Rais Magufuli ndiyo ameuona sasa utendaji kazi mbovu wa Jeshi letu la Polisi?

Rais Magufuli ndiyo ameuona sasa utendaji kazi mbovu wa Jeshi letu la Polisi?

Mifano hii itathibitisha kuwa Jeshi la Polisi linatekeleza majukumu yake kwa maagizo yake Jiwe

Wakati akimsifu Spika Ndigai kwa jinsi anavyowatesa wabunge wa upinzani na kuwatoa nje ya Bunge, alinukukuliwa akisema kuwa wakija huku nje, aachiwe yeye ambaye ata-deal nao......

Hivi unadhani ana uwezo wa kupambana na akina Mbowe personally??

Alichokuwa akimaanisha ni kuwa atalitumia Jeshi lake la Polisi kuwatesa!

Mfano wa pili ni pale Chuo kikuu cha Dar alipokuwa akifungua maktaba mpya alipomwambia Lowassa awaeleze waliokuwa viongozi wenzake wa Chadema kuwa "wa-behave" ama sivyo wataishia jela.......

Unadhani yeye ana uwezo wa kumpeleka mtu jela zaidi ya "kuliagiza" Jeshi lake la Polisi liwakamate viongozi wa upinzani kwa tuhuma za kughudhi na kuwafikisha mahakamani na hatimaye mahakama nazo kutenda "figisu figisu" zake zinazosababosha hao viongozi wa upinzani waozee jela!

Kama ambavyo akina Mbowe na Matiko wanavyoozea jela hivi sasa!
 
Hivi katika utendaji kazi wao akina IGP, Simon Sirro na Kamanda wa kipolisi, wa kanda maalum ya kipolisi Dar, Athumani Mambosaa, ambao sisi wadau tumekuwa tukiwalalamikia kwa muda mrefu sana kuhusu utendaji kazi wao wa "maigizo" ni kwanini Mheshimiwa Rais hajawafukuza kazi??

Lazaro Mambosasa mkuu, aksante
 
Mnafiki mkubwa huyo mbona hakuulizia uchunguzi kuhusu shambulizi la kutaka kumuua lissu, kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda na miili iliyookotwa ufukweni.

Mo Dewji alitekwa miezi mitano iliyopita kipindi chote hicho alikuwa kimya bila kusema chochote kile leo ndiyo anajibaraguza na unafiki wake.
kama alivyosema watanzania sio wajinga tunaelewa yaliyo mkuta MO, aliyekuwa mwenye kiti wa Yanga ,Zakaria na matajili wengine tunaohisi utajili wao siyo wa halali. mzee kajisalimisha yangemkuta nae lazima waishi kishetani
 
Hapa Mambosasa upaki virago vyako...
...karibuni utakua mbuzi wa kafara....yaani zile kalmat,tambuu na chai ya pilipili ulizokua unakunywa zitatafuta pa kutokea

....wiki 2 mtu hajaonekana we unakwenda kwake kujiraaamba....aiseeee we polisi vp?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, Rais Magufuli akitoa lawama kwa watendaji wa Jeshi letu la Polisi kuwa baadhi ya utendaji wao wa kazi kwa kweli hauridhishi.

Akitolea mfano utekwaji nyara wa mfanyibiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji, ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Mo, ambaye tokea lilipotokea suala la utekwaji nyara wake, ambapo ulitokea mwezi Oktoba mwaka jana, hivi sasa ni zaidi ya miezi 5 tumeshuhudia zaidi "movie" katika upelelezi wake, ambapo hadi Leo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na skendo hiyo!

Ndiyo hapo nikawa najiuliza iweje Leo hii ikiwa imepita miezi zaidi ya 5 tokea tukio hilo litokee nchini ndipo Rais anajitokeza hadharani kulilaumu Jeshi lake la Polisi??

Hivi hakuwa akiona kupitia mitandao ya kijamii, hususani mtandao huu wa Jamii Forum namna sisi "whistle blowers" tulivyokuwa tukilishutumu vikali Jeshi lake la Polisi namna linavyofanya "maigizo" katika masuala muhimu ya usalama wa raia na mali zao??

Hivi yeye Mheshimiwa Rais hajui kuwa wajibu na 1 wa Jeshi letu la Polisi nchini ni kulinda uhai wa raia wake na Mali zao??

Hivi si yeye Mheshimiwa Rais tulimsikia wenyewe kwa masikio yetu akiliambia Jeshi lake la Polisi kuwa eti wakiua "jambazi" basi asisikie akiburuzwa mahakamani na badala yake asikie akipongezwa na kupandishwa cheo??

