Rais Magufuli ni lazima atetewe kwa nguvu zote dhidi ya udhalimu wowote

Kalagabaho
Nini maana ya upinzani? Kazi ya upinzani kwa Tanzania hasa Tanganyika lazima wapinzani wapinge kila kitu kwa sababu hakuna kinachofanywa na CCM kikakosa kasoro, vyote vya CCM vina mapungufu mengi ikiwemo ufisadi 10%kwenye miradi yote mikubwa.
 
Ndugu Bila Bila kwa mara nyingine tena unatoka bila bila.

Amin, Bokassa, Mobutu na Al Bashir hawa wote hawana sifa hata moja ya kuwalinganisha na Magufuli. Tafuta mfano mwingine. Hii ni mada ambayo ukitaka tunaweza kuichambua siku nyingine. Toa shaka mimi ni mwanahistoria mzuri.

Jenga hoja yako? Nini sio sahihi katika hili bandiko langu? Ungana nasi kumtetea Rais na serikali yake. Hii sio kwa manufaa yako binafsi. Fanya kama unafanya kwa nchi yako.

Karibu kwetu, sisi ni kundi kubwa, kundi la ushindi
Hoja kuu hakuna demokrasia hakuna uhuru wa kufanya siasa, wapinzani kubambikiwa kesi kupigwa risasi, wenye maduka ya kubadili pesa za kigeni kuporwa pesa zao, kununua Ndege kwa cash bei kubwa wajanja wachache wakala 10%
 
CIA na FBI waliopo ubalozi wa marekani hapo Dsm wanalo file lote juu ya Tukio la shambulio la Tundu lisu endelea kusubiria utapewa taarifa zote.
Minyoo, superb name hopefully imeishia tumboni haijapanda kwa kichwa.

Nyuzi za shambulio la mh. Lissu zipo, huu Ni uzi wa kueleza mazuri ya Rais Magufuli na serikali yake. Ni uzi wa kumtetea yeye na serikali yake dhidi ya udhalimu, uongo, uzindaki na siasa maandazi. Kama unapinga, pinga kwa hoja

Baki kwenye mada, baki njia kuu
 
Ninawasalimu ndugu zangu,

Uzalendo ni kuipenda nchi yako kwa dhati na kuwa tayari hata kufa ukiitetea. Nchi na serikali ni pande mbili za shilingi ileile/moja. Serikali iliyopo madarakani ndio inaongoza, kusimamia na kuratibu shughuli zote za kiuchumi, utamaduni na kijamii za nchi husika. Rais ndie taswira ya nchi. Mwalimu Nyerere alipata kusema " ukimtikisa Rais wa nchi, umeitikisa nchi".

Rais Magufuli amefanya mambo makubwa sana katika kipindi hiki kifupi cha miaka mitano. Pamoja na ukweli kuwa watangulizi wake walifanya kwa kadiri ya uwezo wao, Rais Magufuli ninaweza kusema amefanya na ziada. Mungu ampe maisha marefu yenye mafanikio kiongozi wetu huyu.

Marehemu mzee Mengi alikuwa akisema kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili watu wanaotaka kufanya biashara ni uthubutu. Uthubuti sio kwenye biashara tuu, ni kwenye kila jambo. Rais Magufuli anayo sifa hii adimu. Amethibitisha pasipo kuwa na hata chembe ya shaka kuwa yeye ni zawadi kwa watanzania.

Mzee huyu ni hodari, jasiri, msema kweli, mchapakazi, mfuatiliaji na zaidi sana, ni mzalendo kwelikweli.

Sekta zote za uchumi, kijamii na kiutamaduni amegusa. Angalia miundombinu, kilimo, afya, madini, elimu, utalii, uvuvi n.k. Mambo yameanza kukaa sawa. Tunahiy kumpa mzee wetu miaka mingine mitano ili atuvushe na kuendelea kutuheshimisha.

