Rais Magufuli na kamari ya Machinga na Mamantilie kwa manufaa binafsi ya kisiasa

Ni kukosa long term plans na kujitoa responsibility (ukikosa kazi, au ukilala njaa ujilaumu mwenyewe na sio waliowekwa pale waweke system rafiki)

Its an inevitable time bomb ila wanajua siku likilipuka huenda wasiwepo madarakani au duniani..., Create a Mess today so as someone else will take Care of it down the line....

Hizo ndio Politics za Survival (kufanya vitu rahisi rahisi vinayoonekana ili ukae kwenye power kwa miaka yako kadhaa) atakayekuja baadae atajijua yeye....

Ila mwisho wake ni gap ya walionacho na wasionacho kuongezeka maradufu, ambapo mwisho wa siku ni law of the jungle..., hata mwenye nacho hatakuwa hayupo salama
 
Naona umetoa jibu la kijinga kabisa,unadhani kwanini huyo rais umesimama naye lakini hajafuta sheria ya mipango miji na ile ya barabara? Labda unadhani huyo rais amekuwa anavunja sheria nyingi nyingi halafu arudi chato? Unadhani stendi imejengwa kwa mamilioni halafu huyo rais alikuwa hajui kuna machinga pale nje?
 
Watengewe wap? Nyie watu mna roho mbaya sana watengewe nje ya mji ili wafe njaa sio?
Kwanini watengwe ?, create favourable employment ili kuwapunguza..., wote tukiwa wachuuzi nane atanunua ? Mbaya zaidi wanachochuuza wengi ni ma-middle men hence wachuuzaji either kupata faida ndogo au mnunuzi kupata gharama kubwa
 
Watengewe wap? Nyie watu mna roho mbaya sana watengewe nje ya mji ili wafe njaa sio?
Manzese ni nje ya mji? Karume ni nje ya mji? Buguruni je? Huu ushamba wa kutotembea hata miji mingine ya africa tu unafanya tuwe wa ajabu sana...mnaishia kusifia tu kigali na nairobi msijue walichotuzidi ni hicho tu
 
Umepanick, Kama vipi waruhusuni Hadi Julius nyerere international airport
Huna akili wewe ni mpumbavu mnatumika vibaya na umaskini wako
 
Sina ndugu mmachinga Ila hao machinga njia wanazotumia kupata riziki sio halali kwa mujibu wa sheria zetu.
Sheria zetu za mipango miji haziruhusu mtu kufanya biashara katikati ya barabara
Ni huyu mpuudhi aliyeiba kura tu ndio anahalalisha huu ushenzi
 
Stendi ni mahali pa kufanya biashara za uchuuzi?

Serikali itafute njia mbadala ya kupambana na ajira, yanaweza hata yakajengwa masoko madogo madogo, very simple kwa ajili ya wachuuzi tu.

Mathalani kwa maeneo ya stendi, pembezoni mwa stendi kanajengwa kasoko kadogo, mabasi yakiwa yanaanza safari yanapita hapo kwa ajili ya wachuuzi kuuza vitu vyao.
 
Msingi wa hoja yako nzima umeuvunjia hapo mwisho, ulipoandika "isipokuwa ndani ya nyumba za ibada."

Hapa umetoa mwanya pawepo na sehemu nyingine kama hiyo ya "nyumba za ibada."

Ikulu waende? Vituo vya polisi nako waingie, magereza, vibarazani kwa nyumba za watu, n.k., n.k,.

Huu ni mpango mbovu, usiokuwa na uendelevu wowote.

Kufanya biashara, kama kazi nyingine yoyote inahitaji mpangilio maalum. Haiwezi kufanywa holelaholela tu.

Kwanza wanunuzi wenyewe ndio hatimae watakaolazimisha vurugu hizi zikome. Hata sasa, pita maeneo ya biashara za aina hii, utakuta mtu yupo siku nzima hapati mnunuzi hata mmoja. Hiyo ni biashara balaa!
 
Lakini wanachosahau hapa ni kuwa watu hawa hawa walikua wakitumika na vyama vya upinzani,

Mfano boda boda kuna wakati walikua wanakamatwa wakifika city center ila nyuzi hapa JF hazikukauka kuwatetea kwamba wanaonewa na hawana namna nyingine ya kupata kipato, ikawa hivyo kwa wanasiasa wa upinzani walipiga sana kelele kuhusiana na hao boda boda.

Ninachoona hapa ni kuwa kuna watu wanalilia kupoteza mtaji wao wa kisiasa, kwani kundi hili ndilo walikua wakilitumia kupenyezea agenda zao, sasa kundi limepata mwanga hakuna cha kuwaambia tena.

It is all about politics.

Wapinzani wanalia kupoteza kundi ambalo walikua wanalitumia kudanganya.
 
Asante mkuu. nakubaliana na wewe kwa mada yako kwa 90% isipokuwa kuhusu kujiongezwa msa wa kutawala kwa Rais. Hilo sikubaliani na wewe. Nina uhakika Rais Magufuli hata rudi tena baada ya miaka yake hii mitano. Hataki na hata taka tena.

