Kinacho takiwa ni utaratibu nchi zote zina wamachinga ila kuna utaratibu, uko hapo?Watu mnakuwa wepesi kusahau!
Sio hao machinga ndio chadema kabla ya 2015 walikuwa wanampigia kelele JK kwamba hajali haki za watu akigombana nao kupitia mgambo jiji?
Ile machinga complex imejengwa na bado mgambo wakawa wanagombana na machinga? Mpaka kina Lema wanatoka nje ya bunge kuwatetea?
Mkuu ukiwafuatilia wapinzani unaweza kuhisi hawana vichwa.Lakini wanachosahau hapa ni kuwa watu hawa hawa walikua wakitumika na vyama vya upinzani,
Mfano boda boda kuna wakati walikua wanakamatwa wakifika city center ila nyuzi hapa JF hazikukauka kuwatetea kwamba wanaonewa na hawana namna nyingine ya kupata kipato, ikawa hivyo kwa wanasiasa wa upinzani walipiga sana kelele kuhusiana na hao boda boda.
Ninachoona hapa ni kuwa kuna watu wanalilia kupoteza mtaji wao wa kisiasa, kwani kundi hili ndilo walikua wakilitumia kupenyezea agenda zao, sasa kundi limepata mwanga hakuna cha kuwaambia tena.
It is all about politics.
Wapinzani wanalia kupoteza kundi ambalo walikua wanalitumia kudanganya.
Ndo maana kuna kuwa na mipango miji na inaonyesha wapi masoko,stand za mabus,viwanja vya ndege nk,kama stand inakuwa humohumo soko inakuwa haina maana zaid ya uchafu na kero, kama tunawajal wamachinga tungewajengea sehem yao hapo pemben ya stand kama tunaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo,dunia nzima hakuna mchanganyiko wa hivyo!!Mimi kwa hili naona muheshimiwa Raisi yuko sahihi kabisa. Nini chema kwako kuwa na standi maridadi isiyo na watu wakati watu wako wanakufa njaa au kuwa na standi iliyojengwa kwa kodi za watu wako itakayotumiwa na watu wako kujitafutia ridhiki?
Mambo mengine ni kupima manufaa mapana ya taifa na watu wake. Nasimama na muheshimiwa Raisi, raia watanzania wafanye biashara sehemu yoyote isipokua ndani ya nyumba za ibada.
Hakuna lolote mabanda yamevunjwa usiku wa leo pita ubungo uone tanraod walichofanya mengine yamechukuliwa wenyewe wameambiwa wakaripoti.Huwezi liona hili kama huna upeo wa kuwaelewa wanasiasa.
Magufuli amesema Machinaga na Mamantilie wafanye biashara popote bila bughudha yoyote kinyume kabisa na sheria ya mipango miji na sheria ya kodi.
Mfano mzuri ni hapo kariakoo ampapo ni busness hub ya Tanzania na nchi jirani kujazwa machinga kiasi cha kudi-scarage biashara na wafanya biashara wakubwa eneo hilo. Juzi tena stendi ya mabasi ya mikoani na nchi jirani ya Mbezi imegeuzwa gulio kwa sababu za kisiasa.
Nachokiona hapa kuna movement yenye malengo maalumu inaandaliwa kwa ajiri ya mwelekeo mpya wa siasa za nchi yetu. Kundi hili la vijana lililonyimwa ajira rasmi na mamlaka kisha kuelekezwa kufanya uchuuzi usioweza kuwapatia hata pesa ya kulipia bima ya afya ni hatari kwa usalama wa taifa.
Kesho vijana hawa wakitakiwa kuondoka maeneo hayo ni nani ataituliza hasira yao?
Huendi hili lipo nyuma ya ajenda ya kumuongezea muda Mh Rais kupitia maandamano ya makundi Haya baada ya kuona hoja hiyo hiwezi kuanzia bungeni Bali ianzie kwa civilians.
Mzee Mwanakijiji
Waingie sehemu yoyote isipokua nyumba za ibada. Bwana wetu Yesu Kristu alikwisha wahi kuwafurumusha wachuuzi kwenye hekalu hivyo katazo la kiimani lipo. Ikulu na kwingine kote wanaweza kuingia. Tunatibu njaa kwanza, tunataka watu wetu wafanye kazi ili wale, tukivuka hiyo level then tutaanza kuwa maridadi na kuweka makatazo kama hayo ya nani awepo wapi.Msingi wa hoja yako nzima umeuvunjia hapo mwisho, ulipoandika "isipokuwa ndani ya nyumba za ibada."
Hapa umetoa mwanya pawepo na sehemu nyingine kama hiyo ya "nyumba za ibada."