Hata kwa CCM, Kuna wakati ulikuwa hukatizi mitaani ukiwa na sare za chama. Binafsi ni muhanga wa kuzomewa na watu pale Arusha mjini mwaka 2013. Leo hii tunaona ufahari kuwa wanaCCM. Ukisafiroli nje ya Tanzania, watu wanatuambia nyie mnabahati sana kumpata Magufuli. Tunaheshimiwa sana huko nje. Pamoja na ukweli kuwa hafanyi haya yeye peke yake lakini yeye Kama kiongozi ndie mbeba maoni na dereva wetu. Mafanikio yanaakisi ndoto yake kwa nchi yake na maono yake.

Ninawaomba watanzania wore wazalendo bila kujali itikadi za vyama, dini au kabila, tumuunge mkono Rais Magufuli, tumtie moyo na kumuombea sana. Huyu ni lulu kwetu. Mimi binafsi, nitasimama na kumtetea Rais bila uoga wala aibu.

Ninawapongeza viongozi wa chama na serikali kwa kumsaidia Rais kuifikisha Tanzania hapa ilipo. Viongozi wa dini zote nao ninawashukuru kwa kusimama na Rais bila kujali matusi na dharau kutoka kwa waumini wao. Wamechagua fungu lililo jema. Tusiache kumuombea Rais ili tiendelee kuwa salama.

Nabii mara nyingi hapati heshima kwao, lakini tubadilike, tusisubiri mtu afe halafu ndio tuseme sifa zake nzuri. Haisaidii sana maana hasikii. Tuseme sasa, wakati ni sasa.
Subiri matusi sasa kutoka kwa waropokaji na wengi wao ambao kisomo chao kilikuwa cha kudandia dandia tu. Umahiri wao upo kwenye majungu na propaganda. Wanaona mafanikio lakini wamefumba macho. Wanakula na kusaza lakini wanalia njaa. Wanapeleka watoto wao kwenye shule za ghali lakini wanalialia kama kasuku. Wanategemea ruzuku kutoka kwa walipa kodi lakini kila uchwao wanawatukana walipa kodi ati hawakusoma kama wao. Watanzania badilikeni mpeni Kaizari yaliyo yake na mpeni Mungu utukufu wake. Jumapili njema.
 
Ubaguzi majimbo ya wapinzani kama alivyofanya juzi jimboni Rufiji kwa mh bwege
Hilo wasema wewe ila sijaona kosa Rais kuwaambia Raia wake ukweli kuwa walikosea kuchagua, walichagua Bwege.

Rais aliwaambia kuwa ziko fedha za mfuko wa jimbo na ile changamoto yao ilikuwa ndani ya uwezo aliyekuwa mbunge wao. Sasa kusema ukweli kunakuwaje ubaguzi?
 
Minyoo, superb name hopefully imeishia tumboni haijapanda kwa kichwa.

Nyuzi za shambulio la mh. Lissu zipo, huu Ni uzi wa kueleza mazuri ya Rais Magufuli na serikali yake. Ni uzi wa kumtetea yeye na serikali yake dhidi ya udhalimu, uongo, uzindaki na siasa maandazi. Kama unapinga, pinga kwa hoja

Baki kwenye mada, baki njia kuu
Wewe mbweha uwezo wako wa kufikiri umefika mwisho? Minyoo nipo tumboni mwako nimekutia njaa umejitoa fahamu zote na kumuona mtukufu ni mungu hana doa wala dhambi, kwa ufala wako unaona maendeleo yapo utazani ni pesa zako na zake toka mfukoni, Tambua maendeleo siyo Hisani za CCM, maendeleo ni pesa za walipa kodi na pesa nyingi inatumika kwa mambo ya hovyo hovyo kudidimiza demokrasia, kuwabambikia kesi kuwapiga risasi wapinzani badala ya maendeleo, pesa ilyopotelea huo ingekuwa imeingizwa kwenye maendeleo mda huu Tanzania ingekuwa ni Nchi tajiri kuliko South Africa, German , China na America kutokana na kumiliki rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani.
 
