Jukwaa lina watu wa kila aina.
Kama tukilitumia jukwaa hili, kujifunza, kujielemisha, kujitafakari na kujirudi, tutaiona JF ni zawadi toka kwa Mungu kwaajili ya maisha yetu, kwaajili ya usalama wetu, kwaajili ya wokovu wetu, kwaajili ya mafanikio na ustawi wetu.
Japo wapo wanaotaka kuigeuza JF ionekane ni genge la wahuni, wajinga, wanafiki, n.k; lakini watu ambao Mungu amewajalia hekima, uelewa, unabii, uponyaji na maarifa mbalimbali, wasivunjike moyo bali waendelee kutoa kwa wengine kile ambacho Mungu wetu amewajalia.