Hivi mbona hatujamsikia Mheshimiwa Rais akiyaongelea matukio mengine mengi tu ya kutekwa akina Roma Mkatoliki,kupigwa risasi mchana kweupe kwa Mheshimiwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kuuawa kwa Mwenyekiti wa Chadema, mkoani Geita, Alphonce Mawazo, kuyataja baadhi ya matukio mengi yanayotokea nchini hivi na kutekelezwa na "watu wasiojulikana" ambayo nayo hatujawahi kusikia Jeshi letu la Polisi likimkamata hata mtuhumiwa .mmoja na kumuhoji na baadaye kumburuza mahakamani??

Iweje leo hii Mheshimiwa Rais aliongelee suala la Mo,kuwa ni "special case" na kueleza kuwa Jeshi letu la Polisi limefanya uzembe wa kutoweza mkamata mtuhumiwa yeyote kwa mahojiano na kuwaburuza mahakamani??

Hivi katika utendaji kazi wao akina IGP, Simon Sirro na Kamanda wa kipolisi, wa kanda maalum ya kipolisi Dar, Athumani Mambosaa, ambao sisi wadau tumekuwa tukiwalalamikia kwa muda mrefu sana kuhusu utendaji kazi wao wa "maigizo" ni kwanini Mheshimiwa Rais hajawafukuza kazi??

Ndipo hapo wananchi tumejiuliza swali muhimu sana ya kuwa hivi Mheshimiwa Rais alikuwa "serious" kweli wakati analilaumu Jeshi lake la Polisi??

Nimekuwa pia najiuliza hivi ni kitu gani kilichosababisha Mheshimiwa Rais alilaumu Leo Jeshi letu la Polisi kuhusiana na suala la utekwaji wa mfanyibiashara maarufu nchini, wakati huko nyuma Jeshi hilo la Polisi katika utendaji kazi wake mbovu, lilikuwa likipata "all blessings" kutoka kwake Mheshimiwa Rais??

Mungu ibariki Tanzania
Ngoja nikusaidie kidogo yy wakt akiwa Waziri wa Ujenzi alimpa kesi ya kutishia kuua muandishi moja hv ambae baadae alikuwa Mkuu wa wilaya kisa kuandikwa hbr yke khs kuonga nyumba ya serikali pamoja kumuuzia mdogo wake kinyume na utaratibu ss utategemea udhilifu kutoka kwenye serikali ya mtu huyo...
tapatalk_1542123640746.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumemsikia wenyewe kwa masikio yetu, Rais Magufuli akitoa lawama kwa watendaji wa Jeshi letu la Polisi kuwa baadhi ya utendaji wao wa kazi kwa kweli hauridhishi.

Akitolea mfano utekwaji nyara wa mfanyibiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji, ambaye anafahamika zaidi kwa jina la Mo, ambaye tokea lilipotokea suala la utekwaji nyara wake, ambapo ulitokea mwezi Oktoba mwaka jana, hivi sasa ni zaidi ya miezi 5 tumeshuhudia zaidi "movie" katika upelelezi wake, ambapo hadi Leo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na skendo hiyo!

Ndiyo hapo nikawa najiuliza iweje Leo hii ikiwa imepita miezi zaidi ya 5 tokea tukio hilo litokee nchini ndipo Rais anajitokeza hadharani kulilaumu Jeshi lake la Polisi??

Hivi hakuwa akiona kupitia mitandao ya kijamii, hususani mtandao huu wa Jamii Forum namna sisi "whistle blowers" tulivyokuwa tukilishutumu vikali Jeshi lake la Polisi namna linavyofanya "maigizo" katika masuala muhimu ya usalama wa raia na mali zao??

Hivi yeye Mheshimiwa Rais hajui kuwa wajibu na 1 wa Jeshi letu la Polisi nchini ni kulinda uhai wa raia wake na Mali zao??

Hivi si yeye Mheshimiwa Rais tulimsikia wenyewe kwa masikio yetu akiliambia Jeshi lake la Polisi kuwa eti wakiua "jambazi" basi asisikie akiburuzwa mahakamani na badala yake asikie akipongezwa na kupandishwa cheo??

Hivi mbona hatujamsikia Mheshimiwa Rais akiyaongelea matukio mengine mengi tu ya kutekwa akina Roma Mkatoliki,kupigwa risasi mchana kweupe kwa Mheshimiwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, kuuawa kwa Mwenyekiti wa Chadema, mkoani Geita, Alphonce Mawazo, kuyataja baadhi ya matukio mengi yanayotokea nchini hivi na kutekelezwa na "watu wasiojulikana" ambayo nayo hatujawahi kusikia Jeshi letu la Polisi likimkamata hata mtuhumiwa .mmoja na kumuhoji na baadaye kumburuza mahakamani??

Iweje leo hii Mheshimiwa Rais aliongelee suala la Mo,kuwa ni "special case" na kueleza kuwa Jeshi letu la Polisi limefanya uzembe wa kutoweza mkamata mtuhumiwa yeyote kwa mahojiano na kuwaburuza mahakamani??