Hilo wasema wewe ila sijaona kosa Rais kuwaambia Raia wake ukweli kuwa walikosea kuchagua, walichagua Bwege.

Rais aliwaambia kuwa ziko fedha za mfuko wa jimbo na ile changamoto yao ilikuwa ndani ya uwezo aliyekuwa mbunge wao. Sasa kusema ukweli kunakuwaje ubaguzi?
Huwezi kuwapangia wananchi wa kumchagua kisa unaminya maendeleo makusudi kwa kuwakomoa wananchi huo ni Ubaguzi na dharau kubwa kwa wapiga kura.
 
Angalau sasa hoja zinaanza. Nimefurahi kuona uelewa wako mzuri kwenye mada hi ila mwisho umehitimisha kwa kunilisha maneno.

Ni kweli na nilisema hapo awali, mzalendo wa kweli ni yule ambaye yupo tayari kufa kwaajili ya nchi yake. Ila ni vyema kujiuliza, nchi ni nini hasa? Ni Rais?, ni mimi na wewe? Ni utamduni wetu? N nn hasa? Tafuta jibu.

Rais ndie kiongozi mkuu na taswira ya nchi. Yeye kiitifaki anaitwa raia namba moja. Yeye amebeba maono na ndoto za nchi, akitikisika, nchi imetikisika. Rais anapokuwa anatenda mambo ya maendeleo basil sisi raia was kawaida kumuunga mkono sio kujipendekeza, kumuunga mkono ni uzalendo.

Ninaomba utambue kuwa Rais Magufuli sio malaika na hajawa mtakatifu, anayo madhaifu na huo ndio ubinadamu. Nimeweka orodha ya mambo mazuri anayoifanyia Tanzania. Ungesema lipi ni la uongo?

Dhana ya kutetea inatokana na kundi la watu kuibuka na kupotosha ukweli wa mambo
Swali la msingi ni hilo: NCHI NI NINI?!

Kwa mujibu wa International Laws/laws of Nations, na kwa kuangalia Montevideo Convention (Uruguay) signed on December 26, 1933, States (not states) and Countries are one and the same... can be used interchangeably! Aidha, Artile I inasema:-
The state as a person of international law should possess the following qualifications: (a) a permanent population; (b) a defined territory; (c) government; and (d) capacity to enter into relations with the other states.
Kwahiyo, Rais kama sehemu ya serikali ni member of a State (not state), na mimi kama shemu ya population, am also a member of State!

Aidha, uzalendo wa mtu haupimwi kwa mambo aliyoyafanya bali unapimwa kwa jinsi anavyojitoa kuitetea na kuipigania nchi yake! Anachofanya JPM hakina tofauti yoyote na yale yanayofanywa na Watanzania wengine, wakiwa kama watumishi na viongozi wa umma, au raia wa kawaida!

JPM haja-sacrifice CHOCHOTE kile kufanya anachofanya! Mtu kama Mwalimu, ali-sacrifice ualimu wake na kwenda kuipigania TANU... ule ndo uzalendo! Wengine walivuka mpaka kwenda Uganda kupigana na Nduli Iddi Amini na kuhatarisha maisha yao, ingawaje walikuwa na uwezo wa kukacha... ule ndo uzalendo!!!

Again, Mwalimu aliacha u-PM ambao alihongwa na Wakoloni, u-PM ambao ungempa kila kitu, lakini akasema NO, I must fight for my Tanganyika... ule ndo Uzalendo!!!

Lakini unatumia kodi za wananchi kujenga barabara halafu unasema KAFANYA MAMBO MAKUBWA KWELI KWELI kuliko yeyote yule...c'mon man!!

