Rais Magufuli ni lazima atetewe kwa nguvu zote dhidi ya udhalimu wowote

Umeandika vizuri na kwakirefu, hongera.

Umekiri kwenye bandiko lako kuwa Kuna maendeleo japo unasema sio kiviiiile. Angalau wewe unakiri.

Kufupisha habari, bandiko hili sio kuhusu uspesho wa Rais Magufuli bali kumtetea yeye na serikali yake dhidi ya udhalimu wanaofanyiwa kwa kuambiwa hawajafanya kitu. Kwavile umekiri Kuna vitu vimefanyika, nisaidie basi kuwaambia hao wenzako watafute hoja nyingine na sio kupinga kuwa hakuna kitu.

Asante kwa kuelewa na mjadala wa kuchambua kwa kina unahitaji uzi mwingine. Popote ulipo, agiza Pepsi ya bariiidi unywe mwanetu maana kukiri ukweli nayo ni ibada
 
Huwezi kufanya biashara kwenye mazingira yaliyopo kwasasa jiulize kwanini 'you can not plan business growth with uncertainty policy' huwezi kukuza biashara kwa sera za majukwaani
Sijajua uko sayari gani, wenzako wanafanya biashara na mambo yanaenda vizuri.

Tatizo ni ukitaka kuleta janjajanja, hapo hakuna rangi utaacha ona. Serikali inataka "win-win situation". Rais amefanya vikao na wafanyabiashara na wawekezaji ili kuboresha zaidi.

Tatizo watu walizoea konakona. Sasa hivi ni kufuata utaratibu.
#tulipekodikwamaendeleoyetu
 
You know nothing about the entrepreneur and his environments
 
Hatukatai ni rais lakin kua rais kwa kuonea watu, matukio ya hovyo hata ukifanya bahar iwe angani hautapendwa, tushachoka!!
 
Wawekezaji huwekeza sehemu yenye demokrasia kusiko na vigeugeu tumbua tumbua fukuza fukuza kwenye mfumo bora wa biashara hawataki kuwekeza kusiko na uhuru wa kutoa dukuduku zao.
Tanzania ni salama na demokrasia imetamalaki. Wawekezaji wanafurahi kuona watumishi wasiowaaminifu wanashughulikiwa. Hii inawapa imani zaidi ya usalama wa mitaji yao.
 
Naunga mkono hoja 100%

Jambo kubwa wanalokosea Ccm ni kudhani upendo unalazimishwa

Kumpenda Magufuli si lazima na sio uzalendo
Anayemkosoa ni mzalendo kuliko mnaokesha mkimwimbia mapambio.

Binafsi ninaamini Tanzania itapata maendeleo ya kweli siku ccm ikitolewa madarakani.

Mtetee wewe na familia yako ,,usituusishe kwny ujinga wako.
 
fazili, Mi namtetea kwenye haya unamwonea tu.
Kweli hawezi kuwa Malaika.

Ila Kama anajitahidi.
Tunamsuport kiaina upinzani mda mwingine inazingua.
Huwezi kupinga kila kitu.

Vingine fanya Kama huvioni.

Ni kutuzinguua wanachi tu[emoji4]
Umesema vizuri
 
Siku JPM akistaafu lazima ataingia kwenye kitabu Cha watu mashuhuri wa Karne hii.
 
Keshamaliza muda wake tusubiri na wengine
 
muna tuchosha na porojo zenu CCM ndio wanaotawala Tanzania na huu ni mwaka wao wa 59 sasa anza hapo
 
Hivi mbona watawala watangulizi hawakupenda kusifiwa hivi. Kwa nini utawala huu unataka na kung'ang'ania sana kusifiwa. Hivi hii ni nini sasa! Kuna nini? Yaani ushamba uliooneshwa juzi wa kuita wasanii na kutumia fedha zote hizo wakati mama zetu huku mavijijini hawana dawa na wanajifunika mashuka ambayo ni vitambaa walivyopewa na CCM ni ushamba kweli kweli.
 
Mshana kila jambo na wakati wake, tuko kwenye maandalizi ya kampeni. Tunajiandaa

Hakuna mwanadamu yeyote awaye yule ukijumuisha na ww asiyependa sifa
 
Mshana kila jambo na wakati wake, tuko kwenye maandalizi ya kampeni. Tunajiandaa

Hakuna mwanadamu yeyote awaye yule ukijumuisha na ww asiyependa sifa
Uko sawa lakini pia inategemea na aina ya sifa...Juzi japa Mchomvi karusha ngumi baada ya kusifiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…