Hivi katika utendaji kazi wao akina IGP, Simon Sirro na Kamanda wa kipolisi, wa kanda maalum ya kipolisi Dar, Athumani Mambosaa, ambao sisi wadau tumekuwa tukiwalalamikia kwa muda mrefu sana kuhusu utendaji kazi wao wa "maigizo" ni kwanini Mheshimiwa Rais hajawafukuza kazi??

Ndipo hapo wananchi tumejiuliza swali muhimu sana ya kuwa hivi Mheshimiwa Rais alikuwa "serious" kweli wakati analilaumu Jeshi lake la Polisi??

Nimekuwa pia najiuliza hivi ni kitu gani kilichosababisha Mheshimiwa Rais alilaumu Leo Jeshi letu la Polisi kuhusiana na suala la utekwaji wa mfanyibiashara maarufu nchini, wakati huko nyuma Jeshi hilo la Polisi katika utendaji kazi wake mbovu, lilikuwa likipata "all blessings" kutoka kwake Mheshimiwa Rais??

Mungu ibariki Tanzania
2020 hiyooo yaja kwenye horizon. mtu anatafuta gia ya kuwavuta wenye nazo kuibeba 2020.
 
Yaani Jeshi letu la Polisi linafanya kazi kama vile ni mojawapo ya vitengo vya Sisiem, UVCCM. Ova

Hilo halioni Mheshimiwa Rais, Bali ameliona la kutekwa nyara kwa mfanyibiahara maarufu nchini, Mohammed Dewji!

Ndipo hapo wananchi tunajiuliza,au kapata shinikizo kutoka Jumuiya ya kimataifa, kuhusiana na utendaji kazi mbovu wa Jeshi letu la Polisi??

Kwa kuwa siyo bure Bali iko namna.........

Kibano cha kutoka nje huwa kina randi zote na kadri tunavyozidi kuboronga basi kabla ya uchaguzi maluweluwe mengi tutayaona
 
MKUU WA NCHI ALIUACHA MCHEZO UCHEZWE KWANZA AONE MATOKEO NAZAN KASHAJUA NA MATOKEO SOON YATAONEKANA KUNA WATU WANARUDI KIJIJIN SIO MUDA




"Tumerudi kutoka bukoba msibani "

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania tumelaanika kuwa na Rais muongo,mnafiki na kigeugeu....ni Rais wa matukio,....ni Rais asiye makini kwa raia waliompa dhamana ya uongozi.
Watanzania tumejaliwa kuwa wapole ila tumelaaniwa kutokuwa na viongozi waadilifu (zaidi ya BABA WA TAIFA J.K.NYERERE Mwenyezi Mungu tunakuomba upumzishe mbwawani mwako).
Tuna Rais asiyejali wala kufikiria anachokiongea wakati gani aongee na ni Rais mwenye kiburi cha kijinga.
 
JIWE ameanza kuwa mwanasiasa. Polepole anazua tatizo, analikana Kisha analitatua kujipatia umaarufu. Huo ndio uanasiasa. Anakaribia kuhitimu katika unafiki huu. Atakapohitimu, sifa ya JIWE itakoma na kubaki kuwa muhuni wa siasa kama watangulizi wake ukimtoa Baba wa Taifa, Nyerere.
Anafanya childish
 
Anatugeuza watanzania wote kuwa wapumbavu na malofa!
Ndiyo maana halisi hiyo. Hebu fikiria! Majanga yooote yaliyotokea nchini, kaliona tukio la Mo tu?
Kuna muda gani toka tukio la Mo, ndiyo aje aone Leo Polisi hawafanyi vizuri?
Mbona kwa Akwirina hakuwalaumu nk! WATANZANI NI WAPUMBAVU KULIKO.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mtu wa hadhi kama yake ya Urais hastahili kabisa kutafuta kiki za "kitoto" kama tukio hili la kutekwa kwa Mo

Yeye Rais hawezi tugeuza watanzania wote kuwa ni wapumbavu na malofa!
MKUU MYSTERY, amekwisha weza! Tanzaniano,PUMBAFU TOTALY. Anatugeuza wanavyotaka afu mkuu unasema anataka kutufanya!!! TAYARI SISI NI WAPUMBAVU.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachojiuliza ni kwa namna alivyo na " zero tolerance" kwa watendaji wake, ni kwanini hadi sasa IGP, Simon Sirro na Kamanda Athumani Mambosasa hajawafukuza kazi kama kweli alikuwa "serious" na kauli yake??
Kama hajachukua hatua yoyote dhidi ya makamanda hao, sisi wananchi tutajua Rais wetu alikuwa "location" wakati akitoa tamko hilo!
Ni shida sana hili linchi, naamini hawa wote wasanii wanahusika direct na sakata la MO, na nilisema haya kabla, naona wameanza kuumbuana.
 
Back
Top Bottom