Sasa nikija kwenye mada yako, naona umejikita sana kwenye hoja ya kwamba:
Rais Magufuli amefanya mambo makubwa sana katika kipindi hiki kifupi cha miaka mitano. Pamoja na ukweli kuwa watangulizi wake walifanya kwa kadiri ya uwezo wao, Rais Magufuli ninaweza kusema amefanya na ziada. Mungu ampe maisha marefu yenye mafanikio kiongozi wetu huyu.
Kwahiyo, kutokana na JPM kufanya mambo makubwa sana kuzidi hata wenzake, basi LAZIMA ATETEWE KWA NGUVU ZOTE!!

Kabla ya yote, hayo makubwa sana sana aliyofanya kuzidi hata wenzake ni yapi?!

Tuanze na suala la Uchumi wa Kati ambalo kwa sasa limekuwa Wimbo wa Taifa!

Mapema July World Bank waliingiza TZ kuwa ni miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati mdogo baada ya kufikia GNI per capita (By Atlas Method) ya USD 1080.

Hapa chini ni trend ya ukuaji wa GNI per capita kuanzia Awamu ya Mkapa hadi sasa! Kwavile JPM katumikia fully up to 2019, basi zifuatazo ni takwimu za kila mmoja kwenye miaka yake 4 ya kwanza:-
DNI-2.png

Utaona hapo juu, Mwinyi aliacha nchi mwaka 1995 ikiwa na DNI per capita ya USD 170, lakini miaka 4 baadae, Mkapa akaipandisha from $170 to $330 ikiwa ni ongezeko la $170.

Mkapa akaiacha nchi mwaka 2005 ikiwa na DNI per capita ya $500, lakini miaka 4 baadae, Kikwete akaipandisha from $500 to $670; AGAIN, ikiwa ni ongezeko la $170.

Kikwete akaiacha nchi mwaka 2015 ikiwa na GNI per capita ya $980, lakini miaka 4 baadae, Magufuli akaipandisha from $980 to $1080, likiwa ni ongezeko la ONLY $100 compared na wenzake ambao walipandisha kwa $170!

Sasa hicho alichofanya Magufuli kuwazidi wenzake ni kipi?!

Lakini hata ukija kwenye Foreign Reserve, huko nako hakuna maajabu makubwa ya kumfanya JPM eti awe ndo amefanya mambo ya ajabu kweli kweli kulinganisha na wenzake, na kwahiyo anastahili kutetewa kwa nguvu zote! Ripoti ya BoT ya mwaka 2016 inasema:-
BOT.png

Kwahiyo hapo unaona JK's final Fiscal Year aliacha ikiwa na USD 4.402 Billion ambayo ni zaidi ya TZS 9.6 Trillion! Hivi sasa nimepitia taarifa ya BoT, hawajataja, au labda niseme sikuona walipoandika exact figure ya 2019's fiscal year, ingawaje external source inasema by 2018, Foreign Reserve ilikuwa $5.05, an increase of ONLY 0.65 Billion compared na kile ambacho tulifunga nacho mwaka wa fedha wa 2015.

So, what's so special?! Kununua hizi ndege ambazo zinaitia hasara tu serikali, na matokeo yake, ili kukwepa zisikaguliwe na CAG, ile agency iliyomilikishwa ndege imehamishwa kutoka Wizara ya Uchukuzi to President's Office!!!

We all know ndege ni mradi uliokazaniwa binafsi na JPM mwenyewe kama ilivyokuwa kwa UDOM upande wa JK! Let's be honest here... hivi unaweza kulinganisha tija ya zile ndege na UDOM?!

What makes JPM that special?!

Aanatekeleza miradi ya ujenzi wa hospitali, zahanati na vituo vya afya kwa sababu zile zile ambazo nimeshaziongea sana hapa!!! Fungua makarabrasha yanayohusu MKUKUTA na humo utapata jibu! Again, what's so special kwa JPM?!

Kaingia madarakani na gia za kushughulikia mafisadi, na kwa mbwembwe kubwa, kile Kitengo cha Grand Corruption kikahamishwa kutoka Mahakama Kuu na tukaambiwa "Tumejenga Mahakama ya Mafisadi"!

