Uchaguzi 2020 Rais Magufuli ndiyo anaibuka kuwa atawaongezea mishahara wafanyakazi. Tunamwambia kuwa hatudanganyiki ng'oo

Mkuu umerudi lini? Kwa maana CCM ilishasema wazi kuwa kwa hila na makusudi ya wafanyakazi haihitaji kura zao toka enzi ya JK
 
Meko anaropoka tu hali yake ni mbaya sana,kesho anakuja kaskazini sijui kuuza sura.alishasema hapeleki maendeleo kaskazini sasa sijui kaja kuomba kura za nini...kura zikilindwa ccm hawatoboi majimbo ya kaskazini labda simanjiro na kiteto
 
Mtakoma mwaka huu. Miaka 5 yote mlikuwa wapi? Why now?
Hao maccm walidhani kuwa mwaka 2020 hautafika kamwe!

Ndiyo maana hivi sasa umefika, wanahaha huku na kule na kutafuta kila aina ya uwongo wa kutudanganya watanzania, wakidhani kuwa ndiyo tutadanganyika kirahisi...........

Safari hii tushasema kuwa hatudanganyiki tena na tayari tushavinoa vinoleo vyetu, tayari kwa kazi ya tarehe 28/10/2020
 
Alishindwa miaka 5 ndo ataweza mitano tena.
Sisi sio mademu wa kudanganywa
 
Kama Magufuli ameacha uwongo wa kuwadanganya watumishi wa umma hakutakiwa kuwadanganya tena kwa kutoa ahadi ya uwongo kwa watumishi wa umma ili wampigie kura.

Bali alitakiwa afanye kwa vitendo, watumishi wa umma wakiamka wakute akaunti zao zimetuna,kwa kuwa uwezo huo anao na siyo kuendelea kuwadanganya watumishi wa umma kipindi cha uchaguzi ili apate kura zao.
 
Shule mnaenda kusomea ujinga??????
 
Anadhani sisi watoto wa kutudanganya?
 
Tena alikuwa akijibu hoja na vitisho juu

Yeye alidhani kuwa mwaka wa uchaguzi hautafika milele!

Sikiliza hii:
Tumpumzishe mtu huyu wiki ijayo.

Huyu Magufuli ni mwongo na mnafiki haijawai tokea. Sikiliza hii:
Sikiliza kauli yake hapa:

 
Alisema akipandisha Mshahara italeta mfumuko wa bei,kwa hio sasa hivi akiongeza haitaleta inflation sio?
 
Wafanyakazi msikubali kudanganywa na huyo mtu muongo sana. Akipata atasema hataongeza hadi miradi iishe hivyo wafanyakazi kuendelea kuumia. Ameona uwezekano wa kushinda ni mdogo sasa anawadanganya tena.MSIKUBALI KUMPA KURA ZENU.
 
Hali gani ya maisha iliyopanda mpunga 40,000/= mahindi 30,000/= na mfumuko wa bei 3.4 na wengine wakiwa jukwaani wanaongea wazi mazao ya wakulima bei ni ndogo au unasemea vitu gani vilivyopanda maana hata cement huku nilipo bado 16,500/= sio kubwa kivile.
Kulipa mishahara sio mchezo unawafanyakazi wa umma 1m kati ya wananchi 60m unakusanya 1.5t na ukumbuke hapo aliingia kakuta bilion 850 tu zinazokusanywa kwa mwezi ndio sababu hata mishahara ilikuwa inakopwa ,utawezaje kuongeza mishahara hata kama wewe ndio Rais .Kwahiyo hao wafanyakazi 1m watakula nusu ya makusanyo TRA kinachofata miradi haiendi mtakuja kutukana kuwa wameamua kujinufaisha wao kuweka mamishahara makubwa ili hali sisi wa Tanzania wengi tuna hali duni nyie hamnaga shukrani kabisa kuliona hilo Mshemiwa alijipunguzia mshahara na yeye .

Watumishi 1m kwa watu 59m hawawezi kuwa Grisi ya vyuma kukaza huo ni uongo mkubwa .
Tanzania na Magufuli ni Salama ,Chagua Magufuli Kazi Iendelee*Mitano Tena*
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…