliki ya kuongoza nchi hii Kama biashara au kampuni yao?
 
Back
Top Bottom