Fine... tumejenga mahakama ya mafisadi lakini kila mtu anafahamu mafisadi wakubwa nchi hii ni high profile politicians and top government executives huku wakifanya ufisadi wao kwa kushirikiana na watu wa sekta binafsi kama akina Singasinga!!

Nitajie kiongozi mmoja Tu wa juu aliyefikishwa mahakamani na JPM kwa tuhuma za ufisadi!

Sote tumeshuhudia Andengenye na Lugola wakitangazwa kupiga pesa ya kutosha na watu wakafutwa kazi kabla ya miezi michache baadae hatujatangaziwa tena kusamehewa kwa Andengenye na kupewa kazi tena serikalini!

Again, what makes JPM that special ikiwa hata ile top cream ya mafisadi anachagua amshughulikie nani?!
 
Ninawasalimu ndugu zangu,

Uzalendo ni kuipenda nchi yako kwa dhati na kuwa tayari hata kufa ukiitetea. Nchi na serikali ni pande mbili za shilingi ileile/moja. Serikali iliyopo madarakani ndio inaongoza, kusimamia na kuratibu shughuli zote za kiuchumi, utamaduni na kijamii za nchi husika. Rais ndie taswira ya nchi. Mwalimu Nyerere alipata kusema " ukimtikisa Rais wa nchi, umeitikisa nchi".

Rais Magufuli amefanya mambo makubwa sana katika kipindi hiki kifupi cha miaka mitano. Pamoja na ukweli kuwa watangulizi wake walifanya kwa kadiri ya uwezo wao, Rais Magufuli ninaweza kusema amefanya na ziada. Mungu ampe maisha marefu yenye mafanikio kiongozi wetu huyu.

Marehemu mzee Mengi alikuwa akisema kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili watu wanaotaka kufanya biashara ni uthubutu. Uthubuti sio kwenye biashara tuu, ni kwenye kila jambo. Rais Magufuli anayo sifa hii adimu. Amethibitisha pasipo kuwa na hata chembe ya shaka kuwa yeye ni zawadi kwa watanzania.

Mzee huyu ni hodari, jasiri, msema kweli, mchapakazi, mfuatiliaji na zaidi sana, ni mzalendo kwelikweli.

Sekta zote za uchumi, kijamii na kiutamaduni amegusa. Angalia miundombinu, kilimo, afya, madini, elimu, utalii, uvuvi n.k. Mambo yameanza kukaa sawa. Tunahiy kumpa mzee wetu miaka mingine mitano ili atuvushe na kuendelea kutuheshimisha.

Hata kwa CCM, Kuna wakati ulikuwa hukatizi mitaani ukiwa na sare za chama. Binafsi ni muhanga wa kuzomewa na watu pale Arusha mjini mwaka 2013. Leo hii tunaona ufahari kuwa wanaCCM. Ukisafiroli nje ya Tanzania, watu wanatuambia nyie mnabahati sana kumpata Magufuli. Tunaheshimiwa sana huko nje. Pamoja na ukweli kuwa hafanyi haya yeye peke yake lakini yeye Kama kiongozi ndie mbeba maoni na dereva wetu. Mafanikio yanaakisi ndoto yake kwa nchi yake na maono yake.

Ninawaomba watanzania wore wazalendo bila kujali itikadi za vyama, dini au kabila, tumuunge mkono Rais Magufuli, tumtie moyo na kumuombea sana. Huyu ni lulu kwetu. Mimi binafsi, nitasimama na kumtetea Rais bila uoga wala aibu.

Ninawapongeza viongozi wa chama na serikali kwa kumsaidia Rais kuifikisha Tanzania hapa ilipo. Viongozi wa dini zote nao ninawashukuru kwa kusimama na Rais bila kujali matusi na dharau kutoka kwa waumini wao. Wamechagua fungu lililo jema. Tusiache kumuombea Rais ili tiendelee kuwa salama.

