Uchaguzi 2020 Rais Magufuli na Tundu Lissu wote ni Wakatoliki wazuri. Je, Kanisa halioni umuhimu wa kuwapatanisha?

Naona wewe ulinyimwa upadre.

 
Sawa lakini sidhani kama shetani atakubaliana hili wazo
 
Kanisa liwapatanishe!? Kwani wamekosana NINI? Hawa kila mmoja ana maono yake. Lissu ana maono ya KUUZA NCHI kwa waliomtuma ili wazidi KUINYONYA NA KUIBA MALI NA UTAJIRI WETU wakati Rais wetu ana maono na mtizamo TOFAUTI KABISANA HUO WA LISSU. Tofauti yao kwenye maono yao, yako mbali zana kama mbingu na nchi.
 
Naunga mkono hoja
 
Acha udini mkuu
 
Kupatanishwa na Lissu? Huyu mtu anayeuza nchi mchana kweupe? Labda kama kanisa halina kazi za kufanya.
Ukisikia tu mtu anasema kuna mtu ameuza nchi, ujue huyo mtu au hana akili au ni mtu wa hila au mnafiki.

Maana kiuhalisia hakuna mtu anayeweza kuuza nchi. Haya maneno ya kusema kuna mtu anaweza kuuza nchi, ni maneno ya mitaani ambayo hushabikiwa na watu waliokosa akili hata ile ya kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Excellent viewpoint. Inasikitisha sana kuona Watanzania wengi wakiwemo wasomi wasivyoelewa maana halisi ya demokrasia. Wanafikiri ni suala la kutafuta mtu (aina ya masihi- toka kwa Mungu) au kikundi cha watu wenye “stahili” ya kudumu ya kuongoza nchi. Hakuna mtu au kikundi chenye sifa ya aina hiyo.

Suala ni wananchi kuwa na nguvu na uwezo wa kuchagua, kudhibiti na kuwajibisha viongozi na kuamua mifumo sahihi ya kusimamia shughuli za umma - muda wote. Ni aibu leo hii tunaendelea kutawaliwa kwa mfumo wa kidikteta ulioasisiwa na kudumishwa na TANU/CCM unaompa mtu mmoja “absolute power” ya kuendesha nchi kwa utashi wake. Mtu mmoja ana madaraka yote ya kutumia rasilimali za umma anavyotaka; kukiuka katiba na sheria anavyojisikia; kugawa vyeo, fursa, na adhabu kwa mtindo wa “patronage”, “cronyism” na “subjugation”. Ni dhahama kubwa.

Na yote hii ni kwa sababu kuna “wasomi” wengi wanaootea “kutoboa” kwa fadhila za “Mheshimiwa Rais”. Tunahitaji Rais ambaye ajenda yake kuu itakuwa marekebisho makubwa ya katiba na uendeshaji nchi.
 
Kupatanishwa na Lissu? Huyu mtu anayeuza nchi mchana kweupe? Labda kama kanisa halina kazi za kufanya.
kupatanishwa na Lisu ni kidunia tu je vip kesho kwa Mungu?
kumbuka Dunia ni mapito.
 

Mwenye makosa ni mmoja tu aliyetaka kuchukuwa roho ya mwenzake wakati yeye sio Mungu
 
Unapatanisha watu wawili wanaogombana, huwezi kupatanisha watu wawili ambapo mmoja anatafuta ugomvi na mwingine yuko kimya.
 
Mwenye makosa ni mmoja tu aliyetaka kuchukuwa roho ya mwenzake wakati yeye sio Mungu
Una ushahidi? Hiz ndizo theory za Lissu na CHADEMA ambazo zinaleta friction isiyokuwa ya lazima. Aliposhambukliwa tu wakaingiza siasa, na hivyo kulifanya tukio lote liwe la kisiasa; eti kwa vile kamera zilizimwa basi ilikuwa ni maagizo ya Magufuli, wakati kila mara kamera zile zilikuwa zinazimika kwa kuwa hazikuwa na uwezo wa kufanya kazi 24/7. Hata kumtibu likawa ni jambo la kichama tu. Hiyo inaweza kuwa strategy nzuri ya kusentionalize wafuasi kisiasa, lakini inaweza isitatue tatizo lenyewe kwani wale mahasidi wake bado wataende;lea kuwapo na huenda bado wanamtafuta na inawezekana pia hawana uhusiano kabisa na serikali. Hapo inakuwa ni mwazno wa machafuko yasiokuwa na tija nchini. Hata Mbowe alipoteleza kwenye ngazi akiwa amelewa akatenguka mguu naye alianza kwa kutangaza kuwa alishambuliwa na watu "wasiojulikana" mpaka alipoumbuliwa ndipo akanyamaza.

Kuna kachero mmoja Evaristi Chahali alichambua tukio lile vizuri sana na kunifanya niambini kuwa maadui wa Lissu walikuwa ni watu wasiokuwa na uhusiano na serikali kwa sababu za kiufundi wa kikachero kama alivyozitoa. Chahali alikuwa mmoja wa makachero wa Tanzania waliobobea sana kabla ya kuhamia uskochi.
 
Hili nalo ni jambo njema
 
roma mkatoliki, mo dewj, ben saanane, azori, nondo, kanguye...kwa uchache sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…