Mimi kwa hili naona muheshimiwa Raisi yuko sahihi kabisa. Nini chema kwako kuwa na standi maridadi isiyo na watu wakati watu wako wanakufa njaa au kuwa na standi iliyojengwa kwa kodi za watu wako itakayotumiwa na watu wako kujitafutia ridhiki?
Mambo mengine ni kupima manufaa mapana ya taifa na watu wake. Nasimama na muheshimiwa Raisi, raia watanzania wafanye biashara sehemu yoyote isipokua ndani ya nyumba za ibada.