Nabii mara nyingi hapati heshima kwao, lakini tubadilike, tusisubiri mtu afe halafu ndio tuseme sifa zake nzuri. Haisaidii sana maana hasikii. Tuseme sasa, wakati ni sasa.
Viongozi wa kitaifa wenye tungo tata hujikaanga wenyewe
 
Hoja kuu hakuna demokrasia hakuna uhuru wa kufanya siasa, wapinzani kubambikiwa kesi kupigwa risasi, wenye maduka ya kubadili pesa za kigeni kuporwa pesa zao, kununua Ndege kwa cash bei kubwa wajanja wachache wakala 10%
Hivi unafikiri tumefikaje uchumi wa kati?
Kuna muda wa kila jambo. Siasa hazikuzuiwa ila siasa uchwara na zile za kupotezea watanzania muda wao wa kazi, hizo hapana.
Tunataka maendeleo zaidi na sio maneno zaidi
Sijajua bei ndogo unayoiongelea wewe Ni ipi? Kwani zilitakiwa zinunuliwe kwa bei gani?
Kuhusu maduka ya kubadili fedha za kigeni jua kuwa hatua iliyochukuliwa ilikuwa ya muhimu sana kwa usalama wa nchi linapokuja suala la fedha za kigeni. Wahujumu uchumi walikuwa wanatumia eneo hilo kama kichaka. Fika benki yoyote sasa itabadili fedha bila shida yoyote.
 
Ni nani atamtetea Rais anayewatesa raia anaowaongoza?

*Huduma za afya gharama zake ziko juu.
*Watumishi wa umma hawajaongezwa mshahara kwa miaka mitano.
*Watu wanauawa, kutekwa na kupotezwa kila uchao.
*Wakulima wananyang'anywa korosho utadhani wanaishi uhamishoni wakati wako kwenye nchi waliyozaliwa.
*Na kadhalika, na kadhalika.
A Country is not a company
 
Nchi ina zaidi ya miaka 50 haina maendeleo, pesa nyingi inapotelea kwenye kudidimiza demokrasia mambo yasiyo na Tija kwa Taifa, kwa rasilimali zilizopa Tanzania ilipaswa iwe makao makuu ya UN ni Nchi yenye utajiri mkubwa lakini chini ya CCM hakuna kinachofanyika zaidi ya ufisadi usiokwisha, mda huu Tanzania ilipaswa iwe na viwanda kila kata, vyuo vikuu kila wilaya, Hosptal za rufaa kubwa zenye madaktari Bingwa za kimataifa kila mkoa mpaka Nchi zingine waje kutibiwa Tanzania, barabara nzuri vijijini kote kwenye mazao, daraja toka Dsm mpaka Zanzibar na pemba, hata CCM isingekuwa inatumia nguvu kubwa kuomba kura, maendeleo yenyewe yangejielezea kinagaubaga, CCM kimekuwa chama cha kudidimiza demokrasia hawataki kukosolewa wanatumia pesa nyingi kurejesha mfumo wa chama kimoja, kwa mfumo huu itachukua miaka 200 Tanzania kupata maendeleo.
 
Hivi unafikiri tumefikaje uchumi wa kati?
Kuna muda wa kila jambo. Siasa hazikuzuiwa ila siasa uchwara na zile za kupotezea watanzania muda wao wa kazi, hizo hapana.
Tunataka maendeleo zaidi na sio maneno zaidi
Sijajua bei ndogo unayoiongelea wewe Ni ipi? Kwani zilitakiwa zinunuliwe kwa bei gani?
Kuhusu maduka ya kubadili fedha za kigeni jua kuwa hatua iliyochukuliwa ilikuwa ya muhimu sana kwa usalama wa nchi linapokuja suala la fedha za kigeni. Wahujumu uchumi walikuwa wanatumia eneo hilo kama kichaka. Fika benki yoyote sasa itabadili fedha bila shida yoyote.
Uchumi wa kati umefikiwa kwa nguvu za mkapa na kikwete huyo mtukufu kakutia muendelezo tu wa yale waliyoyaandaa vizuri.
 