Tukija kwenye swala la wamachinga na mamantilie hata mimi naona shida kubwa ipo. Kwa hili swala hata mimi maona matatizo makubwa huko mbele. Rais Magufuli ameshindwa kutumia hela za umma ambazo anazikusanya na kuzisimamia vizuri kuanzisha project kubwa za uzalishaji na mawndeleo na kuwapeleka hawa wote huko.

Wamachinga na mamantilie wa sasa hivi na watakao kuja baadae itakuwa mzigo kwa Taifa letu, kwani tuta kosa nguvu kazi kwenye wataalam wa kuiendeleza hii nchi. Nchi itajaa watu wenye akili ya kichuuzi na sio nguvukazi za kuwezesha kuwaza vyema.
 
Mbona pale JNIA hawapelekwi au pale hapakujengwa kwa Kodi?
 
Hujamwelewa mtoa uzi, anasema Rais hajatoa ajira ,kisha anwaambia vijana wasio na ajira wafanye biashara popote kama njia ya kuwapoza kwa kukosa ajira na ni kinyume na sheria za tawala za mikoa.

1. Serikali inakosa mapato
2. Halmashauri zinakosa mapato


Mbona mlimani city hakuna machinga na mambo yapo fire!!

Mlimani city ingekua ya Serikali mle ndani wangejaa machinga hadi basi.
 
Sheria za mipango miji siyo msahafu, inabadilishwa. Pia nyingi ni subsidiary legislations, hazijatungwa na bunge, hivyo zinaweza zikawa zimebadilishwa. Shule hatujaenda kukariri, tunatumia akili kupambana na mazingira yetu.
Pole Sana ndugu yangu maana hata Cha kukuambia sina
 
Umachinga hauna impact kwa uchumi wa nchi na hakuna nchi ilio toboa kwa kukumbatia masikini.

China na ujamaa wake haikumbstii masikini bali matajiri wakubwa na walipa kodi.
 
Hicho ni kielelezo cha misingi mibovu ya uchumi. Tanzania soko la ajira ni jembamba sana ndiyo maana mpaka vijana waliomaliza vyuo vikuu wanakimbilia kufanya biashara za kutembeza bidhaa za madukani.

Zamani machinga alikuwa ni darasa la 7 kwenda nyuma na hususan watu wa Mtwara. Ila sasa hivi kila kabila na kila kiwango cha elimu kina machinga.

Watengeneza sera wetu wamepotea sana katika hili. Namkumbuka Lowassa mwaka 2014 au 2015 alisema ajira kwa vijana ni bomu linalosubiriwa kupasuka.

Awamu ya 5 chini ya MEKO au JIWE kwanza yenyewe haiajiri mpaka itokee dharura, hivyo kwa miaka 5 yawezekana kati ya graduates 50,000 waliofuzu pengine imeajiri 4,000 tu, chini ya 10%

Pili Awamu ya 5 inapiga vita sekta binafsi kwa kufilisi mabenki, kuwanyang'anya fedha matajiri, kuwa harass matajiri Kama Yusuf Manji, kuwabambikiza madai ya UWONGO makampuni ili Serikali ipate fedha kama Halotel, Vodacom etc

Halafu mazingira ya uwekezaji si rafiki. Toka aliookuja DANGOTE wakati wa JK hakuna muwekezaji mwingine serious aliyeongezeka nchini kwa miaka 5 ambaye angeleta mtaji na ajira. Sasa watu wanaendelea kuzaliana, wahitimu wanaongezeka kufuzu, Ila AJIRA zinapungua.

Wachumi wanasema "there is inverse relationships between population growth against economic expansion".

Mwishowe mtoa mada nilitaka nikuambie kuwa hali unayoiona Ubungo ndiyo hali halisi ya uchumi wa Tanzania mnaoambiwa umehamia uchumi wa kati. Ni aibu hata pale City Centre karibu na Sanamu ya Askari upande wa IPS kuna Mama Ntilie wanapika kwa mkaa na kun
 
Miji imekuwa kama mabanda ya kwenye machimbo ya madini, unashangaa City centre watu wanapika na kuni, na samaki zina pairiwa hapo hapo city centre,
 
Watu mnakuwa wepesi kusahau!

Sio hao machinga ndio chadema kabla ya 2015 walikuwa wanampigia kelele JK kwamba hajali haki za watu akigombana nao kupitia mgambo jiji?

Ile machinga complex imejengwa na bado mgambo wakawa wanagombana na machinga? Mpaka kina Lema wanatoka nje ya bunge kuwatetea?
 
Hawa wachuuzi hawana impact kwenye uchumi mkuu na ndo wanao kumbatiwa na wale walipa kodi wakuu wabapigwa vita,

Hivi kiwada kama Dangote wanalipa kodi kiasi gani? Ni pesa ndefu sana ila ona wanavyo pigwa vita.


Miji imegeuka kuwa kama Slum,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…