Ndugu zangu tangu baada ya uchaguzi nchi yetu inapitia kipindi kigumu watu wanauawa kinyama mchana kweupe kwa sababu za kisiasa , kuchomeana makazi na kutekana.
Kibaya zaidi wenye mamlaka wanadai hali ni shwari kabisa labda kwa sababu wanalindwa kwa mizinga na rada ndiyo maana hawaogopi kinachoendelea nchini.
Leo Rorya mdogo wake Ezekia Wenje kauawa baada ya Wenje kukimbia kujificha, wauaji hawa wametamba kuiangamiza familia nzima ya Wenje na ndugu zake.
Tanzania ni moja, tunatoa roho za wenzetu kwa maslahi gani?
Ili CCM ibakie madarakani?
Au CHADEMA iiingie madarakani?
Mtawala hutawala watu, kiongozi huongoza watu, Leo watu mnawaua mtawatawala akina nani?
Watu mnawaua mtawaongoza akina nani?