Ninawasalimu ndugu zangu,

Uzalendo ni kuipenda nchi yako kwa dhati na kuwa tayari hata kufa ukiitetea. Nchi na serikali ni pande mbili za shilingi ileile/moja. Serikali iliyopo madarakani ndio inaongoza, kusimamia na kuratibu shughuli zote za kiuchumi, utamaduni na kijamii za nchi husika. Rais ndie taswira ya nchi. Mwalimu Nyerere alipata kusema " ukimtikisa Rais wa nchi, umeitikisa nchi".

Rais Magufuli amefanya mambo makubwa sana katika kipindi hiki kifupi cha miaka mitano. Pamoja na ukweli kuwa watangulizi wake walifanya kwa kadiri ya uwezo wao, Rais Magufuli ninaweza kusema amefanya na ziada. Mungu ampe maisha marefu yenye mafanikio kiongozi wetu huyu.

Marehemu mzee Mengi alikuwa akisema kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili watu wanaotaka kufanya biashara ni uthubutu. Uthubuti sio kwenye biashara tuu, ni kwenye kila jambo. Rais Magufuli anayo sifa hii adimu. Amethibitisha pasipo kuwa na hata chembe ya shaka kuwa yeye ni zawadi kwa watanzania.

Mzee huyu ni hodari, jasiri, msema kweli, mchapakazi, mfuatiliaji na zaidi sana, ni mzalendo kwelikweli.

Sekta zote za uchumi, kijamii na kiutamaduni amegusa. Angalia miundombinu, kilimo, afya, madini, elimu, utalii, uvuvi n.k. Mambo yameanza kukaa sawa. Tunahiy kumpa mzee wetu miaka mingine mitano ili atuvushe na kuendelea kutuheshimisha.

Hata kwa CCM, Kuna wakati ulikuwa hukatizi mitaani ukiwa na sare za chama. Binafsi ni muhanga wa kuzomewa na watu pale Arusha mjini mwaka 2013. Leo hii tunaona ufahari kuwa wanaCCM. Ukisafiroli nje ya Tanzania, watu wanatuambia nyie mnabahati sana kumpata Magufuli. Tunaheshimiwa sana huko nje. Pamoja na ukweli kuwa hafanyi haya yeye peke yake lakini yeye Kama kiongozi ndie mbeba maoni na dereva wetu. Mafanikio yanaakisi ndoto yake kwa nchi yake na maono yake.

Ninawaomba watanzania wore wazalendo bila kujali itikadi za vyama, dini au kabila, tumuunge mkono Rais Magufuli, tumtie moyo na kumuombea sana. Huyu ni lulu kwetu. Mimi binafsi, nitasimama na kumtetea Rais bila uoga wala aibu.

Ninawapongeza viongozi wa chama na serikali kwa kumsaidia Rais kuifikisha Tanzania hapa ilipo. Viongozi wa dini zote nao ninawashukuru kwa kusimama na Rais bila kujali matusi na dharau kutoka kwa waumini wao. Wamechagua fungu lililo jema. Tusiache kumuombea Rais ili tiendelee kuwa salama.

Nabii mara nyingi hapati heshima kwao, lakini tubadilike, tusisubiri mtu afe halafu ndio tuseme sifa zake nzuri. Haisaidii sana maana hasikii. Tuseme sasa, wakati ni sasa.
Huwezi kufanya biashara kwenye mazingira yaliyopo kwasasa jiulize kwanini 'you can not plan business growth with uncertainty policy' huwezi kukuza biashara kwa sera za majukwaani
 
Wawekezaji huwekeza sehemu yenye demokrasia kusiko na vigeugeu tumbua tumbua fukuza fukuza kwenye mfumo bora wa biashara hawataki kuwekeza kusiko na uhuru wa kutoa dukuduku zao.
 
Back
Top Bottom