Rais Magufuli ndiyo ameuona sasa utendaji kazi mbovu wa Jeshi letu la Polisi?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,076
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, Rais Magufuli akitoa lawama kwa watendaji wa Jeshi letu la Polisi kuwa baadhi ya utendaji wao wa kazi kwa kweli hauridhishi.

Akitolea mfano utekwaji nyara wa mfanyibiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji, ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Mo, ambaye tokea lilipotokea suala la utekwaji nyara wake, ambapo ulitokea mwezi Oktoba mwaka jana, hivi sasa ni zaidi ya miezi 5 tumeshuhudia zaidi "movie" katika upelelezi wake, ambapo hadi Leo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na skendo hiyo!

Ndiyo hapo nikawa najiuliza iweje Leo hii ikiwa imepita miezi zaidi ya 5 tokea tukio hilo litokee nchini ndipo Rais anajitokeza hadharani kulilaumu Jeshi lake la Polisi?

Hivi hakuwa akiona kupitia mitandao ya kijamii, hususani mtandao huu wa Jamii Forum namna sisi "whistle blowers" tulivyokuwa tukilishutumu vikali Jeshi lake la Polisi namna linavyofanya "maigizo" katika masuala muhimu ya usalama wa raia na mali zao?

Hivi yeye Mheshimiwa Rais hajui kuwa wajibu na 1 wa Jeshi letu la Polisi nchini ni kulinda uhai wa raia wake na Mali zao?

Hivi si yeye Mheshimiwa Rais tulimsikia wenyewe kwa masikio yetu akiliambia Jeshi lake la Polisi kuwa eti wakiua "jambazi" basi asisikie akiburuzwa mahakamani na badala yake asikie akipongezwa na kupandishwa cheo?

Hivi mbona hatujamsikia Mheshimiwa Rais akiyaongelea matukio mengine mengi tu ya kutekwa akina Roma Mkatoliki,kupigwa risasi mchana kweupe kwa Mheshimiwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kuuawa kwa Mwenyekiti wa Chadema, mkoani Geita, Alphonce Mawazo, kuyataja baadhi ya matukio mengi yanayotokea nchini hivi na kutekelezwa na "watu wasiojulikana" ambayo nayo hatujawahi kusikia Jeshi letu la Polisi likimkamata hata mtuhumiwa .mmoja na kumuhoji na baadaye kumburuza mahakamani??

Iweje leo hii Mheshimiwa Rais aliongelee suala la Mo,kuwa ni "special case" na kueleza kuwa Jeshi letu la Polisi limefanya uzembe wa kutoweza mkamata mtuhumiwa yeyote kwa mahojiano na kuwaburuza mahakamani?

Hivi katika utendaji kazi wao akina IGP, Simon Sirro na Kamanda wa kipolisi, wa kanda maalum ya kipolisi Dar, Athumani Mambosaa, ambao sisi wadau tumekuwa tukiwalalamikia kwa muda mrefu sana kuhusu utendaji kazi wao wa "maigizo" ni kwanini Mheshimiwa Rais hajawafukuza kazi?

Ndipo hapo wananchi tumejiuliza swali muhimu sana ya kuwa hivi Mheshimiwa Rais alikuwa "serious" kweli wakati analilaumu Jeshi lake la Polisi?

Nimekuwa pia najiuliza hivi ni kitu gani kilichosababisha Mheshimiwa Rais alilaumu Leo Jeshi letu la Polisi kuhusiana na suala la utekwaji wa mfanyibiashara maarufu nchini, wakati huko nyuma Jeshi hilo la Polisi katika utendaji kazi wake mbovu, lilikuwa likipata "all blessings" kutoka kwake Mheshimiwa Rais?

Mungu ibariki Tanzania
 
Sio hauridhishi tu, ni mbovu na wa kionevu zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani Jeshi letu la Polisi linafanya kazi kama vile ni mojawapo ya vitengo vya Sisiem, UVCCM. Ova

Hilo halioni Mheshimiwa Rais, Bali ameliona la kutekwa nyara kwa mfanyibiahara maarufu nchini, Mohammed Dewji!

Ndipo hapo wananchi tunajiuliza,au kapata shinikizo kutoka Jumuiya ya kimataifa, kuhusiana na utendaji kazi mbovu wa Jeshi letu la Polisi??

Kwa kuwa siyo bure Bali iko namna.........
 
