Huwezi liona hili kama huna upeo wa kuwaelewa wanasiasa.
Magufuli amesema Machinaga na Mamantilie wafanye biashara popote bila bughudha yoyote kinyume kabisa na sheria ya mipango miji na sheria ya kodi.
Mfano mzuri ni hapo kariakoo ampapo ni busness hub ya Tanzania na nchi jirani kujazwa machinga kiasi cha kudi-scarage biashara na wafanya biashara wakubwa eneo hilo. Juzi tena stendi ya mabasi ya mikoani na nchi jirani ya Mbezi imegeuzwa gulio kwa sababu za kisiasa.
Nachokiona hapa kuna movement yenye malengo maalumu inaandaliwa kwa ajiri ya mwelekeo mpya wa siasa za nchi yetu. Kundi hili la vijana lililonyimwa ajira rasmi na mamlaka kisha kuelekezwa kufanya uchuuzi usioweza kuwapatia hata pesa ya kulipia bima ya afya ni hatari kwa usalama wa taifa.
Kesho vijana hawa wakitakiwa kuondoka maeneo hayo ni nani ataituliza hasira yao?
Huendi hili lipo nyuma ya ajenda ya kumuongezea muda Mh Rais kupitia maandamano ya makundi Haya baada ya kuona hoja hiyo hiwezi kuanzia bungeni Bali ianzie kwa civilians.
Mzee Mwanakijiji