Ikulu waende? Vituo vya polisi nako waingie, magereza, vibarazani kwa nyumba za watu, n.k., n.k,.
Huu ni mpango mbovu, usiokuwa na uendelevu wowote.
Kufanya biashara, kama kazi nyingine yoyote inahitaji mpangilio maalum. Haiwezi kufanywa holelaholela tu.
Kwanza wanunuzi wenyewe ndio hatimae watakaolazimisha vurugu hizi zikome. Hata sasa, pita maeneo ya biashara za aina hii, utakuta mtu yupo siku nzima hapati mnunuzi hata mmoja. Hiyo ni biashara balaa!
Round about ya Askari Monument upande wa IPS, kuna Mama Ntilie anapika.Miji imekuwa kama mabanda ya kwenye machimbo ya madini, unashangaa City centre watu wanapika na kuni, na samaki zina pairiwa hapo hapo city centre,
Siku zote biashara holela inaendana na mengi, mojawapo ni uchafu, bughdha, uhalifu, na maisha yasiyo ya kistaarabu.Mimi kwa hili naona muheshimiwa Raisi yuko sahihi kabisa. Nini chema kwako kuwa na standi maridadi isiyo na watu wakati watu wako wanakufa njaa au kuwa na standi iliyojengwa kwa kodi za watu wako itakayotumiwa na watu wako kujitafutia ridhiki?
Mambo mengine ni kupima manufaa mapana ya taifa na watu wake. Nasimama na muheshimiwa Raisi, raia watanzania wafanye biashara sehemu yoyote isipokua ndani ya nyumba za ibada.
Mpumbavu anafikiria kuwa amemfurahisha mtu kujisaidia hata nje ya uwanja akiona amemsaidia anayejisaidia ovyo. Mwenye akili atamzuia anayejisaidia uwanjani, badala atamsaidia awe na choo.Mipango miji nenda Posta na Masaki huko.
Eti nyie ndo mlikuwa mnataka mpewe nchi muwatetee hao machinga na mamantilie.
Mara hii mshasahau kuwa kuna wakati Sugu alilazimika kutoka bungeni kwenda kuongea na machinga na mamantilie waliokuwa wanafukuzwa katikati ya jiji la Mbeya?
Kweli kuimba kupokezana.
Tofautisha biashara na uchuuzi. Hakuna nchi iliyowahi kufuta umaskini kwa uchuuzi. Kama tunawapenda maskini, tuwe na mipango ya kuwaondoa kwenye umaskini, na siyo kuwafanya kuwa maskini wa kudumu.Kuna muda sheria huvunjwa kwa maslahi ya umma.
Hao machinga ndo waliotupa kura za kutosha.
Halafu jiulize,hao unaowaona huko kariakoo ulitaka tuwapeleke wapi wakafanye biashara zao?
Tunakoelekea tutajenga miji mingine hii iliyopo sasa ibaki kuwa masoko. Ikikukera....hama nchi.
[ATAKAPO TOKEA MTU AKAANZISHA JARIBIO LA KUUVURUGA UTARATIBU WA KIKATIBA ULIOPO BASI AFAHAMU YULE ATAKAYE MPOKEA ATAIVURUGA MARA 1000 ] Maana ataona mbona fulani alifanya, Wazee wa chama na wana ccm jambo hili si la kulionea haya hata kidogoMimi kwa hili naona muheshimiwa Raisi yuko sahihi kabisa. Nini chema kwako kuwa na standi maridadi isiyo na watu wakati watu wako wanakufa njaa au kuwa na standi iliyojengwa kwa kodi za watu wako itakayotumiwa na watu wako kujitafutia ridhiki?
Mambo mengine ni kupima manufaa mapana ya taifa na watu wake. Nasimama na muheshimiwa Raisi, raia watanzania wafanye biashara sehemu yoyote isipokua ndani ya nyumba za ibada.
Sawa.Mpumbavu anafikiria kuwa amemfurahisha mtu kujisaidia hata nje ya uwanja akiona amemsaidia anayejisaidia ovyo. Mwenye akili atamzuia anayejisaidia uwanjani, badala atamsaidia awe na choo.
Rais Magufuli anafanya simple politics kuwafurahia maskini wasuo na uelewa, wakati kiuhalisia, anawafanya kuwa maskini zaidi.