JIWE ameanza kuwa mwanasiasa. Polepole anazua tatizo, analikana Kisha analitatua kujipatia umaarufu. Huo ndio uanasiasa. Anakaribia kuhitimu katika unafiki huu. Atakapohitimu, sifa ya JIWE itakoma na kubaki kuwa muhuni wa siasa kama watangulizi wake ukimtoa Baba wa Taifa, Nyerere.
 
Mtiti alio uanzisha Lissu kule nje ndio kisa cha kutoa tamko la aina hiyo. Hiyo kauli ni kama kusema "hata mimi nashangaa kwa nini hawa Polisi hawafanyi uchunguzi?"
Ninachojiuliza ni kwa namna alivyo na " zero tolerance" kwa watendaji wake, ni kwanini hadi sasa IGP, Simon Sirro na Kamanda Athumani Mambosasa hajawafukuza kazi kama kweli alikuwa "serious" na kauli yake??

Kama hajachukua hatua yoyote dhidi ya makamanda hao, sisi wananchi tutajua Rais wetu alikuwa "location" wakati akitoa tamko hilo!
 
Tatizo sio police.

Tatizo ni mfumo wa kikatiba.

Mfumo wa utawala uliomo kwenye katiba.

Upo umuhimu wa kutenganisha dola ambavyo ni Vyombo vya ulinzi na serikali.

Hata mahakama zinahita ji kuwa huru, na uhuru upo katika uteuzi. Tuondoe madaraka Ya Rais kuteuwa, jaji na police, hata kuondoa ameri jeshi mkuu. Tufijirie njia nyengine zaidi ya uhuru ya mihimili hii muhimu.

Hata tume ya uchaguzi pamoja na msajili wa vyama vya siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachojiuliza ni kwa namna alivyo na " zero tolerance" kwa watendaji wake, ni kwanini hadi sasa IGP, Simon Sirro na Kamanda Athumani Mambosasa hajawafukuza kazi kama kweli akikuwa "serious" na kauli yake??

Kama hajachukua hatua yoyote dhidi ya makamanda hao, sisi wananchi tutajua Rais wetu alikuwa "location" wakati akitoa tamko hilo!
Hilo la kuwa LOCATION ndio jibu sahihi, na hawezi kubadilika kwa sababu sisi wananchi tumejenga tabia ya ukimuona Jangala au Kingwendu hata katika maisha ya kawaida na mambo serious azungumze na afanye yale tunayoyaona kwenye clips tununuazo.
 
Tatizo sio police.

Tatizo ni mfumo wa kikatiba.

Mfumo wa utawala uliomo kwenye katiba.

Upo umuhimu wa kutenganisha dola ambavyo ni Vyombo vya ulinzi na serikali.

Hata mahakama zinahita ji kuwa huru, na uhuru upo katika uteuzi. Tuondoe madaraka Ya Rais kuteuwa, jaji na police, hata kuondoa ameri jeshi mkuu. Tufijirie njia nyengine zaidi ya uhuru ya mihimili hii muhimu.

Hata tume ya uchaguzi pamoja na msajili wa vyama vya siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani kwa Katiba hii tuliyo nayo na aina ya Rais tuliye naye, hakika watu wa upande ule tunaoitwa,siyo wazalendo hakika TUTAPATA TAABU SANA!
 
Mohamed Dewji - CCM
Alphonce Mawazo - CDM
Tundu Lissu - CDM
Roma Mkatoliki - Sio CCM

Hapa kuna cha kushangaza?

Hivi Ruge Mutahaba angekuwa CDM unadhani ndege ingetolewa bure isafirishe wafiwa?

Tumebahatika kupata Rais wa raia wa CCM
 
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, Rais Magufuli akitoa lawama kwa watendaji wa Jeshi letu la Polisi kuwa baadhi ya utendaji wao wa kazi kwa kweli hauridhishi.

Akitolea mfano utekwaji nyara wa mfanyibiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji, ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Mo, ambaye tokea lilipotokea suala la utekwaji nyara wake, ambapo ulitokea mwezi Oktoba mwaka jana, hivi sasa ni zaidi ya miezi 5 tumeshuhudia zaidi "movie" katika upelelezi wake, ambapo hadi Leo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na skendo hiyo!

Ndiyo hapo nikawa najiuliza iweje Leo hii ikiwa imepita miezi zaidi ya 5 tokea tukio hilo litokee nchini ndipo Rais anajitokeza hadharani kulilaumu Jeshi lake la Polisi??

