Rais Magufuli na kamari ya Machinga na Mamantilie kwa manufaa binafsi ya kisiasa

Rais Magufuli na kamari ya Machinga na Mamantilie kwa manufaa binafsi ya kisiasa

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,503
Reaction score
15,858
Huwezi liona hili kama huna upeo wa kuwaelewa wanasiasa.

Magufuli amesema Machinaga na Mamantilie wafanye biashara popote bila bughudha yoyote kinyume kabisa na sheria ya mipango miji na sheria ya kodi.

Mfano mzuri ni hapo kariakoo ampapo ni busness hub ya Tanzania na nchi jirani kujazwa machinga kiasi cha kudi-scarage biashara na wafanya biashara wakubwa eneo hilo. Juzi tena stendi ya mabasi ya mikoani na nchi jirani ya Mbezi imegeuzwa gulio kwa sababu za kisiasa.

Nachokiona hapa kuna movement yenye malengo maalumu inaandaliwa kwa ajiri ya mwelekeo mpya wa siasa za nchi yetu. Kundi hili la vijana lililonyimwa ajira rasmi na mamlaka kisha kuelekezwa kufanya uchuuzi usioweza kuwapatia hata pesa ya kulipia bima ya afya ni hatari kwa usalama wa taifa.

Kesho vijana hawa wakitakiwa kuondoka maeneo hayo ni nani ataituliza hasira yao?

Huendi hili lipo nyuma ya ajenda ya kumuongezea muda Mh Rais kupitia maandamano ya makundi Haya baada ya kuona hoja hiyo hiwezi kuanzia bungeni Bali ianzie kwa civilians.

Mzee Mwanakijiji
 
Mimi kwa hili naona muheshimiwa Raisi yuko sahihi kabisa. Nini chema kwako kuwa na standi maridadi isiyo na watu wakati watu wako wanakufa njaa au kuwa na standi iliyojengwa kwa kodi za watu wako itakayotumiwa na watu wako kujitafutia ridhiki?

Mambo mengine ni kupima manufaa mapana ya taifa na watu wake. Nasimama na muheshimiwa Raisi, raia watanzania wafanye biashara sehemu yoyote isipokua ndani ya nyumba za ibada.
 
Mimi kwa hili naona muheshimiwa Raisi yuko sahihi kabisa. Nini chema kwako kuwa na standi maridadi isiyo na watu wakati watu wako wanakufa njaa au kuwa na standi iliyojengwa kwa kodi za watu wako itakayotumiwa na watu wako kujitafutia ridhiki? Mambo mengine ni kupima manufaa mapana ya taifa na watu wake. Nasimama na muheshimiwa Raisi, raia watanzania wafanye biashara sehemu yoyote isipokua ndani ya nyumba za ibada.
Nini maana ya kuwa na sheria ya mipango miji? Shule mlienda kusomea ujinga.
 
Anachomaanisha mtoa mada kuwe na utaratibu mzuri sio kama ilivyo hivi sasa, mfano pale mbagala biashara vibanda vipo mpaka katikati ya barabara ya wendo kasi na pembezo mwa barabara kiasi cha kwamba njia ya watembea kwa miguu imekua finyu na barabara imekua finyu foleni haishi kwa upangaji holela holea, uchafu ndo usiseme umekithiri kila eneo hata hiyo thamani ya hiyo miradi inafunikwa kwa huu ukiritimba. Mimi mwenyewe mjasiria mali ila inahitajika mikakati na sera nzuri kwa hili kundi sio kama ilivyo sasa.

Mimi kwa hili naona muheshimiwa Raisi yuko sahihi kabisa. Nini chema kwako kuwa na standi maridadi isiyo na watu wakati watu wako wanakufa njaa au kuwa na standi iliyojengwa kwa kodi za watu wako itakayotumiwa na watu wako kujitafutia ridhiki? Mambo mengine ni kupima manufaa mapana ya taifa na watu wake. Nasimama na muheshimiwa Raisi, raia watanzania wafanye biashara sehemu yoyote isipokua ndani ya nyumba za ibada.
 
