Ninawasalimu ndugu zangu,
Uzalendo ni kuipenda nchi yako kwa dhati na kuwa tayari hata kufa ukiitetea. Nchi na serikali ni pande mbili za shilingi ileile/moja. Serikali iliyopo madarakani ndio inaongoza, kusimamia na kuratibu shughuli zote za kiuchumi, utamaduni na kijamii za nchi husika. Rais ndie taswira ya nchi. Mwalimu Nyerere alipata kusema " ukimtikisa Rais wa nchi, umeitikisa nchi".
Rais Magufuli amefanya mambo makubwa sana katika kipindi hiki kifupi cha miaka mitano. Pamoja na ukweli kuwa watangulizi wake walifanya kwa kadiri ya uwezo wao, Rais Magufuli ninaweza kusema amefanya na ziada. Mungu ampe maisha marefu yenye mafanikio kiongozi wetu huyu.
Marehemu mzee Mengi alikuwa akisema kuwa moja ya changamoto kubwa inayowakabili watu wanaotaka kufanya biashara ni uthubutu. Uthubuti sio kwenye biashara tuu, ni kwenye kila jambo. Rais Magufuli anayo sifa hii adimu. Amethibitisha pasipo kuwa na hata chembe ya shaka kuwa yeye ni zawadi kwa watanzania.
Mzee huyu ni hodari, jasiri, msema kweli, mchapakazi, mfuatiliaji na zaidi sana, ni mzalendo kwelikweli.
Sekta zote za uchumi, kijamii na kiutamaduni amegusa. Angalia miundombinu, kilimo, afya, madini, elimu, utalii, uvuvi n.k. Mambo yameanza kukaa sawa. Tunahiy kumpa mzee wetu miaka mingine mitano ili atuvushe na kuendelea kutuheshimisha.
Hata kwa CCM, Kuna wakati ulikuwa hukatizi mitaani ukiwa na sare za chama. Binafsi ni muhanga wa kuzomewa na watu pale Arusha mjini mwaka 2013. Leo hii tunaona ufahari kuwa wanaCCM. Ukisafiroli nje ya Tanzania, watu wanatuambia nyie mnabahati sana kumpata Magufuli. Tunaheshimiwa sana huko nje. Pamoja na ukweli kuwa hafanyi haya yeye peke yake lakini yeye Kama kiongozi ndie mbeba maoni na dereva wetu. Mafanikio yanaakisi ndoto yake kwa nchi yake na maono yake.
Ninawaomba watanzania wore wazalendo bila kujali itikadi za vyama, dini au kabila, tumuunge mkono Rais Magufuli, tumtie moyo na kumuombea sana. Huyu ni lulu kwetu. Mimi binafsi, nitasimama na kumtetea Rais bila uoga wala aibu.
Ninawapongeza viongozi wa chama na serikali kwa kumsaidia Rais kuifikisha Tanzania hapa ilipo. Viongozi wa dini zote nao ninawashukuru kwa kusimama na Rais bila kujali matusi na dharau kutoka kwa waumini wao. Wamechagua fungu lililo jema. Tusiache kumuombea Rais ili tiendelee kuwa salama.
Nabii mara nyingi hapati heshima kwao, lakini tubadilike, tusisubiri mtu afe halafu ndio tuseme sifa zake nzuri. Haisaidii sana maana hasikii. Tuseme sasa, wakati ni sasa.