Rais Magufuli nisikilize kwa makini, Sitaki upoteze muda bure

Rais Magufuli nisikilize kwa makini, Sitaki upoteze muda bure

Mbona umerudia rudia sana? Aya 2/3 zingetosha, ...
Hawa wana lao wanalolitafuta nje ya ushauri wake, fikra na maono yake kwamba angefupisha kwa aya 2-3 asingeonekana katika fikra za mshuriwa.
 
Staili ya Uandishi wa Paskalli ni ya kipekee, siyo ya kurukia kwa mbwembwe( jokes)
 
Dogo usitarijie vijana wa Lumumba wakusupport hata kdg, pia huwa wanasoma vipandevipande lkn wasamehe bure ndio upeo wao ulipokomea!
 
Ujumbe wako ni wa kufikirisha sana ,sijui kama wahusika watakuwa na muda ya kusoma na kuelewa ujumbe huu!!Wachina wanakuja na kuanzisha shuhuri za kiuchumi ambazo vijana wetu wanaziweza lakini hawana mtaji halafu tunalalamika kuwa vijana wetu hawana ajira! Mfano ni haya magarage ya magari yanayomilikiwa na machina lakini wanaajiri vijana wetu ambao ndio wanafanya kazi zote kwa ujira kiduchu! Hawa machina wanapata fedha nyingi kutokana na kazi hizo na fedha yote inakwenda China kwani serikali yao inawapa mikopo kuja kuchuma huku; kwanini tunawapa vibali wageni kwa shuhuri ambazo sisi tunaziweza kwa kuwawezesha vijana wetu toka NIT wakazifanya? Mipango yetu ni mibaya hasa kwenye Elimu tunayotoa haiendani na matakwa ya jamii!!ikitisha

Mkuu mambo haya yanasikitisha sana.
 
Una point lakini unalalamika sana hujengi hoja ikajitokezA umetumia neno HUWEZI zaidi ya mara 20 kwenye andiko lako.

Hoja hujaiona Mkuu

Basi ulikuwa husomi bali umeparamia andiko.

Au ulitaka ni underline kama mtoto wa Sekondari, 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Wewe ndio ukasome tena.

Wapi hujaelewa?
Hakuna taifa linaloendelea dunia kwa kutegemea watu wake wa ndani pekee, wapi hujaelewa wewe?

Hata wewe binafsi, fanya kazi ufanyavyo kwa bidii zote, huwezi kuwa tajiri kwa kujitumikisha mwenyewe, lazima utumikishe wengine. Bado hujanielewa na hapa
Kabla ya hamjafikiria kutumikusha raia wa nchi nyingine sijui ili mpige hatua kimaendeleo.

Toeni majibu ni kwanini MAZAO YOTE kama Kahawa, Korosho, Mbaazi na Katani ambayo tayari yalikuwa yameonesha DALILI ZOTE za kumkomboa Mkulima na kuongeza pato la taifa kwa kuingiza nchini BILLIONS OF DOLLARS Kwanini MMEYAUA ???????


Nchi hii hakuna mtawala ajayefikiria kuendeleza nchi hii wala kuwasaidia raia wao kupiga hatua.

Vijimaendeleo unavyoviona ni either Kwasababu ya 10 percent wanayotaka kuchuma au ni mbwembwe tu za kama za housegirl kumpaka mtoto uji mdomoni ili aonekane kanywa wakati uji wote kanywa yeye.

Ni nani anakula KEKI YA TAIFA ???

Tanzania ina watu karibu Milioni 60, serikali yenyewe imeajiri watu Laki 5 tu na imeshindwa kuwadumia ( wengi wana mishahara Laki 5 na mafao yao baada ya kutumikishwa ni mbinde kuyapata )

Watanzania wengine kila mmoja anaishi kama mtoto wa bata.

Hivi ulishagundua ndani ya Taifa hili wenye akili hawatakiwi ?

Hatuwataki kina Zitto, Lissu, Kabendera, Fatma Karume etc

Tunawataka kina Musiba, Musukuma, Mchange, Babu Tale, Mlinga, Kibajaji.

Badi hujauona tu mwelekeo wa taifa hili ??????

Target siyo maendeleo, target yao ni ni kushikilia MADARAKA kadri ya uwezo wao na kuwarithisha watoto wao kama ilivyotokea Zanzibar.

Zingine ni ziada tu.
 
Wewe ndio ukasome tena.

Wapi hujaelewa?
Hakuna taifa linaloendelea dunia kwa kutegemea watu wake wa ndani pekee, wapi hujaelewa wewe?

Hata wewe binafsi, fanya kazi ufanyavyo kwa bidii zote, huwezi kuwa tajiri kwa kujitumikisha mwenyewe, lazima utumikishe wengine. Bado hujanielewa na hapa
Si kweli china imeendelea kwa kutumikisha wananchi wake mpaka leo hii. Hata wewe unaweza kuendelea ukijitumikisha wewe mwenyewe kufanya kazi yako ya kujiajiri kisha kuwauzia watu wenye uhutaji na bidhaa zako. Ulikuwa hujuwi hili?
 
Kweli wewe bado mtoto mdogo. Ujeruman, China na Korea Kaskazini ziko hapo zilipo kwa juhudi za watu kufanya kazi kwa bidii.

Mao aliwachimbisha wachina visima vya mafuta hila ya mitambo.

Hitler aliwakusanya wasomi na kuwaweka kambini kisha kuwaamuru watengeneze mitambo ama mifumo kulingana na taaluma zao.

Kasome tena kisha urudi hapa.
Zipo njia nyingi za kutumikisha taifa jingine
1. Politically
2. Economically
3. Physiologically
4. Physically

Yupo sahihi kabsa kuna njia tofauti kila taifa linatumia kunufaika na taifa jingine
 
Bandiko refu sana ungeweza kuandika fupi tu na ujumbe wako ungeeleweka, umerudia rudia mno maneno. Ushuri wako sijui unalenga nini maana unachokidai hapa mbona ndicho kinachofanyika? Hivi hya makampuni ya kigeni mfano yanyojenga SGR, Nyerere george, daraja la Busisi wewe huyaoni? Au unataka tuwateke watu waje tuwatumikishe halafu sisi tuwe wanyapra?
 
Ndio maaana CANADA walinipaga VISA kilaini sana, kumbe walitaka wakanitumikishe kama Wazanzibar wanavyowahenyesha wanyamwezi pale Unguja.
 
Utafikiaje hatua ya Nchi zingine kukutajirisha bila kujenga miundombinu/mazingira husika!!?

1.Ndio maana zinanunuliwa ndege watu wa nje waje kututajirisha kwa kutalii
2. Ndio maana inajengwa 'stiglaaz goji' mw2113 ili wageni waje wajenge viwanda kwa faida yetu.
3. Ndio maana Inajengwa 'standadi geji' reli na bomba la mafuta La Uganda ili Nchi nyingine jirani zipitishie hapa mizigo zitutajirishe!
4. Nakadhalika nakadhalika!

NASEMA UONGO NGUGU ZANGU?!
 
Back
Top Bottom