Nyny nd mnaokosea sana kuwachukulia watu kama walemavu taifa hili. Sasa msomi mzima kisa kanyimwa ajira anaend kuuza nyanya mtaani elimu yake ina msaada gani hapo. Binadamu anaweza kusurvive no matter what ila ukimlea sana anabweteka nd maan hao watu na elimu zao wanakaa miaka mi5 bdo machinga wanasubiri ajira 2. Anapata ajira material zote zimepotea anakuja kazini madudu 2 na kuiibia serikali ela kwa hasira. Mtu hawez soma engineering kwa mfano aende kuuza mitumba huo ufanisi atapata wapi? Halafu sio kwamba wafukuzwe swala je ni lazima wafanye biashara hayo maeneo. Supply ikiwa ndog sehemu demand inaongezeka well demand ikiongezeka cost inaongezeka ikifikia hyo stage binadamu atatafuta chimbo la bei rahisi. Kwahyo wakiwa kwemye maeneo maalumu watu watafuata 2.Mkuu machinga anaweza akawa mjomba wako, shangazi yako au kijana wako aliyekosa ajira kwenye mfumo rasmi. Hao wote ni watanzania na hii ni nchi yao. Wanayo haki, kama watanzania wengine, kusaka na kupata riziki yao kwa njia halali ikiwa ni pamoja na kufanya biashara sehemu yoyote ya ardhi ya Tanzania, na jambo hili lina akisi uhuru wao wa kweli na si vinginevyo.
Msamehe bure, ili uqualify kuwa mwanaccm lazima kwanza ujitoe ufahamuNini maana ya kuwa na sheria ya mipango miji? Shule mlienda kusomea ujinga.
I like the way you think, especially on what you wrote in this particular post!!!Siku zote biashara holela inaendana na mengi, mojawapo ni uchafu, bughdha, uhalifu, na maisha yasiyo ya kistaarabu.
Kama Stand ya Mbezi patakuwa holela, watu wanaopenda ustaarabu watapakimbia. Njia bora ya kuwezesha kushamiri biashara, ni kuwa na mazingira ambayo yanawezesha wenye hela kutumiabpesa yao. Pakiwa mahali holela, wenye hela hawataenda eneo hilo, na kama wakati wa kusafiri watatumia stand hiyo, watajizuia kufanya unnecessary movements ndani ya stand.
Stand hiyo kama ingekuwa eneo lenye mpangilio mzuri, ingeweza kutukika kama recreation area, ambapo watu wangeenda kuburudika, na kutumia pesa ambayo ingeiwezesha serikali kukusanya mapato, na indirectly kuwasaidia haobwatu wa chini.
Biashara, uchumi na sifa dhaifu za kisiasa, haviendani.
Em achana na hizo mambo wewe kuna mtu anatetea chama hapa. Sio kila sehemu mnapenda kuchoose side. Ko kila anaepinga jambo fulani linalofanywa na serikali ni chadema. Afu hata hao uliowataja si ni wana siasa? Je una uhakika wasingechanwa kwa hichi kinachoendelea?Watu mnakuwa wepesi kusahau!
Sio hao machinga ndio chadema kabla ya 2015 walikuwa wanampigia kelele JK kwamba hajali haki za watu akigombana nao kupitia mgambo jiji?
Ile machinga complex imejengwa na bado mgambo wakawa wanagombana na machinga? Mpaka kina Lema wanatoka nje ya bunge kuwatetea?
Bado hazajabadilishwa Sasa. Na hizo Sheria zimewekwa ili kulinda hiyo miradi. Ukiweka kila kitu holela unauwa hiyo miradi.Sheria za mipango miji siyo msahafu, inabadilishwa. Pia nyingi ni subsidiary legislations, hazijatungwa na bunge, hivyo zinaweza zikawa zimebadilishwa. Shule hatujaenda kukariri, tunatumia akili kupambana na mazingira yetu.
Umeongea point aisee hivi serikali haizionei wivu hizi mall kwa maelezo yaliyotolewa kuhusu ile stand mi nlitarajia panakuwa kama maeneo ya mall serikali ipige ela. Ila sasa anatokea mtu anatembeza mayai ya kuchemshwa. Shame on our gov.Siku zote biashara holela inaendana na mengi, mojawapo ni uchafu, bughdha, uhalifu, na maisha yasiyo ya kistaarabu.
Kama Stand ya Mbezi patakuwa holela, watu wanaopenda ustaarabu watapakimbia. Njia bora ya kuwezesha kushamiri biashara, ni kuwa na mazingira ambayo yanawezesha wenye hela kutumiabpesa yao. Pakiwa mahali holela, wenye hela hawataenda eneo hilo, na kama wakati wa kusafiri watatumia stand hiyo, watajizuia kufanya unnecessary movements ndani ya stand.
Stand hiyo kama ingekuwa eneo lenye mpangilio mzuri, ingeweza kutukika kama recreation area, ambapo watu wangeenda kuburudika, na kutumia pesa ambayo ingeiwezesha serikali kukusanya mapato, na indirectly kuwasaidia haobwatu wa chini.
Biashara, uchumi na sifa dhaifu za kisiasa, haviendani.