Hivi hakuwa akiona kupitia mitandao ya kijamii, hususani mtandao huu wa Jamii Forum namna sisi "whistle blowers" tulivyokuwa tukilishutumu vikali Jeshi lake la Polisi namna linavyofanya "maigizo" katika masuala muhimu ya usalama wa raia na mali zao??

Hivi yeye Mheshimiwa Rais hajui kuwa wajibu na 1 wa Jeshi letu la Polisi nchini ni kulinda uhai wa raia wake na Mali zao??

Hivi si yeye Mheshimiwa Rais tulimsikia wenyewe kwa masikio yetu akiliambia Jeshi lake la Polisi kuwa eti wakiua "jambazi" basi asisikie akiburuzwa mahakamani na badala yake asikie akipongezwa na kupandishwa cheo??

Hivi mbona hatujamsikia Mheshimiwa Rais akiyaongelea matukio mengine mengi tu ya kutekwa akina Roma Mkatoliki,kupigwa risasi mchana kweupe kwa Mheshimiwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kuuawa kwa Mwenyekiti wa Chadema, mkoani Geita, Alphonce Mawazo, kuyataja baadhi ya matukio mengi yanayotokea nchini hivi na kutekelezwa na "watu wasiojulikana" ambayo nayo hatujawahi kusikia Jeshi letu la Polisi likimkamata hata mtuhumiwa .mmoja na kumuhoji na baadaye kumburuza mahakamani??

Iweje leo hii Mheshimiwa Rais aliongelee suala la Mo,kuwa ni "special case" na kueleza kuwa Jeshi letu la Polisi limefanya uzembe wa kutoweza mkamata mtuhumiwa yeyote kwa mahojiano na kuwaburuza mahakamani??

Hivi katika utendaji kazi wao akina IGP, Simon Sirro na Kamanda wa kipolisi, wa kanda maalum ya kipolisi Dar, Athumani Mambosaa, ambao sisi wadau tumekuwa tukiwalalamikia kwa muda mrefu sana kuhusu utendaji kazi wao wa "maigizo" ni kwanini Mheshimiwa Rais hajawafukuza kazi??

Ndipo hapo wananchi tumejiuliza swali muhimu sana ya kuwa hivi Mheshimiwa Rais alikuwa "serious" kweli wakati analilaumu Jeshi lake la Polisi??

Nimekuwa pia najiuliza hivi ni kitu gani kilichosababisha Mheshimiwa Rais alilaumu Leo Jeshi letu la Polisi kuhusiana na suala la itekwaji nyara wa mfanyibiashara maarufu nchini, wakati huko nyuma Jeshi hilo la Polisi katika utendaji kazi wake mbovu, lilikuwa likipata "all blessings" kutoka kwake Mheshimiwa Rais??

Mungu ibariki Tanzania
amejaribu kueleza na alipenda kujua muafaka na hatima ya kitendo cha utekaji wa mo, kukaa kwake kimya kulifanya baadhi ya watu kushangaa na kujiuliza kwann serikali ipo kimya, ila alifanya vile ili asiweze kuingia uchunguzi na kazi ya polisi ila mpaka mwisho hakuna cha maana kilichotajwa na polisi kutokana na story yao ya tukio lote la mo
 
Tatizo la viongozi wetu ni waongo halafu niwasahaulifu[emoji41]
Na Katiba yetu inampa madaraka makubwa sana ya mungu-mtu Rais wetu wa nchi......

Kila analolifanya hawezi hojiwa chochote!
 
Tatizo la viongozi wetu ni waongo halafu niwasahaulifu[emoji41]
Halafu kitu kingine kinachompa "kiwewe" Jiwe ni kusikia kuwa Tundu Lissu atalihutubia bunge la Marekani la Congress mwezi ujao wa April.

Inatarajiwa kuwa Tundu Lissu atakapounguruma pia ataelezea kuwa tokea amiminiwe risasi zaidi ya 30, tena kwenye makazi ya viongozi wa serikali, hivi sasa ni zaidi ya mwaka mmoja na nusu hakuna Hata mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa na Jeshi la Polisi, kwa mahojiano na baadaye kuburuzwa mahakamani
 
Mnafiki mkubwa huyo mbona hakuulizia uchunguzi kuhusu shambulizi la kutaka kumuua lissu, kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na miili iliyookotwa ufukweni.