Sheria za mipango miji siyo msahafu, inabadilishwa. Pia nyingi ni subsidiary legislations, hazijatungwa na bunge, hivyo zinaweza zikawa zimebadilishwa. Shule hatujaenda kukariri, tunatumia akili kupambana na mazingira yetu
Hayo mabadiliko ya sheria za mipango miji yalifanyika lini kuruhusu hu upuuzi wa kuruhusu machinga hadi katikati ya barabara huko kariakoo?
Halafu majitu yanakurupuka eti nchi hii inafuata utawala wa sheria
 
Nini maana ya kuwa na sheria ya mipango miji? Shule mlienda kusomea ujinga.
Mipango miji nenda Posta na Masaki huko.

Eti nyie ndo mlikuwa mnataka mpewe nchi muwatetee hao machinga na mamantilie.
Mara hii mshasahau kuwa kuna wakati Sugu alilazimika kutoka bungeni kwenda kuongea na machinga na mamantilie waliokuwa wanafukuzwa katikati ya jiji la Mbeya?

Kweli kuimba kupokezana.
 
Hayo mabadiliko ya sheria za mipango miji yalifanyika lini kuruhusu hu upuuzi wa kuruhusu machinga hadi katikati ya barabara huko kariakoo?
Halafu majitu yanakurupuka eti nchi hii inafuata utawala wa sheria
Kuna muda sheria huvunjwa kwa maslahi ya umma.
Hao machinga ndo waliotupa kura za kutosha.
Halafu jiulize,hao unaowaona huko kariakoo ulitaka tuwapeleke wapi wakafanye biashara zao?
Tunakoelekea tutajenga miji mingine hii iliyopo sasa ibaki kuwa masoko. Ikikukera....hama nchi.
 
Hayo mabadiliko ya sheria za mipango miji yalifanyika lini kuruhusu hu upuuzi wa kuruhusu machinga hadi katikati ya barabara huko kariakoo?
Halafu majitu yanakurupuka eti nchi hii inafuata utawala wa sheria
Mkuu machinga anaweza akawa mjomba wako, shangazi yako au kijana wako aliyekosa ajira kwenye mfumo rasmi. Hao wote ni watanzania na hii ni nchi yao. Wanayo haki, kama watanzania wengine, kusaka na kupata riziki yao kwa njia halali ikiwa ni pamoja na kufanya biashara sehemu yoyote ya ardhi ya Tanzania, na jambo hili lina akisi uhuru wao wa kweli na si vinginevyo.
 
Yaani awamu hii dar imekua takataka kabisa mabanda ya machinga kila sehem angalia kuanzia pale DIT hovyo kabisa mabanda ya mihogo watu wanapikia kuni city centre, mlimani city hata haionekani imezibwa na mabanda..afu na pale chini ya flyover walianza kujipanga bahati nzuri tu wamejenga uzio. Hatusemi wasifanye biashara bali watengewe maeneo.
 
Leo Mnaona Machinga hawana maana kwasababu tu walipuuz maandamano ya Sodoma wa Ubeljiji.

Nitafungulia Kampuni hapa Tulichoshwa sana na Askari wa Jiji enzi za Mkwere...
 
Halafu msisahau kuwa CCM ndiyo chama TAWALA kwasasa......mipango na mikakati hatakama ni ya kumuongeza muda Magu,ni mipango ya CCM. Kama nyie wengine mpo,ungeni tu mkono juhudi.
 
Yaani awamu hii dar imekua takataka kabisa mabanda ya machinga kila sehem angalia kuanzia pale DIT hovyo kabisa mabanda ya mihogo watu wanapikia kuni city centre, mlimani city hata haionekani imezibwa na mabanda..afu na pale chini ya flyover walianza kujipanga bahati nzuri tu wamejenga uzio. Hatusemi wasifanye biashara bali watengewe maeneo.
Watengewe wap? Nyie watu mna roho mbaya sana watengewe nje ya mji ili wafe njaa sio?
 
Watz kwa ku twist mambo! Mtu anazungumzia wawekewe utaratibu ninyi mnakuja na ngonjera za waachwe kwani wanatafuta riziki, kwani wakiwekewa utaratibu hawata tafuta riziki? Sidhani kama team magu wana akili timamu kichwani, mtu anasema hili wao wanasema lile.

Btw, hamjui tu wana siasa wanawatumia kiasi gani, hakuna future yoyote ya kijana wa kitanzania kuwa machinga au mamalishe kwenye vibanda vya barabarani. Serikali ingekuwa inawapenda ingewawekea utaratibu wa kukopa hata kwa vikundi ili mpate mitaji ya kufanya biashara "za kati za chini" ili muingie katika system za TRA za kulipa kodi.
 
Back
Top Bottom