Wewe ndio ukasome tena.
Wapi hujaelewa?
Hakuna taifa linaloendelea dunia kwa kutegemea watu wake wa ndani pekee, wapi hujaelewa wewe?
Hata wewe binafsi, fanya kazi ufanyavyo kwa bidii zote, huwezi kuwa tajiri kwa kujitumikisha mwenyewe, lazima utumikishe wengine. Bado hujanielewa na hapa
Kabla ya hamjafikiria kutumikusha raia wa nchi nyingine sijui ili mpige hatua kimaendeleo.
Toeni majibu ni kwanini MAZAO YOTE kama Kahawa, Korosho, Mbaazi na Katani ambayo tayari yalikuwa yameonesha DALILI ZOTE za kumkomboa Mkulima na kuongeza pato la taifa kwa kuingiza nchini BILLIONS OF DOLLARS Kwanini MMEYAUA ???????
Nchi hii hakuna mtawala ajayefikiria kuendeleza nchi hii wala kuwasaidia raia wao kupiga hatua.
Vijimaendeleo unavyoviona ni either Kwasababu ya 10 percent wanayotaka kuchuma au ni mbwembwe tu za kama za housegirl kumpaka mtoto uji mdomoni ili aonekane kanywa wakati uji wote kanywa yeye.
Ni nani anakula KEKI YA TAIFA ???
Tanzania ina watu karibu Milioni 60, serikali yenyewe imeajiri watu Laki 5 tu na imeshindwa kuwadumia ( wengi wana mishahara Laki 5 na mafao yao baada ya kutumikishwa ni mbinde kuyapata )
Watanzania wengine kila mmoja anaishi kama mtoto wa bata.
Hivi ulishagundua ndani ya Taifa hili wenye akili hawatakiwi ?
Hatuwataki kina Zitto, Lissu, Kabendera, Fatma Karume etc
Tunawataka kina Musiba, Musukuma, Mchange, Babu Tale, Mlinga, Kibajaji.
Badi hujauona tu mwelekeo wa taifa hili ??????
Target siyo maendeleo, target yao ni ni kushikilia MADARAKA kadri ya uwezo wao na kuwarithisha watoto wao kama ilivyotokea Zanzibar.
Zingine ni ziada tu.