Mo Dewji alitekwa miezi mitano iliyopita kipindi chote hicho alikuwa kimya bila kusema chochote kile leo ndiyo anajibaraguza na unafiki wake.
 
Lissu ametushika pabaya. Ujumbe wake kwa mataifa ya mbali dhidi ya jeshi pendwa umefika sasa tunajikosha.
 
Huyu jamaa ni kama mtu mwenye vichwa vingi. Atakachoongea leo na kesho itategemea kavaa kichwa kipi.

Uongozi ni talanta. Mtu huzaliwa nao.
 
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, Rais Magufuli akitoa lawama kwa watendaji wa Jeshi letu la Polisi kuwa baadhi ya utendaji wao wa kazi kwa kweli hauridhishi.

Akitolea mfano utekwaji nyara wa mfanyibiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji, ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Mo, ambaye tokea lilipotokea suala la utekwaji nyara wake, ambapo ulitokea mwezi Oktoba mwaka jana, hivi sasa ni zaidi ya miezi 5 tumeshuhudia zaidi "movie" katika upelelezi wake, ambapo hadi Leo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na skendo hiyo!

Ndiyo hapo nikawa najiuliza iweje Leo hii ikiwa imepita miezi zaidi ya 5 tokea tukio hilo litokee nchini ndipo Rais anajitokeza hadharani kulilaumu Jeshi lake la Polisi??

Hivi hakuwa akiona kupitia mitandao ya kijamii, hususani mtandao huu wa Jamii Forum namna sisi "whistle blowers" tulivyokuwa tukilishutumu vikali Jeshi lake la Polisi namna linavyofanya "maigizo" katika masuala muhimu ya usalama wa raia na mali zao??

Hivi yeye Mheshimiwa Rais hajui kuwa wajibu na 1 wa Jeshi letu la Polisi nchini ni kulinda uhai wa raia wake na Mali zao??

Hivi si yeye Mheshimiwa Rais tulimsikia wenyewe kwa masikio yetu akiliambia Jeshi lake la Polisi kuwa eti wakiua "jambazi" basi asisikie akiburuzwa mahakamani na badala yake asikie akipongezwa na kupandishwa cheo??

Hivi mbona hatujamsikia Mheshimiwa Rais akiyaongelea matukio mengine mengi tu ya kutekwa akina Roma Mkatoliki,kupigwa risasi mchana kweupe kwa Mheshimiwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kuuawa kwa Mwenyekiti wa Chadema, mkoani Geita, Alphonce Mawazo, kuyataja baadhi ya matukio mengi yanayotokea nchini hivi na kutekelezwa na "watu wasiojulikana" ambayo nayo hatujawahi kusikia Jeshi letu la Polisi likimkamata hata mtuhumiwa .mmoja na kumuhoji na baadaye kumburuza mahakamani??

Iweje leo hii Mheshimiwa Rais aliongelee suala la Mo,kuwa ni "special case" na kueleza kuwa Jeshi letu la Polisi limefanya uzembe wa kutoweza mkamata mtuhumiwa yeyote kwa mahojiano na kuwaburuza mahakamani??

Hivi katika utendaji kazi wao akina IGP, Simon Sirro na Kamanda wa kipolisi, wa kanda maalum ya kipolisi Dar, Athumani Mambosaa, ambao sisi wadau tumekuwa tukiwalalamikia kwa muda mrefu sana kuhusu utendaji kazi wao wa "maigizo" ni kwanini Mheshimiwa Rais hajawafukuza kazi??

Ndipo hapo wananchi tumejiuliza swali muhimu sana ya kuwa hivi Mheshimiwa Rais alikuwa "serious" kweli wakati analilaumu Jeshi lake la Polisi??

Nimekuwa pia najiuliza hivi ni kitu gani kilichosababisha Mheshimiwa Rais alilaumu Leo Jeshi letu la Polisi kuhusiana na suala la utekwaji wa mfanyibiashara maarufu nchini, wakati huko nyuma Jeshi hilo la Polisi katika utendaji kazi wake mbovu, lilikuwa likipata "all blessings" kutoka kwake Mheshimiwa Rais??

Mungu ibariki Tanzania
Sisi tuliosomea kwa undani mambo ya facial expression tunaelewa kila kitu.
 
Back
Top Bottom